Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

... Kuteuliwa kwa Kitila na kwa Anna Mgwira ni mifano tu
Mfano huu umenifikirisha sana. Kwa siasa za Kiafrika ni nadra sana uteuzi usifuate manufaa ya mteuaji ama chama chake.

Kama unaamini kwamba Kitila Mkumbo na Anna Mghwira kama walichaguliwa na Magufuli nje ya mikakati ya kisiasa utakuwa hujitendei haki wewe mwenyewe na heshima yako kwenye fani ya uandishi fikirishi.

Hivi leo hii hao kina Kitila Mkumbo na Anna Mghwira bado ni wanachama wa ACT chama walichokuwamo kabla ya kuteuliwa kwenye nafasi walizo nazo sasa? Uliyasikia maneno waliyoyasema walipoteuliwa?

Inawezekana una hoja lakini unavyoiwasilisha inaleta ukakasi fulani kwenye akili za watu!!
 
Mkuu it's about time...imekuwaje rahisi zaid kusema baada ya kutokea. ... naona umeamua kuwasifu Slaa na Lowassa kwa wakati mmoja....hakuna mashaka wala tatizo kwenye maoni yako....issue hapa lazima uwe mkweli....
Kama unajua utaiunga CCM mkono 2020 kupitia rais Magufuli. ..huoni kama ushauri wako wote kwa upinzani unakuwa irrelevant na wa kinafiki?....
Why bother much wakati unajua you have your guys to support at the ruling system?
Hoja ya kulaumu mfumo ni dhaifu mno....if you don't know katiba yetu inampa mamlaka rais kubadili chochote ndani ya JMT in seconds....

Kuchagua wapinzani. .hapo umehoroja na uongo wa kwango cha PhD. ..are you aware kuwa ili mpinzani apewe cheo lazima arudi ccm na aiponde upinzani?.....Hoja mufilisi kabisa hiyo. ..
Issue za Magu kuwachagua wanao weza ku deliver nayo ni hovyo sana.....umeangalia namna rcs dcs na wakurugenzi wanavofanya kazi? Kwa hisia tu na pupa.....angalao kidogo sikuiz wamepoteana....but its worst down here....

Anyways your opinion, your choice. .....it's up to us to continue with the fight come what may.....
 
Umeandika mengi mazuri lakini yapo machache umejichanganya kiasi kwamba yanakutambulisha wewe ni nani na hayo
machache yanashindwa kukutofautisha na wale unaowaita ulipo tupo au wazungurusha mikono wa mabadiriko..
 
Nilichonote hapa

1. Bado mwanakijiji haoni sababu ya kutomuunga mkono Magufuli.

2. Anaona CHADEMA walikosea kumpokea lowassa hivyo wawaombe radhi watz

3. Mbowe awajibike kwa kumpokea Lowassa.

4. Kuondoka kwa Lowassa upinzani ni uthibitisho kuwa CHADEMA walikosea kumpokea.

4. Anaamini ELna RA ni wachafu na mafisadi.

5. Haoni kama ukaribu wa RA na EL kama utamcorrupt Magufuli maana anaamini Magufuli ni strong enough kuwa collapsed.

6.Anaamimi JPM amefanya mabadiliko makubwa, amebaki njia panda kwenye iwapo JPM atafanikiwa kuibadilisha CCM.

7. Anaamini kuna majeraha Lowassa ameyaacha upinzani, wakati huohuo anakiri kuwa Lowassa hajawahi kuwatetea upinzani.

At this juncture ninakubaliana na Mzee Mwanakijiji kwenye hoja moja tu nayo ni kuhusu kujiuzuru kwa Mbowe au kutogombea maana mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi chamani na kama sikosei wapo ngazi ya mkoa. Mbowe asigombee siyo kama ishara ya kuwajibika bali kama ishara ya kusadifu ile demokrasia inayoimbwa CHADEMA hivyo tu basi.

Pia nimpongeze Mwanakijiji kwa kuendelea kumuunga mkono JPM na kukiri hilo waziwazi. Tofauti na watu kama chahali and the like ambao mwaka 2015 walikuwa kwa JPM sahizi wanajifanya wanatunafkia eti wapo upinzani. Kisingizio eti walimsapoti JPM sababu ya Lowassa. This is absurd, Lowassa anaweza kuwa sababu ya wao kutosapoti upinzani lakini hawezi kuwa sababu ya wao kumsapoti JPM waache kujificha kwenye visingizio wabaki huko na JPM wao.

