Mayele yupo Egypt lakini ki uhalisia Bado yupo Tanzania, Mayele mafanikio na Heshima kubwa katika soka la ndani na nje ya Nchi ameyapata Tanzania.
Kule Drc Mayele alikua maarufu lakini Kwa level yake pale Drc wapo wengi na wamepita wengi katika ligi ya Drc kwaiyo alikua wakawaida Sana.
Mayele amejenga jina akiwa Tanzania uku akimfunika mkongo man Mwenzake Makambo ,Mayele alijituma Sana yeye na wenzake wakafanya mambo makubwa Yanga yeye akiwa kinara.
Kwa ujumla Yanga ya kimataifa ili Bebwa na Mayele na umaarufu wake uka (backfire) mpaka timu ya Taifa ya Congo na kwa wakongomani wote.
Bahati mbaya Amekwenda nchi ambayo lugha haziendani, tamaduni mpya na timu ambayo Haina umaarufu ya pyramid.
Kule watu hawaishi kama Bongo, mdawote mko Avic na washikaji/wachezji wenzako, kule mkitoka mazoezini kilamtu ki vyake kama Ulaya, Sasa Mayele anakua mpweke kwakua muda mwingi ata( chill)na familia yake tu.
Kwaiyo anarudi mtandaoni na kupiga stori na watu wake wa karibu ambao wengi ni wa Tanzania, kwakua anaongea na kuelewa kiswahili, ameshindwa kuwa na washikaji wengi kule misri kwakua tamaduni ziko tofauti Bora ya Drc na TZ zina fanana.
Anafuatilia mambo ya Tz na Drc na hasa ya Tz kwakua anafahamu vingi na anafahamiana na wengi.
Muda mwingi akiwa amepumzika anafuatilia au kuwasiliana na watu wa Tz kwasababu ya upweke, mazingira, tamaduni n.k
Mpaka atakapo weza kuwa na washikaji wapya na kuzoea mazingira mapya ya ugeni ndipo atapunguza kufuatilia ya Tz.
Kwaiyo kama mshikajiwake ni Feisal na inasemekana Kuna Kiongozi wa Azam aliongea na Kiongozi wa Yanga siku Azam inacheza na Dodoma jiji na inasemekana uyo Kiongozi wa Yanga Ali mpiga majungu Mayele wakati akiongea na uyo Kiongozi wa Azam.
Kwakua uyo Kiongozi wa Azam friji haligandishi akampa maneno labda Bangala au Feisal ambao Wana ukaribu na Mayele, Mayele bila kufikiri position yake aliyo iacha Yanga na mashabiki wake aka kurupuka kuongea alicho ongea uku akitambua au kutotambua Yanga inahusisha nchi Nzima isipokua kikundi kidogo Cha uhasi kinacho itwa Simba.
Mayele ame (provoc) nchi ya Wananchi
Ame unyea mkono ulio mlea, Kama Wazazi Yanga naomba wamsamehe.
Kwasasa Mayele yupo Sana mitandaoni kwakua Bado hajapata kampani na kuzoea mazingira mapya.
Kwasasa Mayele anachezea timu ambayo ni kama Azam Haina wafuasi wengi ila ni timu Tajiri pale Egypt ukiondoa Ahly, Zamaleki na Future.
Mayele anatakiwa aongeze juhudi na kuwafunga Ahly, Zamaleki na Future timu vigogo ili aweze kupenya ki umaarufu na kujenga ufalme mpya kule Egypt.
Amtafute nahoza wa zamani wa Azam Himid Mao amwelekeze namna ya kuishi Egypt kwakua tayari ana ukaribu na Sure boy ambaye ata muunganisha na Himid.
Pole Mayele pole Yanga, ivyo ni vitu vidogo tu focus kwenye mechi zijazo tu twae ubingwa aya mengine yanapita.