Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mgombea wa Chama cha ACT-Wazalendo Jimbo la Sumbawanga Mjini, Edwin Kachoma, ametangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro cha Ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kachoma amesema sababu kuu ya kujitoa ni kukosa ushirikiano kutoka makao makuu ya chama, ikiwemo kushindwa kumpatia vifaa vya kuendesha kampeni kama vile bendera na nyenzo nyingine muhimu.
Uamuzi wa Kachoma unakuja katika kipindi ambacho vyama vya siasa nchini vinaendelea na kampeni huku wagombea wa vyama vingine wakiendelea na mikutano na mikakati ya kuwanadi kwa wapiga kura.