Edward Lowassa Richmond kuibuliwa 2008 kama si mapenzi ya Mungu Israel na aseme

Edward Lowassa Richmond kuibuliwa 2008 kama si mapenzi ya Mungu Israel na aseme

Baada ya aibu ya mwaka kumshukia waziri mkuu mstaafu bwana sumaye sasa kiwembe kinanolewa kumnyoa Lowassa kwenye uchaguzi wa kugombea ujumbe wa NEC kuwakilisha wilaya ya monduli.
Mpaka sasa Dr Salash Mokosyo anakubalika na wana monduli wengi na kama Takukuru watafanikiwa kuziba mianya ya rushwa basi uchaguzi huu utakuwa ndio mwisho wa siasa za lowassa nchi hii.
Nakutakia Heri Dr na nina amini mizengwe yote unayopigwa na mafisadi itashindwa na wewe kuibuka kidedea.
Wana Monduli twakutegemea
Nb
Nipo monduli na nitawajulisha yote yanatakayotokea huku.
 
Mimi naona FISADI mzuri ni yule ambaye ameiba na amewekeza hapa TZ kama EL kuliko yule wale ambao wameshatuibia na hatujui wamezificha wapi!

Hilo nalo neno iba nje leta ndani lakini hawa mafisadi wetu wanaiba ndani
 
Hapa kwa kweli aliniacha hoi.
PROB ya huyu mtu hakuwahi kukanusha tuhuma zilizokuwa zikimkabiri akaamua kukubali kwa kujiuzuru!
Kwa hilo hafai kwa TZ.


Habari zisizo thibitika zinasema JK alimwambia amuache yeye aendelee ili walindane maana anguko Hilo lilimhusu sana JK na ingekuwa balaa Kama JK angeanguka kwani serikali nzima ya JK ingeanguka na kuishia segerea ikabili lowasa akubali ili kulinda maslahi ya jk na ccm ndio maana mpaka Leo kawa bubu.
 
Najua Uko kwenye pay slip yake ila ndugu utafua kaniki mpaka itoboke ukidhani una gharisha. Kama Richmond ni JK mbona lowasa hasemi? ****
Wewe huielewi nchi hii unaongea tu bila fact zozote.
Je unaushahidi wa Richmond? Au unapayuka tu? Kwanini sasa usimshitaki? kwanini wengine wanashitakiwa?
Lowassa hana doa ni wewe tu Kipofu.
 
usihusishe Mungu na ujinga wa lowasa! hata wewe fikiria wazo lako upya! nchi hii haiwezi kuliwa na panya kiasi hiki. kama umepewa sabuni ya roho na lowasa, imekula kwake mazima! afadhali tumpe mtikila ambaye kila kesi anayoshtakiwa na serikali anashinda!
 
Tutajuta hafai ni mwizi mkubwa tena ni mroho kupindukia kumbuka kauli ya Nyerere alivyomumbua hakika, vibaraka vyake na wakome kutuandikia madudu ya huyu fisadi komeni kabisa, hafai kwa lolote.
E.lowassa ni GOOD FOR NOTHING VERY CORRUPTIVE OLD MAN.

Hivi kabla hujaandika haya maneno kwa wanaJF umejitizama kweli???,mbona inaonekana wewe na EL hamtofautiani lakini kwa nini unamshambulia sana?? Sikiliza nenda kajitizame kwenye kioo kwanza kisha ndo urejee hapa JF na maneno yako hayo machafu.

EL ni Rais 2015

Inawezekana kwa sababu ni mtu ambaye anawajibika,lakini pia ni Mjeshi na nchi hii ukizingatia hapa ilipofika sasa inahitaji mjeshi walau kuirejesha kwenye mstari kidogo.

Mkuu Labda Rais wa TFF au Laigwan wenzake huko masaini

Unakula MSUBA wewe!!!!!!!!!!!!!!!

