eGA inauawa rasmi?

eGA inauawa rasmi?

olimpio

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2023
Posts
418
Reaction score
866
Sio jambo rahisi sana kujitoa mhanga kuyasema haya, na kipekee nimshukuru Maxence Melo kwa kuweka jukwaa hili; linasaidia sana kupashana habari.

Niwafungue macho kidogo: eGA kupelekwa wizara ya TEHAMA ni jambo lililojaa siasa kubwa sana na uhalifu mkubwa kwa nchi, ni jambo ambalo wametengenezwa wabunge kadhaa akiwemo Kingu na Lugangila ili wasaidie kupush agenda ya kuitoa eGA Wizara ya Rais UTUMISHI, tukumbuke kuwa unyeti na usiri wa mifumo ya Serikali pamoja na taarifa zilizobebwa zilikuwa mikononi mwa eGA, ndio maana eGA hivi karibuni ilihamishwa toka UTUMISHI na kupelekwa IKULU ili kudhibiti wanasiasa waliokuwa wanainyemelea. Over night, genge likaibuka na kuanza kutengeneza propaganda kuwa mifumo ya Hospital kama CT SCAN haisomani hivyo eGA ihame toka UTUMISHI.

Maswali ya msingi: Ni kweli Muhimbili na Bugando hazisomani? Kwanini Waziri aliamua kupotosha? Na kwanini analazimisha eGA ihamie kwake? Tena karibu na Uchaguzi Mkuu? Anataka kufanya nini kwenye mifumo yenye taarifa nyeti za Serikali? Kama hakuna ufanisi huko wizara ya TEHAMA kuna ufanisi gani, mbona ICT Comission inawafia? Kwanini eGA ilihamishiwa ikulu miezi mitatu iliyopita?

Msichokijua ni kuwa kabla ya Bunge la Bajeti, waziri wa TEHAMA aliwapanga wabunge hapo chini ili watie petroli suala hili.

Kingu anasikika akitaka iletwe Sheria eGA waache kutengeneza mifumo, KWELI? Mnajua nani wanataka atengeneze? Tayari kuna makampuni yao ambayo wameya-position kuchukua tender za mifumo ya Serikali. Sio makampuni ya kitanzania kama mnavyodhani, ni makampuni ya nje yaje yasimike mifumo ya mailing system , e-office yenye nyaraka za Siri za Serikali na mifumo ya malipo (GePG) wanakwenda kuwa phased out, control number inaenda kuuawa na kampuni ya kigeni wanaileta.

Watu wana macho ya nyama sana, hawayaoni haya! Jaribuni kuwaza kwanini baada ya kusema wanahamisha eGA tayari wanaanza kupeleka mabadiriko ya sheria ya kuzuia eGA kutengeneza mifumo? Wanafanya haya kwa ajili ya nani? Wanasiasa wanataka pesa za damu wakamalize Uchaguzi wao. Wanafanya hayo kwa kuua ndoto za vijana wa kitanzania!

Reference ziko hapa muone jambo hili lilianza zamani sana. Gusa hapa - Tetesi: - Wanasiasa na mipango ovu ya kuiua E-GA

USALAMA WA TAIFA WAPO KWELI? Inakuwaje whistleblower anatoa taarifa ya hatari namna hii juu ya genge la watu serikalini kuua taasisi systematically over a year ago (May 2023), Idara haifanyii kazi mpaka watu hawa waovu wanafanikisha mipango yao?
Ingekuwa taarifa ya Lissu au Mbowe kutishia kuhujumu nchi mngekuwa kimya? Inakuwaje watu wachache wanaamua kuua taasisi nzima ili wabinafsishe kazi za mifumo zenye nyaraka za siri za nchi na ninyi mpo? Ni kweli bado mko kwenye nyakati za giza bado ? Hamna wataalamu wa TEHAMA wa kujua mambo haya?

NI AIBU KUBWA SANA, mkutano wa kwanza ulifanyika Wizara ya Fedha na Mipango wakati huo hata Nape hajawa Waziri, script nzima mliandikiwa mmeshindwa nini?

Nawasilisha nikiwa naumia sana kwakuwa watu wanadanganywa na wanaua taasisi yenye ubunifu, kama sio kuhujumu nchi hiki ni nini?



 
Although ega was supposed kuwa chini ya hii wizara, jpm hakuwaamini akaiweka ofis ya rais kama protection ila sasa sijui itakuwaje mbeleni
JPM alishtuka sana , wahuni wame overtake sasa imagine eGA inamwenda kuzuiwa kufanya development na kazi hizo wanapewa wakandarasi wa nje
 
JPM alishtuka sana , wahuni wame overtake sasa imagine eGA inamwenda kuzuiwa kufanya development na kazi hizo wanapewa wakandarasi wa nje
Kwani eGA ninini walikuwa wana uwezo nacho? Yaani toka waanzishwe waliweza kubuni na kutengeneza nini?
 
eGa ni Taasisi muhimu sana katika Nchi yetu, eGa inaisaidia sana Nchii hii kwenye suala la Makusanyo ya Mapato ya Serikalii.