Mawazo mengine ya Mzee Mwanakijiji siyapingi moja kwa moja lakini yanahitaji kuwa substantiated enough to convince any reasonable person. Nitapoint out mkanganyiko wa mawazo yake hapa chin.

i. Mzee Mwanakijiji hajaeleza kuondoka kwa Lowassa kunakuwaje uthibitisho wa kuwa CHADEMA (au mbowe kama anavyodai) alikosea kumpokea Lowassa? Hivi kuna uhusiano wa "Kupokelewa" na "kuondoka". Kama kuondoka ni uthibitisho wa kuwa walikosea kumpokea je inamaana CHADEMA walikosea kumpokea Kafulila kutoka nccr maana naye ameondoka? Je wasira alipokelewa upinzani kimakosa ndiyo maana akaondoka? Similar facts are to be treated equally. Mwanakijiji ameshindwa kueleza uhusiano uliopo hapa na kwamba je ili umpokee mtu unatakiwa ujiulize atadumu muda gani? Na je chama kina option ya kumnyima kadi mtu kwa sababu yoyote ile?

Na kama ni kumpa mtu ugombea je ukipewa kugombea Urais unatakiwa usiondoke? Vipi tuna guarantee gani kuwa akigombea Lissu au mbowe hataondoka baada ya uchaguzi? Na akiondoka ni uthibitisho kuwa tulikosea kumpa kugombea?

2. Hoja kwamba Lowassa ameacha majeraha CHADEMA wanayotakiwa wayatibu imekuwa conflicted na hoja yake Mwanakijiji mwenyewe kuwa Lowassa hakuwahi kuwa mpinzani wa kweli hivyo kwa maoni yake alikuwa mzigo maana hakuwatetea wapinzani. Mwanakijiji anmeshindwa kuondoa mgongano katika hoja hii.

3. Mwanakijiji ameshindwa kueleza ni kwa jinsi gani anatuguarantee kuwa JPM ataweza kudhibiti (mafisadi kwa mujibu wake Mwanakijiji) akina EL na RA wanaomkaribia kwa karibu. Na ameshindwa kueleza je kuna ulazima gani CCM na mtu (credible kwa mujibu wa Mwanakijiji) kama JPM awe karibu na "mafisadi" aache kazi zake ofisini aende Lumumba uongozi mzima wa chama kumpokea "Fisadi". Hii inamaana gani na wana umuhimu gani hawa Mwanakijiji anaowaona siyo "wasafi" kupewa heshima kubwa na "msafi" (asiyedanganyika kwa mujibu wa Mwanakijiji)?

4. Kuhusu mabadiliko na utendaji wa JPM ni very subjective inategemeana unatazama kutokea angle gani. Mwanakijiji ameshindwa kuonesha ni angle gani anayomtazama Magufuli maana wapo wanaomtazama kama Rais wa wizara ya "miundombinu na uchukuzi" pekee.

Nawasilisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majeruhi wa kwanza katika senema hii ni Hamphry Polepole. Nadhani kuanzia sasa atakuwa na akiba ya maneno. We acha tu, Kijana alisema bwana.
 
Kwamba Mbowe kumpokea lowassa na lowassa kuondoka ndio ajiuzulu uenyekiti ? Kisa wewe hukupenda basi ndio unataka awajibishwe,ebu niambie unatumia kigezo ghani kujua kwamba jiwe sio fisadi ?
Katika hili Mzee Mwanakijiji ana hoja.

Siyo Mbowe anatakiwa asigombee kwa kuwa ni kiongozi asiyefaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA bali ni yeye aliyeongoza makosa yaliyotufikisha hapa kwenye huu mkanganyiko uliopo hivi sasa.

Hata asipokuwa Mwenyekiti Mbowe bado ni mmojawapo wa ALAMA ya upinzani hapa Tanzania.
 
23. Swali: Una maana gani?
Jibu: Nilisema mwanzoni kuwa ndogo za Lowassa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimekufa. Nimesema hapo juu kuwa ujio wa Rostam Aziz sasa hivi na kumrudisha rafiki yake CCM una maana yake. Kumbuka mwanzoni mwa miaka ya 2000 RA alijulikana sana kama “the King Maker” yaani mtu anayewapatia watu “mfalme”. Vipi kama ndogo ya Lowassa kugombea Urais itakuwa ni kama ya viongozi wale waliokuwa tayari kutawala kwa mhula mmoja tu; vipi kama wanaweza kufanya kama kilichofanywa Urusi? Na yakatokea mabadiliko ambayo ndio wameyapigia mahesabu; vipi kama ndogo ya Lowassa kuwa mgombea wa Urais ni ya 2020? Magufuli amekuwa akilalamikia sana ugumu wa kazi ya Urais na ni jinsi gani umekuwa mzigo mkubwa sana kwake kiasi kwamba niliwahi kuandika Makala kuwa kama kweli anaona ni mgumu hivyo Katiba imeweka njia za yeye kuutua; vipi kama tayari ameanza kufikiria kuutua mzigo huo mara moja kwa sababu unakuja na lawama nyingi sana? Hili wazo ukiliendeleza kwa mbali zaidi unaweza kushtuka sana. Labda ndoto ya Lowassa haijazimika kabisa.


