Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu naona unazidi kuwachokonoa chokonoa wahurumie watakata pumzi.Hii ngonjera ulivyoitunga ungemuimbia uchwara angekupa hela ya chai
ZiwatafuneWadau, amani iwe kwenu.
Hii sasa inaitwa kama mbwai na iwe mbwai. Taarifa rasmi nilizopata ni kwamba Rostam Aziz yupo nchini Afrika ya Kusini ambako ameamua kuweka maskani yake. Taarifa zinasema kuwa kwa sasa biashara zake hapa nchini zinasimamiwa na mdogo wake ambaye pia amepewa jukumu la kusimamia mradi wa kitega uchumi pale Oysterbay Police. Rostam ameamua kuondoka nchini kutokana na biashara zake kutoenda vizuri hasa kutokana na ukweli kwamba zilijengwa kwa misingi ya kubebwa na sasa fursa hiyo haipo tena baada ya Rais Magufuli kuweka misingi ya biashara halali.
Hadi anaondoka nchini, Rostam Aziz alikuwa amemkopesha swahiba wake, Edward Lowasa shilingi bilioni 10 kwa awamu mbili tofauti. Awamu ya kwanza alimpa shilingi bilioni 5 Mwezi Julai 2015 wakati ambapo Lowasa alikuwa na mazungumzo na Mwenyekiti wa CHADEMA FREEMAN MBOWE ya kuhamia UKAWA. Fedha hizo ni miongoni mwa zile Bilioni 10 ambazo Lowasa alimpa Mbowe ili kurahisisha safari yake ya kugombea Urais kupitia UKAWA.
Awamu ya pili Lowasa alipokea shilingi bilioni 5 Mwezi Agosti 2015 ambazo zilienda kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, MBOWE kwa lengo kugawa kwenye majinbo yote ambayo CHADEMA walisimamisha wagombea Ubunge. Hata hivyo, inadaiwa kuwa fedha hizo hazikwenda kama ilivyotarajiwa ambapo Mbowe aliamua kugawa shilingi milioni 50 tu kwa kila jimbo kwa majimbo 30 tu.
Makubaliano ya Rostam na Lowasa ni kwamba, ikiwa Lowasa angeshinda Uchaguzi huo, angempa swahiba wake zabuni ya kuendesha mitambo ya kufua umeme pale Kinyerezi. Aidha, katika makubaliano hayo, waliafikiana pia kuwa ikiwa Lowasa hatafanikiwa kushinda Urais, fedha hizo zirejeshwe kwa njia ya kampuni za Rostam kupewa Zabuni kwenye Halmashauri zitakazoongozwa na CHADEMA. Lowasa alimhakikishia Rostam kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa kama walivyokubaliana. Hii ni kwa sababu, Lowasa alikuwa na mtandao mpana wa ma DED ambao walipata dhamana hiyo kwa ushawishi wake ambao alikuwa na uhakika kuwa hawatamwangusha kwenye Uchaguzi huo.
Hata hivyo, baada ya Lowasa kuangushwa kwenye Uchaguzi na mtandao wake wa Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ndio uliofanikisha CHADEMA kushinda kwa baadhi ya majimbo kuvunjwa, Lowasa anahema na kutweta. Bilioni 10 alizokopa kwa Rostam zinamtesa. Hajui wapi pa kuzitoa na Rostam anasisitiza kuwa lazima Lowasa atekeleze vipengele vya makubaliano yao. Kazi ipo
Unapata wapi muda wa kumfuatilia mtu ambaye mnajiaminisha kisiasa amekwisha??Lowasa dawa ya deni ni kulipa bhana...
Mkuu, hakika Lowasa kaingia choo cha kike. Hapa kavurugwa ile mbaya na ile michongo waliyoiweka Halmashauri imebuma baada ya vyanzo vingi kudhibitiwa na TRALowasa dawa ya deni ni kulipa bhana... Hahahaha mtoto wa mjini Mbowe kamuingiza mjini....
Ndiyo Raha ya kushika Dola.Mkuu, pole sana. Endelea kusubiri hiyo hati
Ukianza kuagiza ndimu na udongo ndo utajua kufilisika kimawazo kukojeHizi ni dalili za kushindwa na kufilisika kimawazo
Kwani zile mlizokuwa mnatafuna vijana wa 4U MOVEMENT na sasa ULIPO TUPO zilikuwa zinatoka wapi? Zile alizokuwa anagawa makanisani na misikitini zilikuwa zinatoka wapi?Zile fedha za "ufisadi wa RICHMOND" ziko wapi? Si azitumie hizo kumlipa Rostam?
Unakumbuka Richmond jamaa "alipiga" Bilioni 450? Hata kama tungekuwa mchwa tusingeweza kuzila hata theluthi!Kwani zile mlizokuwa mnatafuna vijana wa 4U MOVEMENT na sasa ULIPO TUPO zilikuwa zinatoka wapi? Zile alizokuwa anagawa makanisani na misikitini zilikuwa zinatoka wapi?