Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Nadhani Mh. JPM ameshtukia kuhusu possibility ya Lowassa kuungana na Membe upinzani ingekuwa hatariiiiiiii sana kwa CCM, hivyo akamuwahi kumrudisha home kw gharama yoyote ile..!!
Nyamaza hulijui dude linaloitwa ccm. Hili dude limeleta ukombozi kusini mwa afrika halina mfano. Likiamua hakishindikani kitu. Subiri 2020 utabaini njomba
 
JPM nampongeza na kumuombea kwa Mungu kwa kuivua gamba siasa ya TZ na kuleta kutapatapa kukubwa kwa wanasiasa fuata mkumbo.

Sasa kilichobaki, baada ya mtanziko mkubwa kisiasa, ajitoe CCM agombee UKAWA na Lowassa Agombee CCM 2020.

Labda kama hawa wababe wanaorudi CCM wamepitia ubatizo wa moto, ila kama ni yale maji kama ya mto yorodani ya kutaka vyeo na madaraka wakipata nafasi wanaweza kutoboa meli.
 
" Kutokana na umri mkubwa wa chama chetu cha CCM, watu wengi wenye kasoro wamejiingiza kwenye chama hiki. Sasa kimekuwa kama dodoki ambalo linabeba vitu visafi na vichafu. Sasa tumekuwa na watu wa ajabu sana ndani ya chama chetu".Nyerere

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini ahangaike mzee wa watu wakati ninyi ndio mliomsaliti! mlimtupa pembeni yeye pamoja na misingi ya chama ili kupata 'boost' ya muda mfupi, sasa Lowasa amerudi CCM bila shaka yeye na wafuasi wake. CDM inapaswa kujifunza na kutorudia kosa
 
Na amefanya vizuri kuhama mapema ili chama kijipange na kuweka mikakati kuelekea 2020.Kuja kwa lowasa ni faida kwa chadema kwa kuwa kasaidia kuongeza wabunge na madiwani .Lakini kuondoka kwa lowasa ni faida vilevile kwa sababu hakutakuwa na msuguano mkubwa na nani agombee kati ya lissu na lowasa .Maana lowasa ana pesa hivyo angekuwa na ushawishi mkubwa hivyo kuleta taharuki .Kwa kuwa kaondoka mapema hili ni jambo jema sana Kwa lissu na chadema cha ujumla .Twende na Lissu 2020.
 
Mgombea Urais wa Chadema Huenda akawa anatokea Mikoa ya kusini kwa Mara ya kwanza 2020 Baada ya Mlima kuhama Leo
 
Mimi pia kama chadema nimefikiria pia ulichoongea na kimenitisha kama angesepa ule muda wa kukaribia mchakato wa kutafuta wagombea ila kwa muda huu amewahi sana na hana impact maana Lissu is back.
Amekosea sana,angesubiri mpaka 2020 kuelekea uchaguzi awavuruge kwanza ndo asepe.Chickens coming home to roost never did make me sad,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuwa lowasa karudi ccm na ilitegewa kwa vyovyote vile agombee urais kupitia chadema na asingekubali kumuachia Lissu agombee ,sasa njia nyeupe kwa Lissu ,Mungu ni mwema .

Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia
Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mk-Ia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Subgura nakuambia.
“Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.


Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mk-Ia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Subgura nakuambia.
“Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.
 
Back
Top Bottom