Najua Uko kwenye pay slip yake ila ndugu utafua kaniki mpaka itoboke ukidhani una gharisha. Kama Richmond ni JK mbona lowasa hasemi? ****

Kaka mbona unajihami sana kuna nini au umetumwa?kwa nini usistulie upate comment kutoka kwa JF,naona kila comment unataka uijibu,au umetumwa na wabaya wa EL???!
 
Mbona hilo ulilosema sisi twalijua, huyu mheshimiwa Lowasa aliubeba msalaba kunusuru chama na serikali yake. nakumbuka wakati nikihudhuria ibada pale Azania Front mwaka wa 2007-2010 kuna mzee mmoja alidiriki kuniambia nihame bench alilokuwa anapendelea kukaa mheshimiwa Lowasa eti ni fisadi, mimi nilimwambia yule mzee usihukumu usije ukahukumiwa, kama hizo tuhuma dhidi yake zingekuwa za kweli huyu mheshimiwa angekuwa amepatwa na pressure na angekuwa mgonjwa kitandani lakini kwa vile hahusiki ndio maana unamuona anaendelea na maisha yake ya kawaida. Nina hakika yule mzee kama yupo hai atakumbuka maneno yangu. Watu wengi siku hizi wana roho za chuki kiasi kwamba busara haina nafasi kwao, nawaasa ndugu zangu tupendane tutakiane mema sio kama najipendekeza isipokuwa nasema kilcho moyoni mwangu.

Wezi wana roho ngumu sana ndugu yangu........kama ulikuwa hujui

kibaka-moto
 
Kumbe ndio maana TBC bado wanatulazimisha tuendelee kutumia akili za Nyerereeee!

Hayo ni mawazo yako Bwana,sio ya wote na hasa mimi,CCM,CDM,CUF,NCCR-MAGEUZI,Vyote havina lolote,kwani lazima rais atokane na chama,mi namsubiri mgombea binafsi.
 
Kichwa cha habari na yaliyoandikwa tofauti kwanini?
 
Binafsi niungane na wale wasemao kila jambo linapotokea kuna sababu. Zaidi ya hili kuna wasemao apangalo Mungu mwanadamu hawezi kulipangua.

Nasema haya kwa moyo wa dhati kabisa baada ya kukaa na kufikiri dhoruba aliyoipata Mhe. Edward Lowassa mwaka 2008 jambo ambalo wahuni wachache waliamua kulitumia ili kumwaribia heshima yake pamoja na kutaka kumchonganisha yeye na Watanzania.

Ila kwa kuwa Mungu hali ugali wala hanywi uji na kwa kuwa vile vile Mungu si Mwakyembe wala si Sitta hata kabla ya muhusika kuwaeleza Watanzania hali halisi juu tuhuma zile Mungu ameanza kuyadhihirisha haya kwa Watanzania bila shaka yoyote.

Alisema yeye si Mungu wa dhuluma wala si Mungu wa visasi ila yeye ni Mungu wa HAKI kwa watu wake wote na haki yake hiyo ndiyo aliyoanza kuidhihirisha mbele ya jamii na hata kuanza kuonekana kwamba hili jembe na huyu Raisi tumtazamiaye alibebeshwa furushi la misuri lisilomuhusu

Japo amekuwa akilaumiwa sana ila imeendelea kudhihirika kuwa yaliyomfanya kufikia uamuzi ule si mengine bali ni maadili yake aliyofundishwa Chamani na hivyo kuamua kuangikwa msalabani ili kuendelea kukipa heshima Chama chake na viongozi wake.*

Niseme tu Edward si jembe tu bali ni rato, reki, beleshi ni kila kitu. Nimejaribu kutazama tu tena kupitia ktk ile Mikoa inayojifanya eti haimkubali Mikoa ambayo haizidi 9 (na naamini tu hawamkubali Mdomoni ila Moyoni jamaa wanamkubali sana).

