Edo Kumwembe umechemka.

Nimefuatilia uzi mzima lakini simjui nani uliyemzungumzia huyo Edo Kumwembe wa wapi?


Hicho anachokifanya kipo moyoni au njaa imemsukuma kukifanya?

Kitu kingine katika kuchagiza umri wanaotaka huko Europe ye kapeleka wangapi wa chini ya 20?

Mwisho nijisemee tu akili mara nyingi sio maarifa.
 
hayo ndio mambo ya simba na yanga kuwalipa wachezaji ambao umri umeenda kama kina blanon pesa nyingi wakati umri umeenda
 
Edo na Shafii Dauda ni wababaishaji kwny Michezo wanaojifanya wanajua kila kitu na kuponda kila kitu cha Bongo
 
Watz wanapenda sifa za kijinga. Ukweli mchungu hawataki kuusikia. Hapo bado carbon 14 haijapita
 
Umeeleza vizuri sana mkuu.
 
Sasa tatizo liko wapi, umesema wengi wamempa moyo ila 1 tu ndo amemvunja moyo. Uhuru wa kutofautiana mawazo lazim uheshimiwe.
Uhuru wa kutofautiana una mipaka yake huyo mtu aliyekosoa ni prominent figure. Hivyo comment yake italeta shida fulani.
 
Himid sio Mzanzibar usiropoke vitu usivyojua
 
Tatizo la wabongo akikuambia ana miaka 24 ujue huyo ni 29
hii imejitokeza sasa ivi,napata notification fb kumtakia jamaa yangu kheri ya kuzaliwa kuangalia eti kafikisha miaka 25 wakati najua ana chezea 30+
 
Edo ni mzee wa historia yuko poor sana katika analysis.
Nauliza hivi Radhi Jaid yule Mtunisia alienda kucheza premier league akiwa na umri gani?!
 
Hapo uliposema hawawezi kuchambua soka mubashara (live) sina uhakika kwan Eddo kila weekend anakwea pipa kwenda south kutangaza/kuchambua ligi kuu ya uingereza kwenye supersport chanel ya kiswahili.
 
Tatizo letu wa tanzania huwa hatuupendi ukweli hata kidogo, mtu kakuambia ukweli halafu wewe unadai unakatishwa tamaa, hebu wacheni ujinga basi huyo himid ana miaka mingapi anacheza bongo??? Kwanini asiende wakati ule, aje aende leo baada ya kuchokwa huko aliko????
 
Buffon ni zaid ya 39
 
Mleta mada na wachangiaji wengi humu mmeshindwa kuelewa mantiki ya Eddo Kumwembe ambaye kwa mtazamo wangu yuko sahihi kabisa.

Eddo ni kati ya wachambuzi wanaohimiza sana wachezaji wetu wenye vipaji waende Ulaya mapema ktk umri mdogo ili kuwe na uwezekano wa kujifunza kwa angalau miaka 2- 4 na kuwa na uwezo wa kuuzika. Mtu kama Simon Msuva, Mkude n.k wanakaribia kutoka kwenye age nzuti ua kukulika Ulaya. Aishi Manula anapaswa kwenda nje now.

Kwa kiwango cha Himid Mao yuko vizuri lkn Ulaya ni kama ataanza upya ambapo inaweza kuchukua 3 years kabla ya kuuzwa kwenda Ligi bora zaidi. Ndicho anachojutia Eddo, na ni ukweli kwa sababu Eddo anajua Himid kwa uwezo wake ulikuwa ni wa kufika mbali.
 
Nadhani, Eddo katoa mawazo yake....kama we unavyotoa yako hapa na huku wengine tukitoa mawazo yetu kwenye mawazo yako...kama we ulivyotoa mawazo yako kutoka kwenye mawazo ya Edo. Nadhani Watz inabidi tujifunze kuheshimu mawazo ya mtu...hata kama ni kinyume cha mawazo yako
 
Sikumbuki Himid Mao kuishi miaka 12 mfululizo Zanzibar. Maana hicho ndio kigezo cha Mtanzania kutoka Tanzania Bara kuwa Mzanzibari. Kwa kuzaliwa yeye ni motto wa Mao Mkami, mchezaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza. Yaliyosalia yanajieleza yenyewe kuwa yeye si Mzanzibari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…