Egg chops

Egg chops

Hahahaha...ni kweli kabisa....nilipata ugen wa ghafla mida kama sa tisa alasiri na mlo wa mchana ulishakwisha nikaona msosi wa haraka hapa ni tambi/spagett na mayai...

Sasa hiyo mboga mayai.....siunajua ile haraka ee,kitunguu kikaungua...nikabadili fasta...ile namalizia kukausha tambi zangu et wageni wakaaga wanaondoka wamepata sim ya dharula...nilihisi kupasukaaa

Lol...pole. yaani ni km vile kusudi ukiwa unatakA kiyu kitoke vizuri ndo mchafukoo
 
Umenichekesha bibie mie bajia kila nikizidumbukiza kwenye mafuta zinatawanyika..nimeachana nazo kwanza..

Oooh pole jamani...jaribu tena na tena....ule mchanganyiko wa uji wa dengu unatakiwa uwe mzitoo
Ukiwa mwepesi lazima ziachane
 
farkhina mie naomba unielekeze zile eggchop za mayaivna nyama ya kusaga.
 
Mahitaji

1)Mayai yaliochemshwa (kata pande 2 kila yai)
2)Viazi
3)Mayai mabichi
4)Garam massala
5)Pilipili manga
6)Pilipili ya kuwasha
7)Limao au ndimu
8)Bread crumbs au unga wa ngano
9)Chumvi kiasi
10)Mafuta ya kupikia

Namna ya kutaarisha

1)Chemsha viazi hadi kuwiva then bonda bonda hadi iwe laini

2)Add chumvi,garam masala,pilipili na ndimu...changanya vizuri

3)Then tengeza duara kwa hivo viazi then weka kipande cha yai kati...weka pembeni

4)Pakaa unga hizo round za viazi na mayai....
5)Weka mafuta katika karai jikoni yapate moto

6)Vunja mayai then yachanganye vizuri....then chukua hizo round tia kwenye mayai hakikisha mayai yanaenea vizuri

7)Dumbukiza katika karai na kaanga hadi ziwe brown

8)Egg chops tayari kwa kuliwa

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

as ussually ur the best ila hujaonyesha wapi unatumia bread crumbs au ngano mama??
 
as ussually ur the best ila hujaonyesha wapi unatumia bread crumbs au ngano mama??

Step number 4 nimeonesha amu...hivi ulikua wapi shosti

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Step number 4 nimeonesha amu...hivi ulikua wapi shosti

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

ooops ilikuwa usingizi huwezi amini sikuona ndo naona shosti nipo huku Mexico
 
Last edited by a moderator:
Fakhrina. asante kwa maekezo yako mazuri wakati wote. ila nina swali hapo kwenye mahitaji kuna hitaji la mayai na yakatwe sehemu mbili. Na hapo kwenye matayarisho umesema viazi vitengezwe shimo... na kipande cha yai kiwekwe hapo..halafu ifanyike duara! swali langu je hili yai kipande halitachanguka? swali linaendelea baada ya jibu.....
 
No unanya ile yai kulitengezea kama nyumba yaani liwe katikati kwa mkunguka wa viazi...

Yai kama yai unaliziba lisionekana kwa viazi hope umenielewa

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom