Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
EDWARD LEKAITA: TUMEENDA ZAIDI YA TULICHOAHIDI KWENYE ILANI YA CCM 2020 - 2025
Mbunge wa Jimbo la Kiteto mkoani Manyara, Edward Ole Lekaita amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kishindo, ambapo utekelezaji huo umetikisa katika majimbo yote nchini.
Ole Lekaita amesema hayo bungeni Jijini Dodoma leo Juni 19, 2025 wakati akichangia mjadala kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2024, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2025/2026.
“Miradi hii ya maendeleo (iliyotekelezwa) imetujengea heshima kubwa sana Wabunge kwenye Majimbo yetu, imeleta kigugumizi kikubwa kwa watu wanaotamani majimbo hayo...,” amesema Ole Lekaita