Kuna mifumo miwili, hii mifumo imekizi Kimataifa, Kuna MAJIIS na Kuna ERMS hii mifumo ni Balaa, kuna Jamaa Mmoja anaitwa DEWAT yupo pale eGa, huyu Jamaa ni kiumbe kingine kwenye Coding...

eGa do mkombozi wa Taifa hii kwenye Upande wa Ki digitali. Tunahitaji wataalam kama watu wa eGa ili nchi yetu isonge mbele.
 
Ndio tatizo za shit-hole countries, wanaleta siasa kwenye kila kitu.

Ila kwa sayansi ya siasa ya bongo eGA kuhujumiwa ilikua suala la muda tu.
 
Ndio tatizo za shit-hole countries, wanaleta siasa kwenye kila kitu.

Ila kwa sayansi ya siasa ya bongo eGA kuhujumiwa ilikua suala la muda tu.
Mm sioni shida, haya mambo bora yabaki sekta binafsi.

Serikali kama imeshindwa tu kumanage TANESCO wataweza kusimamia Taasisi inayotengeneza mifumo endeshi yote?

Ww angalia tu TTCL walivoshindwa.

Mm naunga hii eGA ife tu sekta binafsi zipewe contracts zifanye kazi. Hata USA wanatoa Tenda kwa makampuni mengine kwa issue kama hizo, sembuse TZ?
 
Au unataja eGA iendelee muendelee kupeana kazi kwa kujuana. Waiue tu, haina faida kwa maslahi mapana ya nchi na kiuchumi
 
Leo hii tuna control number, bila eGa control number isigekuwepo.

Control number imesaidia sanaaaaa, makusanyo yalikuwa yanaishia matumboni mwa watu ambao si wazalendo wa nchi yao.

Nchi yetu itoe sheria ya lanzima, ERMS itumike kwenye taasisi zote za KIHASIBU nchi Nzima.

Naamini serikali iki u trust mfumo wa ERMS tutaendelea sana, na serikali itakusanya mapato yake ipasavyo.
 
Mm sioni shida, haya mambo bora yabaki sekta binafsi.

Serikali kama imeshindwa tu kumanage TANESCO wataweza kusimamia Taasisi inayotengeneza mifumo endeshi yote?

Ww angalia tu TTCL walivoshindwa.

Mm naunga hii eGA ife tu sekta binafsi zipewe contracts zifanye kazi. Hata USA wanatoa Tenda kwa makampuni mengine kwa issue kama hizo, sembuse TZ?
Uko sahihi mkuu. Lakini wakati eGA inapewa meno kutoka kuwa Agency na kuwa Authority, ni serikali hii hii ndiyo ilituamininisha katika hilo. Kuna kitu hakiko sawa kwa hawa viongozi wa CCM. Sidhani kama hata hili Taifa lina dira.
 
eGa wanaenda watu professional mzee, mtu ambae ni incompetence hawezi ku develop mfumo kama ERMS na MAJIIS, kama ulishawahi kutumia hii mifumo utanielewa Mkuu.
Wangekua wanaenda professionals serikalini basi issue ya mtandao iliotokea nyuma hapa isingechukua siku 3 kusolve wakati somalia wamesolve kwa siku 1.

Acha kuongea siasa, serikalini mnapeana kazi kwa kujuana na wengi hawajui wanachofanya, wamejazana wazee tu huko hawaelewi dunia inaendaje kwa sasa.

eGA was not even supposed to exist, ndo maana itakufa natural death
 
Uko sahihi mkuu. Lakini wakati eGA inapewa meno kutoka kuwa Agency na kuwa Authority, ni serikali hii hii ndiyo ilituamininisha katika hilo. Kuna kitu hakiko sawa kwa hawa viongozi wa CCM. Sidhani kama hata hili Taifa lina dira.
Makosa yalifanyika awali kwenye kuitengeneza na kuipa mamlaka, Na ndo maana nasema eGA was not even supposed to exist. So itapapaswa papaswa na mwisho itakufa tu.

Watangaze tenda kampuni zifanyiwe vetting zipige kazi. Mbona Microsoft anasimamia mifumo ya White House, TZ ina siri gn zinazoizidi white house?
 
Kwani eGA ninini walikuwa wana uwezo nacho? Yaani toka waanzishwe waliweza kubuni na kutengeneza nini?
eGa ina mifumo bora kabisa na ya kisasa, can imagine mfumo wa MAJIIS unahudumia mamlaka za maji za nchi hii, kuna mamlaka zina wateja zaidi ya laki tano Ie. DAWASA, kuna mamlaka zina wateja zaidi ya laki na ushehee ARUSHA WSSA, MWANZA WSSA, IRINGA WSSA, DUWASA WSSA, MBEYA WSSA, TANGA WSSA, na mfumo una stahimili kikamilifu ku handles those big Data, eGa ibaki vile vile nchi yetu isoge mbele.

Nchii hii na sisi wazapendo wa nchii tunaihitajii sana eGa.
 
Back
Top Bottom