Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Tusiufiche ukweli

hatujaimarika bali tumesambaana,
mwenyekiti yupo ndani,
katibu ndo hata hasikiki

waliobaki niambieni wapo wapi?
Lema?
sugu?
Mnyika?
N.K,wote wameingiwa ubaridi,afadhali kidogo bulaya na mdee.

Hatuna muunganiko kama chama,sasa kila mtu anatoka kwa staili yake.
Mwenyekiti ashatoka
 
msindai.jpg

Dogo polepole!
 
Mkuu na Chadema wana mshipa wa aibu? Wao si ndiyo waasisi? Sidhani kama kuna wa kumcheka mwenzake. Tena bora CCM walimnyima tiketi ya urais. Chadema walimteua!
CDM had a purpose and the mission was accomplished with many legislators, diwanis, village chairs,and the like.......
Mnamrudisha ili afanye nini? hana mvuto tena kama 2015! Bila mizengwe, bila kumnyima ushindi wake, angelikuwa rais. Lowasa alikuwa anakubalika sana. Haikuwa hasara kumpokea!
 
Mh. rais wetu kipenzi alichanga sh. mil 50 za matibabu ya ruge wakati akiwa mgonjwa, we unaehuzunika sahz ulichanga sh ngapi?
 
Lowassa alipojiunga Chadema tuliona mbwembwe za Mwenyekiti chadema Freeman Mbowe akiitisha press conference akiongea kwa complex superiority na mbwembwe nyingi kutamgaza ujio wa Lowassa Chadema.Mbona Mbowe hutoi tamko kulikoni? Unaumwa au?
 
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rais Magufuli, Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Humphrey Polepole n.k

Habari zaidi...

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, nchini Tanzania. Lowassa alikuwa mgombea wa kinyang’anyiro cha urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na vyama vinavyounda umoja wa UKAWA katika Uchaguzi mkuu 2015.

Kurejea kwa Lowassa kulikuwa kukitabiriwa na baadhi ya watu, lakini mara kadhaa Lowassa alikanusha kuwa anampango wa kurudi katika chama hicho.

Vyanzo vya habari vinasema hatua hiyo imewashitua watu wengi, kwa sababu ya kile ambacho kilisababisha yeye kuhama chama hicho.

Lowassa baada ya kuitumikia CCM kwa kipindi kirefu alikihama chama cha hicho kufuatia mvutano uliotokea baada ya kutoidhinishwa na chama hicho kuwa mgombea wa urais.

Sherehe za mapokezi yake wakati akirejea rasmi Ijumaa zilifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyoko Lumumba Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho John Magufuli.

Lowassa mara kadhaa amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli, Ikulu ya Tanzania.

Kumekuwa na wimbi la wanachama wa upinzani kuingia CCM tangu Magufuli achaguliwe 2015, kitu ambacho kimekuwa kikizungumziwa katika duru za siasa kwamba kinadhoofisha upinzani.



View attachment 1035375
View attachment 1035459
View attachment 1035448

Unaweza soma pia:

Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums

Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums

Nae kanunuliwa, kweli CCM kwa usajili ni hatarii!
 
Si useme wewe sasa !.

Tawala za ki Africa zinatumia mbinu chafu kwa wapinzani wao. Badala ya kubadilisha sera na uongozi kuvutia wapiga kura, zenyewe hutumia vyombo vya Dola kudhibiti wapinzani wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Chama cha Upinzani chenye zaidi ya miaka 26 kwenye siasa lakini bado wanategemea ruzuku ya Serikali ambayo haijulikani inaendaga wapi, bado wanalia kuibiwa kura. Media kwa ajili ya kukitangaza chama hakuna wanalia na TBC, gazeti limebinafsishwa na mwenyekiti, Makao Makuu ya Chama yapo uchochoroni. Yaani hakuna mbinu zozote za kupambana na watawala ni Bussiness as Usual na ulaghai. Halafu mnalalamikia eti mbinu chafu. Nyinyi mbinu zenu safi ziko wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CDM had a purpose and the mission was accomplished with many legislators, diwanis, village chairs,and the like.......
Mnamrudisha ili afanye nini? hana mvuto tena kama 2015! Bila mizengwe, bila kumnyima ushindi wake, angelikuwa rais. Lowasa alikuwa anakubalika sana. Haikuwa hasara kumpokea!
Kwenye vijiji Lowasa alikuwa hajajiunga na CDM. Unapingana na wanaosema pengine bila Lowasa CDM ingepata wabunge na madiwani wengi kuliko iliopata 2015?
 
Lowassa alipojiunga Chadema tuliona mbwembwe za Mwenyekiti chadema Freeman Mbowe akiitisha press conference akiongea kwa complex superiority na mbwembwe.nyingi kumtamgaza ujio wa Lowassa Chadema.Mbona Mbowe hutoi tamko kulikoni? Unaumwa au?

Atoe tamko gani wakati mkeka wake umechanika?
 
Wewe bimkubwa una mtindio wa ubongo
Lowassa alipojiunga Chadema tuliona mbwembwe za Mwenyekiti chadema Freeman Mbowe akiitisha press conference akiongea kwa complex superiority na mbwembwe.nyingi kumtamgaza ujio wa Lowassa Chadema.Mbona Mbowe hutoi tamko kulikoni? Unaumwa au?

In God we Trust
 
Back
Top Bottom