Elections 2015 Edward Lowassa sio lazima yeye tu ndiye awe Rais wetu 2015, Rais wetu wa 2015 ni...


well said Pasco,so wote tumshabikia Lowassa tuko c.c.m or after maslahi,wengine tunampenda tu with no reason
 
Last edited by a moderator:

Watu kama ww nilitegemea wathink bigger kumbe ndoroboooo!!
who's this lowasa jmn?? Ushabiki wa kipumbavu huu afadhali tungekuwa wajinga kuliko kuwa wapumbavu!!,
Lowasa lowasa MTU gani anashindwa hata kujenga hoja intellectually?? kazi kuongea subjectively tuu!!
Smart mind zitapima hoja za MTU objectively siyo blaah blaah hapa!!!
Alikua anasubiria uraisi kwa nguvu tangu ajiudhuru sasa akiupata wote waliomkamia kipindi kile atawaswaga!!!
Marafiki & genge lake linalomzunguka la kihuni na matapeli tuu!!
Kwann atumie nguvu nyingi sana kuusaka urais???
Kiongozi bora huombwa kuwaongoza watu kuliko kujipendekeza mwenyew zaidi!!?
NON-ALIGNMENT movement itatusaidia watz, TUACHANENI USHABIKI ZANDIKI nchi ibadilike, LET'S NOT LIVE WITH THE PAST TOMORROW!!!
 
Mkuu Pasco kuna jambo moja umepungukiwa, nalo ni kumsigizia Mungu kwamba atatupangia raisi watz! Nakiri wazi kwamba hili hulitambui kwamba watz hawatapata raisi aliechaguo la Mungu!
Mkuu msnajo simsingizii Mungu, bali hakuna lolote linalojitokea tuu pila kupangwa!, yaani hakuna jipya chini ya jua!, lolote linalotokea liwe zuri au baya, lilikuwa ndilo litokee tena namna hiyo hiyo litakavyotokea!, hiyo yeyote atakayepitishwa kuwa rais wetu, huyo ndiye yule aliyepangwa na Mungu!, anaweza kuwa ni mzuri hivyo Taifa letu likakombolewa na anaweza kuwa ni mbaya hivyo tukawa doomed!.
Asante kuniheshimu, heshima ni kitu cha bure, hata mimi pia naheshimu wote na ndio maana nikipandisha uzi wowote humu jf, kila atakayechangia uzi wangu, anakula like yangu, haijalishi content ya mchango huo!. hivyo asante kwa heshima!.

Hili la CCM kukaa pembeni, siku nyingi nimelizungumza humu, tatizo ni hatuna mbadala!, CCM ikae pembeni tuache vacuum?!. Unless kama unataka kuniambia CCM ikae pembeni na tuijaribu Chadema!, yaani tuifanye Ikulu yetu ni sehemu ya majaribio!.

Hili kuhusu CCM imetufanya nini, nimeisha zungumza sana hapa Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!.
nimesema
 
Nimezisikia hizi tetesi, ndani ya saa 72, nitawaletea majibu!.

Pasco
 
Nilikuwa nalipitia hili bandiko kwenye mukhtadha wa haya madiliko ya Lowassa kuhamia Chadema, nikalikuta bado liko valid hadi October 25!.

Lowassa took a great risk kuhama kutoka CCM, the greater the risk, the greater the rewards!.

Natoa wito kwa wanabodi, mliweke bandiko hili kwenye kumbukumbu yenu, baada ya October tukumbushane,

Mwacheni Mungu aitwe Mungu!, Rais wa Tanzania kwa Awamu ya 5, ni Edwrad Ngoyai Lowassa!.

Pasco.
 

Bandiko liongezewe neno hili The guy in the list of SHAME be a HERO aka FISADI AWA MFALME
 

We ushasema lazina awe afu unasema asipokuwa yeye Mungu hajapanga. So unamlazimisha Mungu?
 
We ushasema lazina awe afu unasema asipokuwa yeye Mungu hajapanga. So unamlazimisha Mungu?
Mkuu All TRUTH, kuelewa nako kuna levels, nakushauri soma tena na tena na tena, kama bado hujaelewa, rudi hapa tutakusaidia kukuelewesha!.

Kusoma huku umetulia na kutafakari, kutakusaidia kuboresha kiwango cha uelewa wako, ila kama kutokuelewa kwako ni levels za uelewa, then hakuna jinsi, bali tutalazimika kukusaidia kukuelewesha!.

Pole!.

Pasco
 
Kama Mungu atatupangia rais mwenye tuhuma za wizi tangu ujana wake, na tena mgonjwa..huyo Mungu atakuwa mwenyekiti wa CCM anaekutana na wezi kwenye kiti cha enzi (ikulu)

Nimecheka kwa sauti mie ......ahsante kwa kunichekesha mkuu
 

Kwanza kabisa kupitia uzi huuu nikiri tu na kusema ndio nimeelewa kuwa kumbe wewe ni Pasco wa PPR.
Anyway, tuyaache hayo. Nikija kwenye huu uzi nilipopigia mistari humo ndio kunakonipa ukakasi.
Leo hii wewe Pasco kusema kuwa wewe ni maskini wa kutupa nakataa kukubaliana na wewe hata uainishe vipi aina za umaskini unazozijua. Nadhani hujatembea kiasi cha kutosha Tanzania hii kujionea maskini wa kutupa wanafananaje ingawa 7 7 inafanyika mara kwa mara Dar es Salaam na Nane Nane inafanyika Dodoma na Lindi bila kusahau miko mingine kama Morogoro na Arusha, hakika kwa ushereheshaji wako wa matukio haya lazima utakuwa ushapata nafasi ya kutembelea sehemu hizi. Sitaki kuzichambua aina za umaskini lakini kwa hili la wewe kujiita "maskini wa kutupa" naomba urudi magotini ukamuombe Mungu msamaha kwa kuendana kinyume na uhalisia wa maisha yako.

Pili nadhani nimejibu katika kipindi tofauti na mda ulioandika uzi huu. Wakati unaandika uzi huu kilikuwa ni kipindi ambapo Lowassa bado alikuwa CCM na sasa hali ya kisiasa imebadilika kwa kiasi kikubwa na sasa Lowassa yuko UKAWA kwa tiketi ya CDM. Sijui umeliangaliaje hili kwa mapana yake.

Tukutane Nane Nane Dodoma pale wiki ijayo tutaongea mengi zaidi baada ya mahojiano ya TV
 
Last edited by a moderator:
Tulipoitahadharisha CCM kutenda haki, vinginevyo 'patachimbika!', tulibezwa sana humu!, leo Mwenyekiti wa CCM Arusha amehamia Chadema, huku ndiko kuchimbika kwenyewe!, sasa ni rasmi kuwa mkoa wote wa Arusha mzima mzima ni Chadema!, CCM haiwezi tena kushinda hata udiwani!, na huu ni mwanzo tuu, kilele ni tarehe 25 October, pale Utukufu wa Mungu, utakapodhihirishwa kwa Tanzania, kwa 'jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!.

Jumapili Njema.

Pasco
 
Mimi nilisema sio lazima Lowassa, wasikilizeni hawa wanasema nini?
 
Lowassa ndie raisi wa awamu ya 5 wa JMT iwe Mungu amepanga au la
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…