EFTA kukusanya Sh50 bilioni kwa ajili ya wajasiriamali wa kilimo, usafirishaji

EFTA kukusanya Sh50 bilioni kwa ajili ya wajasiriamali wa kilimo, usafirishaji

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014

Nicomed Bohay - EFTA
Taasisi ya fedha Equity for Tanzania (EFTA) imezindua hatifungani ya Sh50 bilioni kwa ajili ya kukopesha vifaa vya killimo, usafirishaji na ujenzi.

Akizungumza katika uzinduzi huo leo Februari 10, 2026, Mkurugenzi Mtendaji wa EFTA, Nicomed Bohay amesema kuwa wamefikia hatua hii ili kukidhi mahitaji ya wateja katika mikopo ya uzalishaji.

“Leo kwa mara a kwanza tumezindua bond kwa mara ya kwanza. Taasisi yetu imekuwa kwa zaidi ya miaka 20, tumeweza kujenga mifumo ya uongozi ya kudhibiti hasara na tumefikia muda ambao tuko tayari kuingia kwenye soko la mitaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta za uchumi,” amesema.

Amesema kipaumbele katika hati fungani hiyo ni sekta ya kilimo, “tunatarajia angalau asilimia 50 ya uwekezaji wetu uwe kwenye kilimo, kwa mfano matrekta, mashine za kusindika mazao ya kilimo, nashine za mafuta, kusaga, magari ya kusafirisha mazao kutoka vijijini na kuleta masoko makuu mijini.”

Amesema pia wataangalia pia sekta ya ujenzi kwa kukopesha vifaa vya jenzi wa majengo na barabara.

Pia kuna sekta nyingine tutaziangalia kama ujenzi, bulldozer, mashine za ujenzi, mashine za kuchimba barabara.

Alisema kiwango cha chini katika uwekezaji huo kinaanzia Sh500,000, ambapo fedha zitakazopatikana zitatumika kununua mashine kwa ajili yakukopesha wajasirimali.

“Manufaa ya uwekezaji ni bondi pekee ambayo inafaida kubwa kuliko bondi zote za Soko la Fedha la Dar es Salaam. Hakuna bondi inayofikia asilimia 14 kama kwetu. Pamoja na kutoa feida nzuri kwa wanaowekeza, lakini wajasiriamali na wakulima wanakwenda kufaidika.”

Kuhusu marejesho ya mikopo alisema ni ni tofauti na benki zinazotaka yalipwe kila mwezi. “Sisi tunakwambia ni zigzag, kwamba utalipa leo mwezi ujao hulipi, mwezi huu nitalipa Sh800,000 mwezi huu Sh1 milioni mwezi huu hulipi, mwezi huu Sh3 milioni. Marejesho kaka haya hayapo kabisa kwenye taasisi nyingine za fedha lakini EFTA unaoangalia mzunguko wa fedha katika biashara husika.”

David Magambe aliyewakilisha Mamlaka ya Mitaji na Masoko (CMSA) amesema EFTA imekidhi matakwa ya kisheria ya kuuza hati fungani.

“Kwa mantiki hii mauzo ya hati fungani ya EFTA yamekidhi matakwa ya sharia. Napenda kuipongeza bodi na menejimenti ya EFTA kwa kukidhi masharti haya.

“Utoaji wa hatifungani unatoa matumaini katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya sekta ya fedha unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka 10 ulioanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2021 na utatekelezwa mpaja mwaka 2029/30. Lengo ni kuwekeza upatikanaji wa fedha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo,” amesema.


David Magabe -CMSA


Profesa Andrew Temu
 
Ni jambo jema sana. Tunaomba msimamie mitaji ya watu vuzuri
 
Sijui hii corporate bond ilichangamkiwa kwa kiwango gani ngoja tusubiri matokeo!
 
Back
Top Bottom