Pasco mkuu nakupa taji kwa kuchanganya na kujichanganya kwa makusudi. Kuwa tu wakwanza kulijuza jamvi kwamba team Lowassa sasa ndani ya PCR (palliative care room) kwasababu kuu tatu . Moja timu hii imegundua kwamba chama hakipo pamoja nao na hii imewekwa wazi na jinsi Lowassa alivyofanyiwa Songea na wakuu wa chama huku hotuba ya JK ikimlenga moja kwa moja. Tathmini ya team Lowassa kwa hotuba ya JK haikufurahisha team na ndio maana sasa mkakati ni kutanganza nia kabla au siku chache baada ya adhabu yake kwisha ili kushinikiza chama kikubali kwa kuuandaa umma.
Pili, ni dhaihiri rais ajaye ni yule ambae hatatiliwa shaka kama ambavyo JK amesema kwenye hotuba Songea na tayari team husika imepigwa nusu-kaputi kwa criteria hii maana mtu wao ndio anayeongoza kwa kuwa na mashaka mengi kupita mgombea yeyote anayetarajiwa. Well labda kamzidi Chenge...sijui. Tatu UKAWA wameamua kutompokea Lowassa endapo atahasi ccm kwasababu kwamba hawataeleweka kwa umma kwa kumpokea mtu waliyemtaja miaka ya nyuma kwamba ni Fisadi Papa. Hii inaondoa plan B ya Lowassa maana team inajikuta ipo kati ya nyundo na jiwe gumu.
Sasa mkuu Pasco amesoma upepo na kutoka na gear ya afya mbaya kana kwamba ubaya wa afya yake umeanza jana.
Mkuu Ugonjwa wa Ukimwi, kwa taarifa yako, chaguo la Kikwete kwa rais ajaye, sio determinant ya nani atakuwa mgombea wa CCM 2015, bali ni persuasive tuu, Mwinyi hakuwa chaguo la Mwalimu, Mkapa hakuwa chaguo la Mwinyi!, Kikwete hakua chaguo la Mkapa!. Determinant ni "wale wapima upepo" kama nia ni CCM kupata ushindi wa kishindo, watapima upepo wananchi wanamtaka nani, jee ni mgombea gani atakayepatia ushindi wa kishindo, then watakielekeza chama ni fulani!.
2005, finalist walikuwa Dr. Salim, Prof. Mwandosya na Jakaya Kikwete, kama ni merits, uwezo, akili na usafi, JK ndie alikuwa mchavu, mzinzi, uwezo duni na kilaza!, lakini ndie aliyekuwa anapendwa, ana sura nzuri, anasmile vizuri, akapitishwa, wale waadilifi, wenye uwezo na briliant brains wakatupwa!. Ndio maana nikasema EL akatwe kwa haki, Ufisadi, Afya sio hoja, hoja ni kukubalika na uwezo tuu!.
Ukawa mpaka sasa hawana mgombea anayekubalika na atakayeuzika kwa urahisi, japo Chadema tayari chaguo lao ni Dr. Slaa, Chadewa wana mtihani mgumu kuwashawishi washirika wao CUF, ambao ni muslim fundamentalists na ma extremist kumkubali ex catholic priest!, CCM wakimtosa EL, akicross into Ukawa, that is the only way wapinzani watakanyaga ikulu ya magogoni na litimie lile neno la Mwalimu "Rais Bora atatoka CCM!", wasiwasi wangu kwa hili CCM inalijua, hivyo wakidhamiria kwa dhati kumchinjia EL baharini, hawatasubiri zoezi la uchukuaji fomu, aje kukipasua chama, watamshungulikia mapema kabla kuhakikisha EL akikatwa, there will be no EL wa ku cross to opposition!, EL nae hili analijua fika kuwa hawezi kuachwa hivi hivi ajiunge Ukawa!, kuliko CCM kumfia mkuu, bora huyo muuaji wa CCM atangulie yeye!, ndio maana EL amemuweka yule 'jamaa' kuwa Mwenyekiti wake wa mipango mkakati!.
Hili la afya mgogoro is just by the look of it with naked eyes, lakini unaweza kabisa kumquat in reality he is as fit as fiddle!, kama Lyatonga Mrema alivyosema jana, japo by the look of him, you can see he is a sick man, mwenyewe kasema haumwi, vyeti vipo, na kaahidi 'hafi mtu!".
Pasco