Kwahiyo mkuu unataka kusema shule zote nchini zinafundisha kwa kiingereza? Kwa exposure ya Messi utasema hadi leo asijue kiingereza kweli?
Wakati huko Argentina aliondoka muda mrefu! Wakati Samatta amesoma shule za Kayumba akaingia moja kwa moja kwenye mpira hicho kiingereza angekijulia wapi?
My point is usijivunie kujua kiingereza wakati hakuna kilichokusaidia! Na wala siyo kwamba kujua kiingereza ndiyo kipimo cha akili ya mtu hilo halipo wala tusijidanganye!
Haya tuache mifano ya watu binafsi tuje kwenye nchi. Angalia China kule kiingereza hawakijua na hawakipendi ila angalia level yao ya maendeleo na lugha yao inavyoheshimika!
Halafu angalia nchi kama Kenya ambao wanajivunia kujua kiingereza! Yaani wanakihusudu kiasi kwamba wanatubeza watanzania na kuona kama wote hatukijui lakini wako wapi!