Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Chadema inamalizwa na wanachadema wenyewe!!! Angalieni hata comments zao baada ya tukio hili!!! Naomba muweke kumbukumbu hii, bila kutubu makosa ya 2015 na kuwajibika tusitarajie mabadiliko ya kisiasa. Chadema inaenda kuwa NCCR mpya, mark my word!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Chadema inaonekana kutokuwa na strategy ya kujikosoa yenyewe tofauti na CCM walivyo. Japokuwa CCM wanafanya kwa kiwango kidogo, Chadema hawafanyi kabisa. Bila kujitathmini, kujikosoa wenyewe na kujirekebisha, Chadema itakuwa sikio la kufa
 
Kwa siasa za CHADEMA kama ilivyo kwa mchezo wa soka ni wazi uwezo wa Mbowe kuipatia nguvu zaidi umeisha na kitakachofuatia ni kuiporomosha bila shaka na mbaya zaidi itakuwa ni kabla ya 2020.

Huu ni utabiri wa mwana JF mmoja kwa Chadema
 
naona kama vita ya 2015 bado mbichi....mzee kahisi tishio la jasusi kaona na yeye aunde kambi yake yenye nguvu...hiyo ndio siasa...sasa...kumbuka rostam na apson ni team lowassa na wameshafika kwa mzee....nadhani hapa kuna makubaliano...
Duuuh . . . . . such a fantastic opinion. Ila mzee huoni kwamba Apson alikuwa 'kikazi' kwa Lowasa?
 
Kama ilivyo kawaida, endapo atajitokezza kiumbe kumkashfu au KUMSEMA vibaya Lowasa Basi ajiandae kupambana na jeshi la polisi.

Awali maneno yake yalikuwa ya uchochezi ila leo Mhe. Dingilai kasema amefutiwa dhambi zake na amekuwa mpya.

Usimtamkie mabaya mzee wetu, Msukuma yule jamaa yako uliyemtusi amerudi kwao Sasa jiandae kumfanya rafiki ukigoma acha chama.

Nape mzee karudi so jiandae kumsujudia,

Makonda jiandae kumsalimia kwa heshima mzee baba la sivyo utapoteza ukuu wa mkoa.

Ridhiwan baba karudi, ulimkejeli Sasa amerejea jamvini

Sent using Jamii Forums mobile app

Duuh . . . .mliotajwa hapo juu mpo?
 
Kweli, hapa Chdema wamshushe Lissu na Fatma Karume, weka pale Zitto awe waziri wa fedha, waziri mkuu tutampata tu humo humo upinzani
 
Shetani hajawahi kuongoka. Sasa timu ya wenyewe huko ccm imekamilika. 1. EDWARD LOWASA 2.ROSTAM AZIZI na 3 ANDREW CHENGE. ccm mbele kwa mbele wizi ni mila yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ninaamini kabisa kama wahenga walivyosema, hata shetani azeeke namna gani hawezi kuwa malaika

CCM ni ile ile, na mpinzani wa kweli atatoka nje ya CCM

Only time will tell
 
Kama zinavyodumu za Mangi. Akisema hakuna wa kupinga. Hata alipomleta mgeni wenu wote mlishangilia. Kasoro Dr. Naye ili awe salama basi ilimbidi akimbie nchi..
Kwani kama angebaki angedhurika? Na ni nani ambaye angemdhuru kama kweli angedhurika kwa kutoondoka nchini?
 
Lowassa alipojiunga Chadema tuliona mbwembwe za Mwenyekiti chadema Freeman Mbowe akiitisha press conference akiongea kwa complex superiority na mbwembwe nyingi kutamgaza ujio wa Lowassa Chadema.Mbona Mbowe hutoi tamko kulikoni? Unaumwa au?
Labda tusubiri mwenyekiti atakapo toka rumande
 
Shetani hajawahi kuongoka. Sasa timu ya wenyewe huko ccm imekamilika. 1. EDWARD LOWASA 2.ROSTAM AZIZI na 3 ANDREW CHENGE. ccm mbele kwa mbele wizi ni mila yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo no.1 kwenye orodha yako aliondoka CCM miaka kadhaa iliyopita huku akipata support ya kutosha toka kwa uliyemuweka no.2. Swali ni je, walikokuwa kabla ya kurudi CCM walikuwa wanaiba ama kuendeleza wizi unao usema? Na, mwenyekiti si ndiye ambaye alituaminisha sisi wananchi ya kuwa ni msafi baada ya kufanya kampeni kwa miaka 8 dhidi ya orodha ya mafisadi papa naye akiwemo?
 
Nimesoma waraka wa Lissu kuhusu Lowassa na mashinikizo yanayo mkabili hadi kuamua kufunika USO Kwa aibu na kufanya lile lisilo tegemewa na kurudi kule kule waliko mtukana matusi ya nguoni wakati wa kampeni na baada ya kampeni.
Ukiacha mashamba na ranchi zake kutishiwa kunyang'anywa, TRA na mafao yake kubwa zaidi ni kusota jela kwa mume wa binti yake Sioi miaka mitatu sasa na binti sio ajabu anaangua kilio kila siku Nyumbani kuwa kama sio wewe baba kuwa Chadema mume wangu asingesota jela.
Pengine anaulizwa na binti au mama Regina kuwa hivi Sioi angekuwa mkwe wa Warioba, Salimu au Msuya angesota namna hii Kwa kesi isiyo kichwa wala miguu?
Mwanamume yeyote ukipima hali hiyo ya Lowassa unapata jibu kuwa alifikia wakati wa kuchagua kuwa na family na sio hao wapiga kura milioni sita.
Tumwambie Lowassa tumekuelewa, aende na akae kimya asilete matamshi kama Waitara maana atawatibua nyongo watu na makombora ya majibu atakayo pata yanaweza kumuua kabisa.
Kila lakheri Ngolay, ukituheshimu tutakuheshimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaaa amerudi kwao....ila watu wagumu sana Lowassa ni ccm damu, kumbukeni aliwahi kukosea kwenye mkutano wa chadema aliwahi kusema ccm oyeeeeee[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Back
Top Bottom