Eddo na wenzie walipokea fedha kututoa kwenye reli?

xx
xx
GSM wamejimilikisha Timu, utopolo ni Mazuzu
Makolo mnapenda sana kujifariji! Blanda ya kuuza 49% ya hisa za klabu kwa 20B bado inawatafuna na matokeo yake mnajaribu kuonesha kila linalofanyika kwa Yanga ni blanda kama ile ya kwenu!!

Ngoja niwaulize!! Kwani cha ajabu ni kipi pale?! Ina maana hamfahamu GSM wana mkataba wa kutengeneza jezi tangu kitambo?!

Au niwakumbushe kwamba wakati Mwamedi alipoikuta Simba ipo taabani, akatumia mwanya huo kununua 49% kwa bei chee kwa sababu alifahamu kwa njaa ambayo mlikuwa nayo, KATU MSINGEKATAA!

Kinyume chake, GSM alipoikuta Yanga ipo taabani wala hakutaka ku-take advantage bali akaamua kufanya nao biashara ya kutengeneza jezi!!

Ngoja niwakumbushe habari ya September 07, 2019 ambayo inasema:-
Kampuni nyingine ni GSM walioshinda tenda ya uuzaji wa jezi za Yanga iliyotoa Sh bilioni 1.3, pia kampuni hiyo imeongeza fedha kwa kutoa Sh milioni 150 ya udhamini kupitia magodoro yao ya GSM.
2019 Yanga ilikuwa njaa tupu, lakini GSM akaamua kufanya nao biashara badala ya kujimilikisha timu kama alivyofanya Mwamedi!

Halafu ona mlivyo kiroja!! Kutoka kwenye website yenu wenyewe, Da' Barbara anawajuza:-
Klabu ya Simba imeisaini mkataba wa miaka miwili na kampuni ya Vunjabeigroup wa kutengeneza na kusambaza jezi za timu ya wakubwa, wanawake na vijana wenye thamani ya Sh bilioni mbili.
Yaani mnajaribu kukejeli mkataba wa Sh 1.8 Billion kwa mwaka wakati wa kwenu ni 1.0 Billion kwa mwaka... like serious?! Utamu zaidi, huyo anayelipa 1.8 Billion kwa mwaka bado huwa anafanya mambo mengi zaidi kwa klabu kuliko huyo mwenye mkataba wa 1 Billion kwa mwaka!!

But wait... GSM analipa 300M kwa mwaka ili kutangaziwa biashara zake! Hivi mnaweza kutuambia yale mapicha ya mabox ya sabuni ambayo Mwamed kayajaza kwenye mafulana yenu huwa analipa kiasi gani?!
 
Acheni wapige hela, mkiambiwa kuchangia hela mnaufyata. Ila kupiga kelele ndiyo mnaweza.
 
Kama Yanga aliyeingia mkataba wa jezi kwa 1.8 Billion kwa mwaka ni Magumashi... na vipi kuhusu Makolo ambao mkataba wao ni 1.0B kwa mwaka?!

Kama Yanga aliyeingia mkataba wa udhamini wa 300M kwa mwaka ni magumashi, hivi unaweza kutueleza Mwamedi anawalipa shilingi ngapi yale mapicha picha ya viroba vya unga alizoweka kwenye jezi za Makolo?

Hata kama ni kweli Rage alisema Mashabiki wa Simba ni Mbumbumbu, ndo mshindwe kutumia akili japo kidogo kujua huu ni mchana na huu ni usiku?!

Yanga walikuwa na sababu zipi za kuwatumia akina Edo kuwatoa watu kwenye reli kwa jambo ambalo wenyewe waliamua kuliweka public?!

Wameita Waandishi wa Habari, na wakajitokeza!!

Yanga wenyewe wame-post kwenye page yao! Acting CEO amepost kwenye page yake! Manara nae ka-post! Lakini pamoja na yote hayo, Kazumari anawaambia Edo katumika kuwatoa kwenye reli, nanyi mnakubali tu bila kujiuliza HOW!!

Ama kweli Rage hakukosea!!
 
Kama ambavyo "Mwamedi" amejimilikisha timu ya makolo, na mpaka leo hawajui bilioni 20 ilienda wapi. Makolo ni mbumbumbu!
Nabado anawaambia ametoa fweza nyingi mfukoni kuiwezesha timu wakati hata msemaji wa klabu alikua halipwi zaidi ya kuvolunteer tu.
 
Nimekuelewa Chief uliposema kuwa Simba SC wakiuza Timu kwa MO nao wanaiga kwa kuuza Timu kwa GSM

Walipiga sana kelele.. Lakini kumbe nimegundua Simba SC ndo mchonga njia..!
 
