Mkuu ni jukumu la jeshi kumkemea na kumpiga marufuku ili lisijitokeze kwa wengine! Ni kinyume na maadili ya kijeshi kwa mtu kutaka utukufu binafsi..
Mkuu nafahamu vipo vitu vingi ambavyo Marekani wanadanganya dunia lakini kwa hili la Osama hapana.. Wadanganye ili wapate faida gani?? Why should they go to such length kutengeneza hoax ya kiwango hiki?? Ili waachive kitu gani??
Ati Osama ni operative wa Marekani??
Wamarekani wana mapandikizi ya kutosha huko mashariki ya kati lakini Osama not one of them..
Tukumbuke watu zaidi ya 3,000 walikufa pale NY siku 9/11.. Ni rahisi kwetu kuongelea kiwepesi wepesi kuwa wamarekani wamejilipua kwasababu hatujui uchungu ambao wamarekani walipitia kwenye tukio lile..
Ati walijilipua ili wakavamie middle east kuiba mafuta!! Really??
Hakuna kiwango cha mafuta kinachoweza kufikia thamani ya ya rasilimali na roho za watu zilizopotea siku ya 9/11.. Ni rahisi kwetu kujadili kirahisi rahisi kwa kuwa hatujui uchungu waliopitia wenzetu.
Kama zikiendelea stori tu pasipo concrete evidence!! Nitakuwa binadamu wa mwisho duniani kuamini Osama yuko hai, operative wa CIA, wamarekani walijilipua.