Katika hii Mikoa sasa, toka Mwaka 2010 ukianzia ngazi ya Kitongoji kila siku iwayo kwa Mungu watu 5-10 humzungumzia na humkubali sana huyu jamaa, ukienda ngazi ya Kijiji ni watu 11-30, Kata ni watu 31-50, Tarafa ni watu 51-80, Wilaya ni watu 81-199, na Mkoa ni watu 200-399 ndio ambao humzungumzia na zaidi humkubali huyu mtu.

Sasa kama hivi ndivyo zidisha mara Mikoa tuliyo nayo mara siku 365 mara miaka iliyobaki ili tuingie kwenye uchaguzi halafu jumlisha utendaji wake halafu vile vile toa maadui zake walioanza kurudi kwake bila kushurutishwa then nipe jibu Uraisi ataukosea wapi Nchi hii.......

Baada*ya hesabu hizo sasa fikiri je huyo balaa aliyepewa jina la Richmond kama angetokea mwaka huu ama mwaka kesho Urais Edward angeupata je manake ingemchukua muda sana kutumia busara kama aliyoitumia toka Mwaka 2008 hadi leo. Mwacheni Mungu aitwe Mungu bana......

You know what Edward; Haters hate b'se they hate seeing you DO BETTER!

Karibu *Ikulu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa........

Hakuna sabuni inayoweza kumsafisha Lowa hasa na rich monduli yake
 
Habari zisizo thibitika zinasema JK alimwambia amuache yeye aendelee ili walindane maana anguko Hilo lilimhusu sana JK na ingekuwa balaa Kama JK angeanguka kwani serikali nzima ya JK ingeanguka na kuishia segerea ikabili lowasa akubali ili kulinda maslahi ya jk na ccm ndio maana mpaka Leo kawa bubu.

Ububu wake unamponza wa TZ hawamwelewi na zaidi wanajua anahusika na ndio maana alikubali kiulaini kuachia ngazi kuliko kwenda mahakanmani kujibu tuhuma.lol!
 
Mbona hilo ulilosema sisi twalijua, huyu mheshimiwa Lowasa aliubeba msalaba kunusuru chama na serikali yake. nakumbuka wakati nikihudhuria ibada pale Azania Front mwaka wa 2007-2010 kuna mzee mmoja alidiriki kuniambia nihame bench alilokuwa anapendelea kukaa mheshimiwa Lowasa eti ni fisadi, mimi nilimwambia yule mzee usihukumu usije ukahukumiwa, kama hizo tuhuma dhidi yake zingekuwa za kweli huyu mheshimiwa angekuwa amepatwa na pressure na angekuwa mgonjwa kitandani lakini kwa vile hahusiki ndio maana unamuona anaendelea na maisha yake ya kawaida. Nina hakika yule mzee kama yupo hai atakumbuka maneno yangu. Watu wengi siku hizi wana roho za chuki kiasi kwamba busara haina nafasi kwao, nawaasa ndugu zangu tupendane tutakiane mema sio kama najipendekeza isipokuwa nasema kilcho moyoni mwangu.
ka hujui nyamaza, huyu ni mwizi tena wa hali ya juu sana!
 