Wa makolo kabla.ya mkataba si walitoa nafasi ya wenye uwezo wa kuweza kutengeneza jezi na vifaa vingine wapeleke ofa zao.?.au hukua hai kipindi kile. ? Na huu wa leo wa yanga wapi walitangaza kuhitaji mzabuni.?
 
NazaninLuc Emely alikua sahihi zaidi alipo waita manyani na manara akiposema hamnazo alikua sahihi 100% hayo yoote mbona yanaelezewa na watendani wa simba.. matabgazo ya Mo analipia au hujui .?. Uwe na muda wa kuuliza kabla.hauja andika huu upuuzi wako.
 
Ww binti kazumari ni takataka sana
 
Wa makolo kabla.ya mkataba si walitoa nafasi ya wenye uwezo wa kuweza kutengeneza jezi na vifaa vingine wapeleke ofa zao.?.au hukua hai kipindi kile. ? Na huu wa leo wa yanga wapi walitangaza kuhitaji mzabuni.?
Ni kama ambavyo Rage alivyowaita kwamba ni Mbumbumbu, na umbumbumbu wako umeuthibitisha hapa kwa kushindwa kujibu swali dogo sana!! Nimeuliza analipa NGAPI... JIBU SWALI HILO!!

GSM kaweka wazi kwamba ni Sh 300M kwa mwaka, with an annual increment of 10%... Mwamedi ngapi?!
 
Mbumbumbu anaweza kuwa mwerevu akipewa maarifa ila wapumbavu hao ni mgando kabsa yaani wajima manyani hawabadiliki kamwe
 
Mbumbumbu anaweza kuwa mwerevu akipewa maarifa ila wapumbavu hao ni mgando kabsa yaani wajima manyani hawabadiliki kamwe
Duh... POVU MAX, na mitusi juu!!

In short, Mbumbumbu huna jibu, whichi means unapiga kelele kwa jambo usilolijua!! Oh, GSM hivi, mara GSM vile kumbe hata hujui huyo Mwamedi analipa shilingi ngapi kuweka yale makorokoro yake kwenye jezi zenu!!

Anyway, busara zinanishawishi nikupuuze lakini hata akiulizwa mtoto wa darasa la pili, mara moja atafahamu ni nani mpumbavu kati yangu na wewe...
 
Kazumari himself, I like the guy, namuelewa sana.
 
Hivi kuna tusi hapo juu.? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£ 1300 kwa uzi mmoja 🀣🀣🀣 ukitoa wale wawili walio bakia wote ni buree kabisaaa yaani hamnazo
 
Hivi kuna tusi hapo juu.? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£ 1300 kwa uzi mmoja 🀣🀣🀣 ukitoa wale wawili walio bakia wote ni buree kabisaaa yaani hamnazo
Jibu ulichoulizwa, kama huna jibu, PIGA KIMYA!!
 
Sie mashabiki tunataka timu yetu ishinde tu basi, mbona nyie MO kamiliki timu yenu kila kitu na mpaka sasa hamfaham kama bil 20 zimetoka au bado.Jezi yenu bidhaa zimejaa na anafanya atakavyo Ile MO Foundation mpaka inokosa sehemu ikawekwa nyuma,mkivaa jezi ile MO Foundation kama haipo makalioni basi ipo kiunoni kama shanga.
 
Una smartphone au laptop ya kazi gani ingia tafuta taarifa zipo.
 
Man, huko kwenye 20B umeenda mbali mno!! Hapa wanabwabwaja kuhusu Mkataba wa Jezi huku wakisahau kwamba ule wa Yanga wanaoita tunapigwa ni 1.8 Billion kwa mwaka, wakati wa kwao ni 1B kwa mwaka!!

Wanabwabwaja kuhusu udhamini wa 300M wakati wao HAWAFAHAMU Mwamedi yale makolo kolo aliyoyajaza kwenye jezi zao analipia shilingi ngapi... HAWAJUI!!

Mara oh, Hersi Said ni mwajiriwa wa GSM huku wakisahau kwamba Barbara nae ni Mwajiriwa wa Mwamed...

Mbaya zaidi, wala hawafahamu kwamba Hersi amechaguliwa na Wanachama, na kwahiyo anaweza kuondolewa na Wanachama wakati Wanachama wa Makolo HAWANA UBAVU wa kumtoa Barbara!!

Yaani Chenga+
 
Yanga tunataka honest sale ya shares , hatutaki magumashi.
Kama GSM wamejimilikisha hisa za club kinyemela imekula kwao tutaenda mahakamani kuzidai.

Yanga ni dude kubwa sana , hawa GSM wasidhani wanaweza kulipata kwenye sahani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…