EDO: Kama Simba walihujumiwa kwanini wamemfukuza kocha?

EDO: Kama Simba walihujumiwa kwanini wamemfukuza kocha?

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
EDO: SIMBA KUMFUKUZA KOCHA NI KUWEWESEKA NA KIPIGO.

"Majuzi Simba wamefungwa bao tano na watani zao,nimekumbuka mengi.Nadhani lilikuwa ni hitimisho la anguko lao dhidi ya watani wao.Kipimo cha maendeleo ya Simba sio Yanga,lakini unahitaji kuangalia kwa umakini mwenendo wa mtani wako kwaajili ya kujijenga kesho yako iliyo salama zaidi"

"Simba waliidharau Yanga wakati inajijenga.Simba walilewa na utawala wao wa miaka ya hivi karibuni..Simba walimdharau Hersi,wakaidharau na Yanga wakati ikiendelea kujitafuta"

"Simba walibeza hata Yanga kufika Fainali za Kombe la Shirikisho barani Afrika.Ule mda wa madaraka ni mtamu.Simba walikuwa katika madaraka ya soka la nchi hii kwa miaka minne mfululizo halafu na wakasahau kuidharau Yanga"

"Leo Simba wamefungwa mabao matano na Yanga na anasakwa mchawi. Mtu wa kwanza kutolewa kafara ni Kocha Robertinho.Ameondoka.Ameshakwenda kwao"

"Inadaiwa kwamba kuna wachezaji wanashutumiwa kuwa waliihujumu mechi,Kama unaamini kuna wachezaji wamehujumu mechi kwanini umfukuze Kocha? Hapo hapo Mwenyekiti wa Simba,Murtaza Mangungu naye anatuhumiwa kuhusika na kipigo.Swali kipigo kilitokana na Robertinho, wachezaji au Mangungu? Nadhani huku kote ni kuweweseka tu"

EDO KUMWEMBE via MWANASPOTI.

#FutbalPlanetUpdates
1699964250967.jpg
 
Unaamini kweli mechi iliuzwa??
Iliuzwa na nani???

Coz Kila mtu pale ukoloni.....ni Simba dam dam
Ni kweli iliuzwa,Yanga waliwapa pesa wachezaji kadhaa wa Simba,ndio waliouza mechi,kocha aliyetimuliwa analijua hilo na alitaka kusema,wakamuwahi kwa kumtimua ili viongozi walioshiriki hiyo dhambi wasiabike asilani,upo bloangu??
 
Kwanin mnajua hili....msiende TAKUKURU coz waziri aliwakaribisha pale mkashtaki
 
"Leo Simba wamefungwa mabao matano na Yanga na anasakwa mchawi
Wakati mnachambua huo ujinga wenu Simba ipo ndani ya team 10 bora Africa.

Endeleeni na uchambuzi wenu usio na tija kwenu na mashabiki wote wa Uto.

Simba ni wababe na wataendelea kuwa wababe hata kama mliwafunga 5 kamwe hamjauzima ubabe wa Simba.

Rais wenu anajua kuwa bado hajaifikia na hataifikia Simba akiwa rais.

Kama huamini mpigie kisha atakuambia ukweli.
 
Walimfukuza ili asisanue ukweli kuhusu huko kuuzwa kwa hiyo mechi,kwani akiwa nje hata akisema wasioelewa watamchukulia kama anaropoka tu kwa kuwa ameshatimuliwa
Una akili,kama anajua wachezaji waliuza match kulinda career yake ya soka ilibidi ndio aseme sasa kufukuzwa kwake alionewa ila wachezaji waliuza ile match
20231113_210256.jpg
 
Wakati mnachambua huo ujinga wenu Simba ipo ndani ya team 10 bora Africa.

Endeleeni na uchambuzi wenu usio na tija kwenu na mashabiki wote wa Uto.

Simba ni wababe na wataendelea kuwa wababe hata kama mliwafunga 5 kamwe hamjauzima ubabe wa Simba.

Rais wenu anajua kuwa bado hajaifikia na hataifikia Simba akiwa rais.

Kama huamini mpigie kisha atakuambia ukweli.
Timu bora zipi master? 😂
20231113_191700.jpg
 
Wakati mnachambua huo ujinga wenu Simba ipo ndani ya team 10 bora Africa.

Endeleeni na uchambuzi wenu usio na tija kwenu na mashabiki wote wa Uto.

Simba ni wababe na wataendelea kuwa wababe hata kama mliwafunga 5 kamwe hamjauzima ubabe wa Simba.

Rais wenu anajua kuwa bado hajaifikia na hataifikia Simba akiwa rais.

Kama huamini mpigie kisha atakuambia ukweli.
Hatujakataa Hilo mkuu

Lkn jibuni swali la Edo kumwembe
"Swali kipigo kilitokana na Robertinho, wachezaji au Mangungu?
 
Back
Top Bottom