Tetesi: Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,895
Reaction score
20,392
Wadau, amani iwe kwenu,

Ni dhahiri kwamba Lowassa na Sumaye hawana amani ndani ya CHADEMA. Hawana dira wala mwelekeo. Kila wanalopanga halipangiki na CHADEMA hakionekani kuwa chama chenye mwelekeo wa kushika dola.

Kamera ya Lizaboni imenasa kikao cha mkakati wa Lowassa kutaka kujiengua na CHADEMA na kurejea CCM. Kwa sasa anaendelea na mazungumzo makali na baadhi ya wafuasi wake waliobaki CCM ambao wamemgomea kwenda upinzani. Kilichomshtua zaidi Lowassa ni hili wimbi la sasa lililoshika kasi la viongozi na wafuasi wa chama ambao aliona kuwa ni kimbilio lake wakimkimbia na kujiunga na CCM.

Je, viongozi wangu watampokea Lowassa? Mimi nasema wasiwe wepesi kukubali ujio wa Lowassa. Ni vema tukafunga gate valve ili asiruhusiwe kurejea tena chamani. Ameshaivuruga CHADEMA na sasa anataka kurejea tena CCM na kutuvuruga. Tusiruhusu jinamizi likatukumba tena ndani ya CCM.
 
WEWE NI UCHUMIA TUMBO NDIYO UNAKUSUMBUA NA LAANA YA KUTAFUTIA KUTEGEMEA NA KUCHUMIA TUMBO....NA MZIDI KULAANI KWA KUTEGEMEA VIUNGO VYA MWILI NA WANA WA ADAM ILI MUISHI NA WATU WOTE WASEME AMINA.
 
hivi ni lazima kuanzisha thread kama huna cha maana au jambo linaloakisi ukweli ukashare na wanajamii ? kuna haja ya mods kupima content ya kila kinacholetwa hapa... vinginevyo threads nyingine zinafutwa tu hakuna namna
 
Nipo masomoni Uingereza. Napambana na kitabu. Ndo maana sipo sana humu
pambana mama, pambana, urudi ukiwa dr. Lizaboni, tuone watu watakavyochonga, msalimie malkia pale Birmingham
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…