EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi

Mbona Majizzo amekwambia wasikizaji wake awakufurahishwa na kauli ya Hando ndio maana ameamua kumchukulia hatua tatizo sisi tunataka kulaumu atakisichokuwepo
Unaamini ulichokiandika,alichosema Majizo au nguvu iliyo nyuma ya kuomba msamaha?Kalaga baho mwanakwetu!
 
Hili tukio limenigusa sana, sasa kosa la Hando ni lipi?
Kutoa maoni yake? au?
Hivi nchi yetu ni ya hovyo kiasi hiki?
 
Hayo maoni angeyaweka kwenye page yake ya IG au FB wala Sio tatizo.

Ishu ni kutumia ofisi ya mtu kutoa misimamo yako binafsi... Inaleta sintofahamu kujua ni msimmo wa kampuni au msimamo wa mtu binafsi. Kuliondoa hilo ndio wenyewe wametoa ufafanuzi.

Hayo ya kuchukuliana hatau kiofisi watajuana wenyewe kulingana na sheria na miongozo ya Sehemu za kazi. Nadhani kila mahali Kuna taratibu zake.
 
Of course au kwenye site Wapinzani nk maana Ile tv anakofanyia kazi haijasajiliwa Kama chombo Cha mlengo fulani au Kama ana akili angemualika mtu back kwenye kipindi ndio afikishe hayo maoni yake.
 
Wewe ndoumelewa
 
Magufuli alikuwa kiongozi mzuri lakini kwenye swala la kuabudiwa na watu kujikombakomba kwake aliharibu. Maadili ya viongozi/waandishi wahabari/raia wengi yapo kwenye kujikomba,kusifia uongo,uoga ili mradi mambo yaende.Mbn wakati wa Jk watu walikuwa wanaongea tu na kusikilizwa
 
Ona kundu hili muda wote kusifia tu
 
jamaa anahofia watamfukunyua ishu za poda. Wanapigania uhuru wa habari gani sasa hawa wajinga.
 
Chama cha mambuzi kwenye ubora wake. Serikali ya Samia sawa na Magu tu hawataki kusikia hoja mmbadala. Jizo kapima upepo BAADA ya kupokea simu kadhaa akaona familia yake isijelala njaa. CCM kukupoteza kwa maslahi yao binafsi Sio shida kwao. Wanachotaka kusiki ni kuwa wanaupiga mwingi baaaasi.
 
Sisi tusifu tu tusikosoe..Huu ndio ugonjwa utaoimaliza hii nchi...
 
Yaani tabia ya kujikombakomba imekua ndio life style. Imefikia hatua nikamsikia binadamu mmoja anayeitwa mchungaji naye anahimiza Watu wawe wanajikombakomba ili wafanikiwe.
 
Sisi tumeridhika na hii katiba, nyie walafi wa madaraka ndio mnapanga kuweka vyeo humo mara sijui serikali za majimbo, lengo lenu kula Hela za wananchi kwa mtaji wa kupiga domo

Wanaotaka katiba bora ndio wenye ulafi wa madaraka, ila wanaopora uchaguzi hao hawana ulafi wa madaraka! Uza ubongo huo bro maana unakaa nao kwa hasara.
 
Kwani Hando kapewa onyo na Serikali au mmiliki wa Taasisi? Mwenye radio yake na wasikilzaji wa hiyo radio wameona alichokisema Hando akina afya kwa radio yao ndio maana wanataka kumchukulia hatua

Utakuwa mwendawazimu kufikiri eti wenye kituo wamembana mtangazaji wao bila shinikizo la dola. Kila mara huyo Hando anaongea maneno ya hivhivyo dhidi ya wapinzani na hawamchukulii hatua, ila kaongea dhidi ya serekali ndio anabugudhiwa.
 
#Gerald ameukosea umma wa watanzania, ameonyesha yeye ni mtu wa aina gani ya kwamba hukumbuki hata hatua chache ya kule tulipotoka, pia amejitoa ufahamu ya kwamba hukumbuki hata awamu ya tano ndiyo iliyokuwa inakopa huku ikiuhadaa umma tunajenga kwa fedha za ndani, amejitoa ufahamu hukumbuki tena, au alitaka serekali iwe inakopa kwa siri siri kama awamu iliyopita?, kuweka mambo wazi imekuwa tatizo?, alitaka tufichwe fichwe,
(homeboy what are you doing man?) umeanza kupasha nini mkuu?,
Namuomba waziri nape, umma wa watanzania na Mh. Rais wetu mpendwa, TULIPUUZE SUALA HILI NA TUSILIPE UZITO WOWOTE,
TUSONGE MBELE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…