Edward Ngoyai Lowassa anaumwa, alazwa ICU Muhimbili

Edward Ngoyai Lowassa anaumwa, alazwa ICU Muhimbili

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.

Taarifa kutoka kwa familia hiyo zinasema kuwa kiongozi huyo amelazwa katika hospitali hiyo kwa karibu wiki nzima baada ya kufanyiwa upasuaji.

Akizungumza leo Ijumaa Januari 28, 2022 na Mwananchi, Mbunge wa jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa ambaye ni mtoto wa Lowassa amesema baba yake alilazwa katika hospitali hiyo alipopatwa matatizo ya tumbo.

"Baba alilazwa kama siku tano zilizopita. Wala haina siri, alifanyiwa upasuaji wa tumbo, lakini bahati mbaya ikaleta complication (hitilafu). Alifanyiwa hapo hapo Muhimbili,” amesema Fredrick.

Amesema wanaomba watanzania, kuendelea kumuombea ili afya yake iendelee kuimarika

"Tunashukuru sana kwa maombi ya Watanzania na tuna imani ataruhusiwa kurejea nyumbani," amesema.
 
Kawaida sana.

Hata mimi nilishafanyiwa Sigmoid Resection pale Kairuki.

Utumbo ulikua umejikunja, wakachana hapa tumboni, wakakata utumbo.

Kisha wakaunga tena.

Hali hii humtokea mtu yeyote.

Nampa pole.

Mie nilishatengemaa, sema ndio hivo tena, baadhi ya mazoezi siwezi (naogopa) kufanya, mfano katatumbo - ile ya kuondoa kitambi.
 
Huyu ndie alifaa awe raisi baada ya JK sema tu fitina za JK na Ben
 
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa amelazwa kwenye Hospital ya Taifa ya Muhimbili.

Kwa mujibu wa taarifa toka ndani ya familia inasema alilazwa hapo kwa wiki sasa kutokana na kufanyiwa upasuaji wa Tumbo.

Taarifa hizo zinasema alipata complication kidogo baada ya kufanyiwa upasuji, lakini hali yake inaendelea vizuri.

Admin naomba uunganishe na thead hii kumbe tayari ipo hapa muda mrefu

Asante

 
Yeye Lowasa aliwaomba radhi lini Watanzania waliomwamini na kumpigia kura zaidi ya million 6?
Watu million sita ni wengi Kiasi Kwamba laana yake haiwezi kusambaa kwa Wote na ikawadhuru!! Lakini huyu Nape ni mmoja peke yake aliyekuwa anamrushia Edward matusi ya nguoni!!! Alitakiwa ampe Heshima ile ile anayompa Mwandosya!!!
 
Nape kama ana akili , huu ni wakati wake muafaka kukimbia na kwenda kumuomba msamaha Edward; asipofanya hivyo laana ya Lowassa itamuandama hadi kaburini!!!
Laana imuandame yeye(Manvi) km Nani!?
Huyo ndo baba Jeni baibai.
 
Pole Sana Mzee wetu. Tunakuombea mno. Unastahili heshima. Moyo mweupe usiyo na kinyongo. Umesaidika wengi Taifa hili wakubwa kwa wadogo. Mzee mkarimu Sana. Maombi ya uliowagusa yafanye KAZI hakika
 
Pole sana Boss wangu. Mbele ya Mungu utapona na kutoka hospitalini.
 
Back
Top Bottom