olimpio
JF-Expert Member
- Apr 5, 2023
- 418
- 866
Sio jambo rahisi sana kujitoa mhanga kuyasema haya, na kipekee nimshukuru Maxence Melo kwa kuweka jukwaa hili; linasaidia sana kupashana habari.
Niwafungue macho kidogo: eGA kupelekwa wizara ya TEHAMA ni jambo lililojaa siasa kubwa sana na uhalifu mkubwa kwa nchi, ni jambo ambalo wametengenezwa wabunge kadhaa akiwemo Kingu na Lugangila ili wasaidie kupush agenda ya kuitoa eGA Wizara ya Rais UTUMISHI, tukumbuke kuwa unyeti na usiri wa mifumo ya Serikali pamoja na taarifa zilizobebwa zilikuwa mikononi mwa eGA, ndio maana eGA hivi karibuni ilihamishwa toka UTUMISHI na kupelekwa IKULU ili kudhibiti wanasiasa waliokuwa wanainyemelea. Over night, genge likaibuka na kuanza kutengeneza propaganda kuwa mifumo ya Hospital kama CT SCAN haisomani hivyo eGA ihame toka UTUMISHI.
Maswali ya msingi: Ni kweli Muhimbili na Bugando hazisomani? Kwanini Waziri aliamua kupotosha? Na kwanini analazimisha eGA ihamie kwake? Tena karibu na Uchaguzi Mkuu? Anataka kufanya nini kwenye mifumo yenye taarifa nyeti za Serikali? Kama hakuna ufanisi huko wizara ya TEHAMA kuna ufanisi gani, mbona ICT Comission inawafia? Kwanini eGA ilihamishiwa ikulu miezi mitatu iliyopita?
Msichokijua ni kuwa kabla ya Bunge la Bajeti, waziri wa TEHAMA aliwapanga wabunge hapo chini ili watie petroli suala hili.
Kingu anasikika akitaka iletwe Sheria eGA waache kutengeneza mifumo, KWELI? Mnajua nani wanataka atengeneze? Tayari kuna makampuni yao ambayo wameya-position kuchukua tender za mifumo ya Serikali. Sio makampuni ya kitanzania kama mnavyodhani, ni makampuni ya nje yaje yasimike mifumo ya mailing system , e-office yenye nyaraka za Siri za Serikali na mifumo ya malipo (GePG) wanakwenda kuwa phased out, control number inaenda kuuawa na kampuni ya kigeni wanaileta.
Watu wana macho ya nyama sana, hawayaoni haya! Jaribuni kuwaza kwanini baada ya kusema wanahamisha eGA tayari wanaanza kupeleka mabadiriko ya sheria ya kuzuia eGA kutengeneza mifumo? Wanafanya haya kwa ajili ya nani? Wanasiasa wanataka pesa za damu wakamalize Uchaguzi wao. Wanafanya hayo kwa kuua ndoto za vijana wa kitanzania!
Reference ziko hapa muone jambo hili lilianza zamani sana. Gusa hapa - Tetesi: - Wanasiasa na mipango ovu ya kuiua E-GA
USALAMA WA TAIFA WAPO KWELI? Inakuwaje whistleblower anatoa taarifa ya hatari namna hii juu ya genge la watu serikalini kuua taasisi systematically over a year ago (May 2023), Idara haifanyii kazi mpaka watu hawa waovu wanafanikisha mipango yao?
Ingekuwa taarifa ya Lissu au Mbowe kutishia kuhujumu nchi mngekuwa kimya? Inakuwaje watu wachache wanaamua kuua taasisi nzima ili wabinafsishe kazi za mifumo zenye nyaraka za siri za nchi na ninyi mpo? Ni kweli bado mko kwenye nyakati za giza bado ? Hamna wataalamu wa TEHAMA wa kujua mambo haya?
NI AIBU KUBWA SANA, mkutano wa kwanza ulifanyika Wizara ya Fedha na Mipango wakati huo hata Nape hajawa Waziri, script nzima mliandikiwa mmeshindwa nini?
Nawasilisha nikiwa naumia sana kwakuwa watu wanadanganywa na wanaua taasisi yenye ubunifu, kama sio kuhujumu nchi hiki ni nini?