Edward Lowassa Richmond kuibuliwa 2008 kama si mapenzi ya Mungu Israel na aseme


Mkuu naona kazi uliyotumwa uko karibu kuimaliza lakini kumbuka sio wote mafala wataokubaliana na hoja zako za kumsafisha huyu Fisadi,kumbuka chama chake na yeye pamoja na mwenyekiti wao ambae ndio Rais Kikwete wote ni wanafiki wakulindana kwa kuwa wote ni wezi so hakuna wakumkamata mwenzie kumbuka Dr Wilbroad Slaa alisema PANYA HAWAKAMATANI SEMA WANAPOKONYANA KILE WALICHOIBA so sishangai unavyomtetea ati sio jembe tu bali ni rato sasa kama yeye hajahusika na Richmond basi aweke hadharani nani alihusika na kama hajahusika ni kwa nini akubali kubeba msalaba wakati muhusika yupo??Tusidanganyane hii yote ni njaa tu hakuna issue hapa
Ili awe msafi moja kwa moja na mumkaribishe Ikulu kama ulivyosema karibu Ikulu basi
ATIRIRIKE LIVE na hata mie hapo nitachuja huo ushahidi wake na hapo hapo atakuwa amesaidia Taifa lake kumkamata mwizi aliyeleta na kusainisha mkataba kati ta Richmond na Serikali ya Bongo.
 
Huyu Mungu bwana, naona anatumiwa kwa kila namna yake, hivi haiwezekani kabisa kuwa Mungu aliruhusu jambo hili limkute Lowasa? au tunataka kusema shetani ndio alisababisha hili jambo limkute Lowasa, je ile kamati ya bunge a.k.a tume ya mwakyembe, ilikuja kwa jina la Mungu au la shetani? tuwekane sawa jamani ili tusimlaumu Mungu au shetani, ama tusimpe sifa Mungu kumbe ni shetani aliyefanya jambo hili..ninachofahamu mimi ni kuwa inatakiwa tumshukuru Mungu kwa kila jambo, na ni afadhali ya jambo lilotokea leo kuliko litakalo kuja kesho
 
kwani ccm haina mtu mwingine zaidi ya lowassa
 

Unadhani mafisadi wanakufa kwa pressure wakati wanaserikali ya kuwalinda? Angekufa Chenge basi vijisent vyake vilipofichuliwa huko ulaya lakini wapi kwanza ndo anadunda ndani ya chama cha magamba anapita bila kupingwa. Pressure itatoka wapi wakati unanyenyekewa kama mfalme ukiwa fidadi papa hapa Tanzania?
 
sasa tuambieni ni nani fisadi wa richmond ebu mwageni ukweli tujue na sisi,ili tujiunge kumsafisa E.L,vinginevyo tutaendelea kuamini hivyo, mpaka pale yeye E.L atakaposema ukweli.

hata akisema, huo hautakuwa ukweli, alitakiwa aseme kipindi kile, kwa kuwa alikubali kuwa chaka la mwenye richmond, yeye ndiyo amekuwa mwenye richmond!!!
Hawezi tena kumrushia mtu mwingine hilo furushi la mavi, lazima lichafue mvi!!!
 
Ndugu Wana Jamvi!
Najua ntapata Matusi na challenge nyingi lakini imebidi niseme.

Mh Lowasa ni chapakazi sana na Atakae bisha Itabidi kabla ya kuchangia bora apitie jf doctor.

Lowasa ndiye kiongozi pekee wa ccm mwenye msimamo na maamuzi yasiyopinda akisema amesema habadiliki.*

Lowasa ni mtu mwenye roho nzuri sana na mwadilifu japo yeye kwenye uadilifu kapitiliza kwa kuwa mwadilifu kwa ccm na serikali yake zaidi ya wa tanganyika.

Lowasa kafanya mengi ya kukumbukwa mfano shule za kata etc. Lowasa Hana tamaa wala sio mropokaji mfano mzuri jiulize ni mwana ccm gani ambaye Yuko tayari kujiuzulu japo ubalozi wa Nyumba kumi bila kufukuzwa au kuamrishwa? Jibu ni no one.

Lowasa alidiriki kuachia uwaziri Mkuu bila kulazimishwa Bali kushauriwa nasisitiza kushauriwa na sio kulazimishwa, natamani lowasa Angekuwa Rais toka 2005 maana Naamini maendeleo yangeonekana kwani asingekuwa na wa kumuogopa lakini kila kizuri hakikosi kasoro.

