rajabu seleman
Member
- Feb 15, 2018
- 15
- 2
Mgonjwa amepona ama amevishwa ponpon?Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Magufuli na Polepole.
Hawa watu wawili walitushambulia sana eti mafisadi yamewakimbia na yamehamia Chadema. Sisi kweli kama Chadema tulibanwa sana kuhusu Lowassa ila tulijikongoja tuu. Kiuhalisia mwaka 2015 tulipoteza uhalisia wetu kichama ingawa Lowassa kweli alikuwa mtu wa watu. Tulilazimika kuwafanya wengine kukaa kimya maana kama chama tuliua agenda zetu kuu. Hatimaye sasa tutapumua.
Nimeshangazwa sana na mapokezi ya kifalme aliyopewa Lowassa huku serikali kuu zaidi ya nusu wakihamia Lumumba kwenda kumpokea mkubwa yule. Ni kwa mara ya kwanza kuona mtu akipokewa na viongozi wote wakuu wa chama na serikali. Mtu ambaye watu hao hao walidai kawakimbia! Leo wao ndiyo waliomkimbilia! Mbaya zaidi Magufuli anampokea Lowassa huku akiwa kasimamiwa na zee la mipango aka Rostam Aziz. Dah kweli dunia ina mambo.
Lowassa najua amerudi CCM ili kulinda fursa zake kibiashara pamoja na hatima yake ya uzeeni. Ni hayo tu.
Nasubiri kuona sasa mapovu ya kina Polepole na Bashiru baada ya madon kujihakikishia kuwa sasa wamemzunguka mkubwa wao. Acha kabisa siasa hizi za kibongo. Pia nasubiri neno la Slaa (Najua hatosema chochote maana anatumikia)
Wanataka kutuondolea concentration ya msiba wa kitaifa
Nimeandika kuwa Lowasa kuja CDM huwezi kusema ni hasara. CDM ilinufaika sana na ujio wake.. wabunge, madiwani, wenyeviti/mitaa/vitongoji, Chama kikuu cha upinzania. ruzuku, to mention but a few.Hapana Retired; usimuone hivi Lowassa na nadhani si haki kumuona hivyo. Wale wote waliomuunga mkono na kumtumia alipokuja inapaswa kumshukuru tu na kumtakia kila la kheri. Haya mengine si ya lazima. Sidhani kama kurudi kwake ni jambo la kushangaza au kushtua vile. Kwamba alibakia kwa miaka mitatu lazima mumpe hongera na shukrani zake.
Unadhani ana njaa ya pesa kama we!!kura za uraisi nipatie mimi na wabunge wengi wa ccm..huyu mamvi huwa simwelewi kabisa.
alimzuia mke wake asiteuliwe viti maalum,akamzuia mtoto wake asigombee kwenye marudio ya uchaguzi kumbe alikuwa na la kwake jambo.
Si useme wewe sasa !.Mbona kila anayeandika humu anaona negative impact kwa ccm tu,vipi negative impact kwa CDM mbona haziandikwi au kusemwaswmwa sana
Kwani ana Uwezo wa kuongea ,hujaona jana kaongea Sentensi moja tuKama hilo uliliona mkuu nakupa big up. Lakini bado hatuko salama tumeonesha Chadema tunakumbatia ufisadi ukiwa tu na maslahi.
Damage 2020 huyu jamaa ataongea sana atataja hata kwa exagration kuwa ndani ya CDM kuna uozo ikiwemo hati miliki ya vyeo kama mwenyekiti, Ukanda , Ruzuku nk
Kwa ma Ccm mapokezi yao ni yale ya "The spy is Back" atakaa tu akila popcorn movie ikiendelea
Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa,uko sahihi lakini inammana kweli hakuna impact ambayo ni negative kwa CDM??Si useme wewe sasa !.
Tawala za ki Africa zinatumia mbinu chafu kwa wapinzani wao. Badala ya kubadilisha sera na uongozi kuvutia wapiga kura, zenyewe hutumia vyombo vya Dola kudhibiti wapinzani wao.
Sent using Jamii Forums mobile app