Omutwale
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,429
- 1,053
Tarehe 27 Novemba 2010 EL alikutana na Waandishi wa Habari. Na tarehe 19th October mwaka huu tena amekutana na Waandishi. Alichokisema mwaka jana na alichosema tena mwaka huu hakina utofauti. Japo ahadi alizotoa mwaka jana, mwaka huu akuzitolea taarifa kueleza amefikia wapi kiutekelezaji.
Kwa ufupi mwaka jana alieleza kusitisha uvumilivu dhidi ya waandishi na akatishia kuanza kuwachukulia hatua za kisheria na kinidhamu kupitia mahakama na MCT. Ni mambo yaleyale kayarudia tena baada ya mwaka mmoja. Hapo chini, nimechukua rejea toka vyombo viwili tofauti ili kukuonyesha mikwara na usahaulifu wa Wanasiasa wetu.
Kwa ufupi mwaka jana alieleza kusitisha uvumilivu dhidi ya waandishi na akatishia kuanza kuwachukulia hatua za kisheria na kinidhamu kupitia mahakama na MCT. Ni mambo yaleyale kayarudia tena baada ya mwaka mmoja. Hapo chini, nimechukua rejea toka vyombo viwili tofauti ili kukuonyesha mikwara na usahaulifu wa Wanasiasa wetu.
By Novatus Makunga said:20th October 2011
Lowassa: Uvumilivu basi: 20th October 2011
- Atangaza kupambana na wote wanaomchafua
- Atazungumzia gamba, Dowans wakati mwafaka
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amesema uvumilivu wake dhidi ya watu wanaomchafua kwa njia mbalimbali kupitia vyombo vya habari umekwisha na sasa ataanza kuchukua hatua za kisheria dhidi yao.
Ndugu wana habari, naamini mmekuwa mkifuatilia kwa karibu habari zinazoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari zinazolihusisha jina langu na harakati kadha wa kadha chafu ambazo hata mimi mwenyewe ninayehusishwa nazo huwa nazisikia na kuzijua baada ya kuwa zimesharipotiwa katika vyombo hivyo vya habari, alisema Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli.
......Alisema kuwa baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, sasa ameamua kuanza kuchukua hatua mbalimbali za kisiasa na kisheria ambazo ameeleza kuwa anaamini zitatoa majibu sahihi dhidi ya wale wote waliokuwa nyuma ya ajenda hizo alizoziita chafu dhidi yake.
Alisema kuwa tayari amepanga kuwasilisha malalamiko yake kwa mamlaka husika zinazosimamia mienendo ya kimaadili na weledi wa kitaalauma wa vyombo vya habari kama vile Msajili wa Magazeti na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
27 Novemba 2010
- Lowassa: Nimechoka kuzushiwa
- Ajipanga kuchukua hatua za kisheria kujisafisha na Mwandishi wetu......
Nimechoka kukaa kimya kila mara zinapotengenezwa habari za uongo juu yangu. Imefika mahali sasa nimeamua kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale ambao kwa makusudi na kwa nia mbaya wanafinyanga uzushi dhidi yangu na wakati mwingine dhidi ya familia yangu, alisema Lowassa aliyezungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana. ..................
Habari hizo zinazomhusu Frederick na ambazo zililitaja pia jina langu hazina ukweli wowote. Nimechoka kuzushiwa na kushambuliwa kwa mambo ambayo si ya kweli. Nimekuwa kimya na sasa wameanza kuichafua hata familia yangu. Nimewasiliana na Frederick mwenyewe ambaye amenihakikishia kuwa tayari ameshaanza kuchukua hatua za kulifikisha suala hilo mbele ya vyombo vya kimaadili na kisheria kama Baraza la Habari Tanzania (MCT) na mahakamani ili kulisafisha jina lake, alisema Lowassa.