Inanilazimu kusema lowasa hafai kuwa Rais au kiongozi kwani Yuko tayari kulinda maslahi ya wachache au kikundi kuliko wengi au taifa huo ndio udhaifu wa jembe lowasa ila yeye ni bora kuliko aliye kuweko. Lowasa Ana sifa zote za kuwa leader 9/10% kasoro ni Iyo moja tu wakati JK Ana 2/10%.

Tujiulize swali kabla ya limkibali lowasa kuwa kiongozi japo katibu kata.

(Kama ni kweli kuwa JK ndio Richmond na lowasa alikuwa kondoo wa kafara Kama anavojiita kwanini aliamua kulinda maslahi ya ccm badala ya taifa? Kama aliogopa mtu mmoja na kuwatesa watu 45m for years je wakiwepo wa kumtishia Kama kumi si atatutesa for century au atuache tufe wote?

Kuhusu richmond lowasa Alisema haongei chochote mpaka muda ukifika kwani yeye Ni kondoo wa kafara Kama ninavoamini kuwa jamaa anasimamiaga kauli zake mpaka Leo haja bonga swali najiuliza anasubiria mpaka lini? Au mpaka JK kinga ya urais imtoke? JK na ccm ni bora kuliko watanganyika wote? *Huo ni mtazamo wangu binafsi nanitasimamia msimamo wangu mpaka mwisho lowasa hafai kuwa kiongozi wa taifa bali anafaa kuwa kiongozi wa taasisi au kikundi flani.

Wapambe wa lowasa msitoke povu fikirieni japo kidogo na sio kumtetea mimi binafsi nampenda sana lowasa Natamani sana Angekuwa rais lakini sio 2015 Natamani ingekuwa toka 2005 maana mpaka Leo ungekuta nimemjua real lowasa tujadili Kama taifa na sio mkristo na msilamu CDM na ccm au cuf tujadili kitaifa zaidi think big.

Moderator najua utaifuta hii Mkuu ila sio mbaya maana najua ata wewe ujumbe utaupata maana huwezi futa bila kusoma.

Nawasilisha.
 
Alitaka pia kuleta Mvua ya Kichina pale Bwawa la Mungu lakini wakamzuia!
 
Tutajuta hafai ni mwizi mkubwa tena ni mroho kupindukia kumbuka kauli ya Nyerere alivyomumbua hakika, vibaraka vyake na wakome kutuandikia madudu ya huyu fisadi komeni kabisa, hafai kwa lolote.
E.lowassa ni GOOD FOR NOTHING VERY CORRUPTIVE OLD MAN.
 
Ma pro lowasa watakuja apa na povu likiwatoka ila ukweli utabakia pale pale ni mchapakazi ila hafai kuaminiwa
 
Alitaka pia kuleta Mvua ya Kichina pale Bwawa la Mungu lakini wakamzuia!

hakuna aliymzuia isipokuwa ile nchi aliyokwend kuomba mvua ilipinduliwa madarakani kabla mvua hawajatuletea
 
Mkuu Labda Rais wa TFF au Laigwan wenzake huko masaini
Tanzania wapo zaidi ya watu million 40 na anayepiga kura sio wewe pekee na huwezi kuwaamria wa TZ kutokumchangua Lowassa.
Lowassa atabaki kuwa Rais 2015
 
Alitaka pia kuleta Mvua ya Kichina pale Bwawa la Mungu lakini wakamzuia!

Hapa kwa kweli aliniacha hoi.
PROB ya huyu mtu hakuwahi kukanusha tuhuma zilizokuwa zikimkabiri akaamua kukubali kwa kujiuzuru!
Kwa hilo hafai kwa TZ.
 
Tutajuta hafai ni mwizi mkubwa tena ni mroho kupindukia kumbuka kauli ya Nyerere alivyomumbua hakika, vibaraka vyake na wakome kutuandikia madudu ya huyu fisadi komeni kabisa, hafai kwa lolote.
E.lowassa ni GOOD FOR NOTHING VERY CORRUPTIVE OLD MAN.

Mimi naona FISADI mzuri ni yule ambaye ameiba na amewekeza hapa TZ kama EL kuliko yule wale ambao wameshatuibia na hatujui wamezificha wapi!
 
Ukweli mtupu! Bora Nape!
 
Tanzania wapo zaidi ya watu million 40 na anayepiga kura sio wewe pekee na huwezi kuwaamria wa TZ kutokumchangua Lowassa.
Lowassa atabaki kuwa Rais 2015


Najua Uko kwenye pay slip yake ila ndugu utafua kaniki mpaka itoboke ukidhani una gharisha. Kama Richmond ni JK mbona lowasa hasemi? ****
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…