Edwin Odemba Tafuta Hela Ukodishe Star TV Kwa Mzee Diallo

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
13,417
Reaction score
23,310
Screenshot_20240817_194105_Google.jpg

Kwa sasa huwa naangalia Star TV vipindi 2 tu; Medani za Siasa na BBC ambacho Star TV wanakipitisha tu kwenye kituo chao.

Star TV kwisha kabisa haina vipindi vyenye mvuto zaidi ya Medani za Siasa cha Edwin Odemba aka Chief Odemba

Huyu nguli wa maswali ambayo ni multi task, multi discipline ni sawa na tembo aliyejificha sebuleni. Uwezo wake ni mkubwa kama yule Mganda wa VOA aliyestaafu Shaka Ssali enzi zake.

Kuendelea kutumikia STAR TV kwa namna yeyote ni sawa na kuchimbia shekeli ndani ya udongo (Mathayo 25:14-30)

Ushauri:-
(1) Tafuta tajiri mwenye hela kisha ingia mkataba uikodishe Star TV kutoka kwa Diallo.

Au

(2) Ondoka Star TV nenda kwenye TV Station kubwa ukakuze brand yako
 
Odemba anajitahidi ila bado ni mweupe kwenye mambo ya imani. Juzi nimeona analazimisha kuuliza Yeriko Nyerere akiri kwamba anaishi kwa sababu ya Mungu, Yeriko namwambia yeye anaamini mizimu ya kiafrika, aodemba analazimisha kwamba ni Mungu.

Odemba anapaswa kufahamu kwamba haya mambo ya imani, imani yako sio lazima iwe imani ya mtu mwingine. Kama yeye anaamini Mungu basi aelewe kuna wengine hawaamini hicho kitu kinaitwa Mungu.
 
Unaamini kuwa Yeriko sio mkristo?
 
Anajitahidi sana tena sana.

Atazidi kuwa vyema zaidi Akiboresa pia na ile ongea yake ya nukta ambayo inakula muda.

Aongee kawaida tu anajitahidi,niliona juzi alivyokuwa anambananisha bwana yericko nyerere na yule mkuu wa wilaya ya ubungo.

Kongole kwake.
 
Binafsi nawakubali mno wanahabari ambao wanawabananisha watu mpaka wanajuta kwenda studio
 
Odemba anajitahidi ila bado ni mweupe kwenye mambo ya imani. Juzi nimeona analazimisha kuuliza Yeriko Nyerere akiri kwamba anaishi kwa sababu ya Mungu, Yeriko namwambia yeye anaamini mizimu ya kiafrika, aodemba analazimisha kwamba ni Mungu.

Odemba anapaswa kufahamu kwamba haya mambo ya imani, imani yako sio lazima iwe imani ya mtu mwingine. Kama yeye anaamini Mungu basi aelewe kuna wengine hawaamini hicho kitu kinaitwa Mungu.
Siyo kwamba Odemba alimlazimisha Yericho aseme anaishi sababu ya Mungu, bali ile ni tekniki tu ya kumbana muulizwaji atoe jibu sahihi
 
Back
Top Bottom