Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe nyau hebu kwenda zako wewe hujui chochote unatoa povu tu. Kazungushe mikono huko. Kama una hoja lete, sio viroja.
Link Godbless Lema: Kuna siku mtavililia vyama vya Upinzani viwasemee hamtavipata. - JamiiForumsWaziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.
Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.
Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rais Magufuli, Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Humphrey Polepole n.k
Habari zaidi...
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, nchini Tanzania. Lowassa alikuwa mgombea wa kinyang’anyiro cha urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na vyama vinavyounda umoja wa UKAWA katika Uchaguzi mkuu 2015.
Kurejea kwa Lowassa kulikuwa kukitabiriwa na baadhi ya watu, lakini mara kadhaa Lowassa alikanusha kuwa anampango wa kurudi katika chama hicho.
Vyanzo vya habari vinasema hatua hiyo imewashitua watu wengi, kwa sababu ya kile ambacho kilisababisha yeye kuhama chama hicho.
Lowassa baada ya kuitumikia CCM kwa kipindi kirefu alikihama chama cha hicho kufuatia mvutano uliotokea baada ya kutoidhinishwa na chama hicho kuwa mgombea wa urais.
Sherehe za mapokezi yake wakati akirejea rasmi Ijumaa zilifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyoko Lumumba Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho John Magufuli.
Lowassa mara kadhaa amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli, Ikulu ya Tanzania.
Kumekuwa na wimbi la wanachama wa upinzani kuingia CCM tangu Magufuli achaguliwe 2015, kitu ambacho kimekuwa kikizungumziwa katika duru za siasa kwamba kinadhoofisha upinzani.
View attachment 1035375
View attachment 1035459
View attachment 1035448
Unaweza soma pia:
Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums
Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums
Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums
Unaijua CDM 2010? Halafu Useme CDM haikuwa na mvuto?Never, CDM haikuwa na mvuto kama alipoingia Lowasa, mvuto ulikuwa mkubwa!
Lao mpja mipango tu ile!Mzee Wa Msoga Alishindwa Nini Kumpa Jamaa Wa Enzi Za Boys To Men Mpaka Akachafuliwa Na Yale Matope? Rafiki Yake Angekuwa Magogoni Mzee Wa Msoga Angejilimia Nanasi Zake Fresh Tu Bila Stress Za Kuchafuliwa Legacy Yake.
Katubu bin kaungama karudi nyumbani huku akiangaliwa haswa ni mwana kondoo au igizo.Mwanzoni CDM walikuwa wanasema fisadi papa 2015 wakazunguka nchi nzima kumsafisha. Upande wa pili CCM jangwani pale Kikwete akasema fisadi ameenda upande mwingine leo hii mtu asiye wataka mafisadi kampokea bira shida na kamsafisha.
Ama kweli huyu mzee yuko na akili sana
Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli Lowassa kavuruga watu.
Ha ha ha ha Lowassa kiboko yao na kawaweza.
Chadema walimwita Fisadi weeeee akahamia kwao...wakalamba matapishi na wakanywea balaa.
We fikiria Lissu na mdomo wake ule akanywea.
Lema na mdomo wake ule na viapo vyote kuwa ni haki toka kwa Mungu kumzomea Lowassa akanywea na kunyenyekea.
Alivoenda Chadema , CCM wakamsema weee, kina Polepole wakamwita malaya na fisadi wee..
Sasa karudi. Ccm wote ziii...Polepole kanywea..ccm imenywea.
Hivi sasa ngoma droo. Hakuna ccm wala chadema anayeweza muita Lowassa fisadi. Wamebaki kama BAK na mwenzie wanavyotifuana kwa kitu kile kile...
Lowassa kiboko..jamaa korofi sana ha ha ha
omera wewe
Wanajuana vyema wale wote.kiufupi tz hakuna upinzani...Mkuu mzee slaaa alimfananisha lowasa na Choo cha kiafrika, Sasa alichoo kiita Choo boss wake slaa (jiwe)anakiita lulu.
Swali ni slaaa alikikimbia choooo leo choo kimemfuata mzee slaa.atakikimbia Tena hicho choooo. ?
Sent using Jamii Forums mobile app