...Yule Aliyepangiwa na Mungu!.
Wanabodi,
2015 ndio hii, mimi ni miongoni mwa tuliojibainisha wazi, kumkubali Edward Lowassa as "The One and Only" Best President this country can ever have apart from Nyerere!. Hii haina manna Lowassa ndio lazima awe rais. Rais wa Tanzania kwa 2015 ni yule tuu, aliyepangiwa na Mungu, sio lazima awe ni Lowassa, ila kwa vile Mungu bado hajatuambia amempangia nani, kama aliepangiwa na Mungu ni Edward Lowassa, basi ni lazima awe yeye!.
Nakiri nimekuwa inspred kuandika mada hii, kufuaria mchango wa mwana jf huyu kwenye uzi fulani!
Mkuu So Notorious, kwanza nakubaliana na wewe, Pasco huyu unayemjua sasa ni mshereheshaji tuu wa maonyesho ya Saba Saba na Nanenane, kwa nyie watu wa kisasa. Pasco aliondoka rasmi newroom mwaka 2002 na tangu hapo hajawahi kuajiriwa tena, sasa amebaki kama Mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea. Sasa ili kumjua Pasco, rudisha mawazo yako mwaka 2002 ulikuwa level gani, na kuanzia hapo ndipo turudi nyuma!.
Pasco hajawahi kuwa spokesperson wa Lowassa, hajawahi kufanya kazi yoyote kwa Lowassa, hajawahi kuhudhuria press conference yoyote ya Lowassa, hajawahi kuandika au kuripoti news yoyote ya Lowassa na wala hajawahi kufika Monduli, au kuhudhuria zile sherehe maarufu za Monduli!.
Kitu pekee alichofanya Pasco humu jf, ni kumkubali Lowassa, katika ukweli dhahiri usio na mawaa yoyote kuwa ndani ya CCM, Edward Ngoyai Lowassa, ndie the one and only best presidential candidate CCM has, na ikitokea asipitishwe, then asipitishwe kwa haki, vinginevyo patachimbika!.
Hata hivyo kumkubali kwangu Lowassa, ni personal tuu, tena kwa kujitolea, siko Team Lowassa!, sijawahi kuwepo!, wala sijawahi kupokea hata senti moja kutoka kwa Lowassa!, hivyo hoja ya kumlamba mtu miguu kwangu haipo!, ningekuwa mlamba miguu, ningemlamba Mkapa ambaye mtoto wake nimesoma naye darasa moja sekondari kwa miaka minne!, wakati kwa wengine wote Mkapa ni rais, mimi nimekwenda kwake kama baba fulani!. Ningekuwa ni mtu wa kujikomba komba na kujipendekeza, ningejikomba kwa Riz 1, nimekutana nae UDSM na tunaiva sana, hivyo angenishika mkono anipeleke kwa mshure wake!, why nilambe miguu ya mtu?!. Mimi niko kwenye lile kundi la "Maskini Jeuri" kama kina "Kozi mwana mandanda, kulala njaa kupenda!".
Ila pia nina mtu wangu wa karibu kwenye Team Lowassa, hii ndio timu yenye mkono mrefu kuliko team nyingine yoyote so far!. Tatizo langu na timu hii ni moja tuu, hali ya Afya ya Mzee wetu!, kwa vile rais wa Tanzania 2015, ameishachaguliwa na Mungu, then, alilolipanga Mungu, binadamu hawezi kulipangua!, ndio maana kule nyuma Mungu aliwahi kufanya muujiza wa "Jiwe walilolikataa waashi likafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!", na kuna mtu alielezwa kuwa "Wewe ni mwamba, na juu ya mwamba huu, nitalijenga taifa langu!", kwa Tanzania hapa tulipofika, tuna mwamba mmoja tuu, "Mwamba wa Kaskazini!"
Lazima awe!, na asipokuwa basi itakuwa Mungu hakumpangia!, hivyo atakayekuwa rais wetu, 2015, ni yule tuu Mungu aliyempangia!.
Wasalaam!.
Pasco.