GE2025 Edwin Kachoma Ajiondoa Kugombea Ubunge Sumbawanga Mjini Kupitia ACT-Wazalendo

GE2025 Edwin Kachoma Ajiondoa Kugombea Ubunge Sumbawanga Mjini Kupitia ACT-Wazalendo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mgombea wa Chama cha ACT-Wazalendo Jimbo la Sumbawanga Mjini, Edwin Kachoma, ametangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro cha Ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kachoma amesema sababu kuu ya kujitoa ni kukosa ushirikiano kutoka makao makuu ya chama, ikiwemo kushindwa kumpatia vifaa vya kuendesha kampeni kama vile bendera na nyenzo nyingine muhimu.

Uamuzi wa Kachoma unakuja katika kipindi ambacho vyama vya siasa nchini vinaendelea na kampeni huku wagombea wa vyama vingine wakiendelea na mikutano na mikakati ya kuwanadi kwa wapiga kura.

Hilo jina tuu, kachoma linaakisi
 
Huyo jamaa ni mtu wa serikali. Alifanya hivyo makusudi kwa maelekezo maalumu. Hao Ngogwe waliambiwa No reforms No election wakaingia kichwa kichwa.
Wanasema mhuni hasusiwi, waache waingie ghetoni kwa muhuni halafu wakitoka na maumivu tutawapa pole maana tuliwakataza wasiingie wao wakalazimisha.
 
Kweli kabisa, hasa wapinzani wenyewe wakiwa wa aina ya tapeli Mbowe.
Mtaandika sana kujifariji lkn uhalisia na mziki mmeuona nawashangaa sana mnamuwaza tapeli na chama kawaachia sasa shida yenu nini? Wahenga walisema wimbo wa kujifunza haukeshi ngomani!
 
Back
Top Bottom