Hayo mambo uliyoyaandika ni mazito sana, sidhani kama umewahi kufikiri hivyo.
 
Brother why kuondoka kwa lowassa iwe ni mkanganyiko ? umesahau slaa alishiriki katika kumleta lowassa ? kipi kigumu kuondoka kwa mbunge kama waitara aliyechaghuliwa na wananchi au mgombea uraisi ? je kuondoka kwa wabunge kama waitara hilo nalo nikosa la mbowe ?
 
Hoja hapa si kuondoka kwa Lowassa ama wabunge kama Waitara au Gekul, hoja ni kwamba ujio wa Lowassa uliifanya CHADEMA kusalimu amri kwenye ajenda yake ya msingi ambayo ni "vita dhidi ya ufisadi".
 
Msamehe bure mwanakijiji
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja hapa si kuondoka kwa Lowassa ama wabunge kama Waitara au Gekul, hoja ni kwamba ujio wa Lowassa uliifanya CHADEMA kusalimu amri kwenye ajenda yake ya msingi ambayo ni "vita dhidi ya ufisadi".
Namna ghani walisalimu hamli ? chama cha siasa akiwezi kuwa na agenda moja tu
 
Nimejifunza kuwa humu ndani ni vigumu kwa mtu kuandika pasipo kusukumwa na itikadi za kisiasa.
My brother Mwanakijiji ana hoja na nimwandishi bora, ila kinacho mponza ni itikadi na chuki alizonazo zidi ya mtu/watu au chama asichokipenda na ndio maana kila akiandika huacha mkanganyiko.
 
Hoja hapa si kuondoka kwa Lowassa ama wabunge kama Waitara au Gekul, hoja ni kwamba ujio wa Lowassa uliifanya CHADEMA kusalimu amri kwenye ajenda yake ya msingi ambayo ni "vita dhidi ya ufisadi".
Mkuu hebu kuwa realistic hivi huwa mnamaanishaga nini mnaposema CHADEMA imesalimu amri kwenye hoja ya ufisadi?

Mnaweza mkathibitisha kuwa kuna ufisadi umefanyika halafu CHADEMA wakashindwa kuusemea? Huwa wenzetu mnatumia kipimo gani?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe kupisha wengine ni wao zuri. Ila wazo hilo linatiwa doa na kutia mashaka nia yake pale linapotolewa zaidi na "wapinzani" wa CDM kuliko wanahadema wenyewe.

Mtu unajiuliza, wanataka Mbowe atoke halafu wamuweke nani? Mtu wao? Ni lini CCM ikaitakia CDM mazuri? Na vice versa? Maana wengine tumeona wengi ni wanafiki tu na wasaliti tu. Kwa hivyo naweza kuwaelewa CDM risk wanayoiona ya kumtoa Mbowe. Maana mpaka serikali ya CCM imeunda sheria kabisa ili kuhakikisha Mbowe anang'oka! Kuna nini nyuma ya pazia? Ni mambo gani CCM wanashindwa kutekeleza Mbowe akiwa mwenyekiti wa CDM? Maana kama CDM ina kiongozi dhaifu, kimantiki ni jambo jema kwa CCM na tusingepaswa kusikia kelele zote hizi kutoka upande huo.....wangekaa kimya tu.

Kuna kitu, sio bure.

NB: Napenda vyama vya siasa viwe na demokrasia ya kweli. Kwa sasa, sio CCM wala CDM tunaweza kwa dhati kabisa kusema wana demokrasia ya kweli. Well, pengine hiyo ndio siasa!
 
Hajarudi burebure! Utashituka mwenyewe siku ukisikia.
 
Swali langu kwa mwanakijiji ni hili, kama ndoto ya Lowassa kugombea urais 2020 itahuishwa na RA, wewe utasimama upande gani? Unaweza vilevile kumjibia Dr. Slaa kama ukipenda.
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…