EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi

Sawa unajiona nawe upo kundi la wasomi?
Pole endelea kutafuta ugali wa wanao na ada na kodi ya nyumba.
Siyo kwamba nipo kundi la wasomi, Mimi ni msomi mbobezi ambaye nimetengeneza wasomi wengine. Usicheze na MBA
 
Ni kweli siyo kila mwenye PhD au Masters anaweza kuongea eneo lolote bali eneo husika na fani yake. Kama huna shahada ya uchumi au fedha yeyote huwezi kuongea kwa uafasaha hoja za uchumi.

Nyie ambao hamjasoma ndiyo kabisa mnatupotezea muda bure kwa kuendelea kubishana badala ya kujifunza.

Bunge lilipitisha Bajeti ya Tsh 42 Trllioni yenye nakisi dhidi ya mapato ya Tsh 19 Trillion, je Gerald Hando anadhani nakisi itazibwa na nini?

Miradi mikubwa ya SGR, JNHEPP, Busisi na Makao Makuu Dodoma ndiyo vinakula sehemu kubwa ya mikopo
 
Athari za mikopo kwa uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja haihitaji Masters kujua.
Msiwazibe wananchi midomo kwa kivuli cha elimu, kila mmoja ana haki ya kutoa maoni maana hiyo mikopo italipwa kwa kodi zetu.
Maoni hayakatazwi na wala hawezi kupata shida kwa hilo. Tatizo yeye ni mtangazaji nankatumia chombo cha mwajiri vibaya kuelezea maoni binafsi.

Kama unajuwa newsrooms zina watu wanaitwa News Editors, ndiyo wenye kazi za kuchuja habari ili wananchi wapate habari ambazo ziko na maadili na haziko biased.

Hando anaadhibiwa na mwajiri wake siyo Serikali. Mwajiri hakumtuma kuongea ile taarifa ambayo ilikuwa haija tafitiwa vya kutosha
 
Swali letu limelenga kujua hatua alizochukuliwa tu , kwa nchi isiyo ya kidemokrasia kama Tanzania yote uliyoyaandika ni sahihi
Suala la hatua atakazochukuliwa ni kati ya mfanyakazi na mwajiri wake. Hata huko kwenye nchi unazozifaham kwenye ukomavu wa demokrasia, lazima uheshimu na kuzingatia miiko ya kazi.

Kwenye kibarua changu nikionekana na jezi ya chama chochote Cha siasa itakua tayari nimeshatengeneza mgogoro na mwajiri.

Hata nikiongelea jambo lolote kuhusu mwajiri bila ruhusa au maelezo maalum napo nakua matatani. Wasichotaka ni maoni yangu kuchukulia kama msimamo au maoni ya mwajiri.
 
Naona moja ya adhabu aliyopewa na mwajiri wake ni kutokuwa hewani.
Nimemsikia baby mama, Kitenge na Mussa tu kwenye magazeti.
kwanza sijui kama likizo ya baby mama ilikuwa imeisha vizuri.
 
Majizo anafahamu fika hiyo redio aliipataje,anafahamu kuwa siyo msafi na anajua halipi Kodi na tozo inavyostahili.Alichofanya ni kuokoa biashara yake.
 
Utakuwa mwendawazimu kufikiri eti wenye kituo wamembana mtangazaji wao bila shinikizo la dola. Kila mara huyo Hando anaongea maneno ya hivhivyo dhidi ya wapinzani na hawamchukulii hatua, ila kaongea dhidi ya serekali ndio anabugudhiwa.
Unajua Majizzo ni chama gani? Inawezekana Majizzo amekerwa na tabia ya Hando kuwasema na kuwakosoa hadharani viongozi wa chama chake
 
Mkuu Satoh je unamjua mtu mmoja wa kuitwa DR Ulimboka!!? Huyo Ulimboka yalimpata ya kumpata kipindi cha JK!!
Mkuu kipindi cha Ulimboka kama ulikuwepo je kwa aliyoyafanya Ulimboka alistahili kuonewa huruma je unajua ni watu wangapi walikufa kwa sababu ya Ulimboka? Alichokipata Ulimboka alistahili tena alikipata kidogo alionewa huruma
 
Mkuu tatizo watu humu wanapenda kujisahaulisha mdogo wa Heche alimvua Mzee wa watu fulana yenye nembo ya CCM kwa madai nyumba Ile ni Chadema na maneno mengi ya dhalau Mzee wa watu alivua fulana yake ndio akapata kazi na akaambiwa asiludie tena
 
Unajua Majizzo ni chama gani? Inawezekana Majizzo amekerwa na tabia ya Hando kuwasema na kuwakosoa hadharani viongozi wa chama chake

Hao akina majizo hata kama wako CCM sio kwasababu ya kuamini itikadi yake, bali ni kama kinga ya biashara zao zenye makandokando.
 
Unajua Majizzo ni chama gani? Inawezekana Majizzo amekerwa na tabia ya Hando kuwasema na kuwakosoa hadharani viongozi wa chama chake

Amepost akiwa msoga- chalinze bila shaka aliitwa na ile familia. Mtu amekaa zaidi ya siku 3 ndo azungumze? Kwanini asizungumze siku ile hando alivyofunguka?? Aliitwa msoga uyo
 
Na wewe ni walewale tu "a functional illiterate" na degree yako uchwara. You can not think out of the books you were forced to read in school! Shame.
 
Hao akina majizo hata kama wako CCM sio kwasababu ya kuamini itikadi yake, bali ni kama kinga ya biashara zao zenye makandokando.
Ilo naweza kukubaliana na wewe sasa wakati wao wanaficha makandokando yao alafu anatokea mtu anataka kuwaharibia si inabidi kumshughulikia
 
Amepost akiwa msoga- chalinze bila shaka aliitwa na ile familia. Mtu amekaa zaidi ya siku 3 ndo azungumze? Kwanini asizungumze siku ile hando alivyofunguka?? Aliitwa msoga uyo
Akuposti akuwa Msoga ameposti akiwa Msata wewe unajua Majizzo kwa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…