Ndugu zngu habari za leo, ni muda kidogo nilikuwa nje ya ulingo, namshukuru Mungu nipo leo tena, wapendwa wapenda amani na maendeleo ya TZ naomba mkae mchunguze ukweli upo wazi, jamani Kagame ni rais ambaye alitokea jeshini na ameifanya nchi yake kuwa kama ilivyo japo ameiongoza kwa mkono wa chuma kwa muda, lkn leo, kila nyumba pale Rwanda wana ng'ombe wa maziwa waliopewa na Rais wao kwa kuwajali watu wake, rwanda leo ina ndege zinazokwenda mpaka dubai zikichukuwa wa TZ jamani nasema tena, wanaochukia huyu Ndugu yetu Lowasa kuwa rais wanampango wao, lkn kwa hapa tulipo nchi inatakiwa kuwa na kiongozi ambaye hata marafiki zake wamuogope, na waogope ikulu na waogope haki ya wa TZ, fikilini eti TANESCO tena kuna ufisadi sababu, wakubwa hawakupewa ten percent kwa ajili ya vikombe vya kwenye nguzo za umeme, jamani haya mpaka lini? Lowasa peke yake ndiyo mtu atakae tufikisha mahala pakuona mwanga na faida ya rasiimali za zetu. Najua watu wengi mtaendelea kutukana au kusema wanao sema ukweli kuhusu huyu jamaa wamehongwa lkn TZ inahitaji mtu ambaye akikohoa wakuu wa mikoa wanaamka wanauliza tuwasaidieje wa TZ, wakuu wa wilaya wawatetemekee wa TZ wanao hitaji misaada ya serikali.
Ukweli ni taa hatakama ikombali utaiona, japo ni njiti ya kiberiti katikati ya giza la nchi yetu itaonekana Lowassa analifaa taifa letu na siyo CCM, porojo siyo ufanisi, najua Dr, anafaa zaidi lkn wakuu wa mikoa wameteuliwa na CCM kwahiyo Lowassa akisema wote wataogopa kz wataifanaya,
samahani kusema san lkn ukweli umenifanya kusema yote.
Nafikiri mtu pekee ndani ya ccm mwenye sifa ulizotitaja hapo juu ni John Pombe Magufuli, na sio mtu mwingene yeyote.Kwa ufupi ni kwamba mtu pekee ambae watz wanamkubali na kama anagombea urais hata leo anapita kwa 90% ni John Pombe Magufuli!
 
Kumjadili lowassa kwenye viongozi bora ni kupoteza muda. Poor Tanzanians
 
Wewe huielewi nchi hii unaongea tu bila fact zozote.
Je unaushahidi wa Richmond? Au unapayuka tu? Kwanini sasa usimshitaki? kwanini wengine wanashitakiwa?
Lowassa hana doa ni wewe tu Kipofu.


Asante Kama Mimi ni kipofu Sijui nchi inavokwenda lowasa msafi nk. Ila embu JIULIZE kwanza kwanini lowasa hamtaji Richmond ni nani? Anasema kaonewa Ina maana aliye muonea Yuko juu yake au chini yake? Kama ameweza kuficha maovu kwa maslahi ya wachache ndio mtu unayesema anafaa??? Anakufaa wewe Mkuu na ubarikiwe kwa kujua nchi hii Zaidi ya tuijuavo sisi..kifupi nikukumbushe usimdharau usiye mjua huenda Mimi baba yako Kama sio mzazi basi wa kambo Wacha kauli chafu
 
Mleta mada ameorodhesha takwimu wala hakutuambia zimetoka wapi na kwa vigezo gani!

Hsitoria ndio inamhukumu Lowasa.Sio wanaomchukia.
Mwizi ni yule aliyekamatwa na ngozi siyo aliyeiba Ng'ombe.

Midhali jina la Rostam Aziz li hai, Edward Hosea, Mwakyembe, Selelii, Karamagi, Mbuzi wa kafara Msabaha n.k ni kitu kigumu sana kumsafisha huyu bwana.
Midhali dini zipo ushahidi wa matumizi ya dini utajieleza wenyewe

Tatizo la Lowasa si mavazi au kuoga, ni uchafu wa Roho.
ENL ni mchafu wa roho kiasi kwamba anatoa matumaini kuwa akionekane peponi basi vibaka, majambazi n.k. watakuwa na nafasi kubwa tu katika ufalme wa mbinguni.
 
Ububu wake unamponza wa TZ hawamwelewi na zaidi wanajua anahusika na ndio maana alikubali kiulaini kuachia ngazi kuliko kwenda mahakanmani kujibu tuhuma.lol!

Ni kweli Mkuu angeweza kumtaja Richmond ni nani Na ikadhibitika hausiki ningerudisha Imani ila ningemkanya kutokuwa bubu kwenye maslahi ya taifa... Ila it's too late maana Hata akisema Leo Hatuta muelewa
 
Back
Top Bottom