Egypt vs Tanzania Nov 5, 2009

Egypt vs Tanzania Nov 5, 2009

Jamaa hawawezi hata kupiga pass tatu....Maximo should go!
 
Hawa wajinga watatufunga 10 leo, aibu sana. Mwezi ujao ranking za fifa tutakuwa zaidi ya 100.
 
Aibu tupu wacha nikafanye kitu cha maana! Keep us updated
 
Duh, sikujua kumbe sisi wachovu namna hiii...lo
 
Ngoja niendelee na mambo yangu, hamna kitu hapa. Tutajuuuta kujifanya tunajua mpira.
 
Yaani kila dk 10 tunafungwa goli moja,kama Mechi ni dk 90 basi itakuwa hatari!
 
Tuweke mpira kwapani, kipindi cha pili tusiingize timu
 
halafu watu wanapiga kelele tunataka timu ngumu, hamna kitu humo...... wabongo ni kupiga kelele hukuhuku east afrika, siku tukiwabaatisha wenzetu kenya, uganda nk
 
We need Kaseja.....
Hata Kaseja nae angefungwa tu coz game halichezwi na kipa pekee, pia kama wachezaji ndani mnaharibu haiwezekani kipa kuokoa michomo yote, so generally timu ni mbovu!
 
Jamani kwani mpira lazima tushinde???,kuna kufungwa,kushinda ama kutoka sare,kimsingi tumeipeleka timu Cairo kajili ya kupata uzoefu tu na si kushinda.Hawa jamaa wa Misri ni wazuri sana,si mliona mpira waliouonesha kwenye Confederation Cup..Hata hivyo tusubiri dakika 90 wakuu maana kwenye Soka lolote laweza tokea(kama walivofanya Man Utd juzi).Tuwache vijana wapate uzoefu(hata wakitufunga magoli mengi kiasi gani ni mpira tu)
 
We need Kaseja.....

Kaseja wa nini tena???,hata angekuwa Kaseja bob kichapo hakikwepeki,tena usikute huyo Kaseja wako angeshachapwa 6 time hii.Waacheni Taifa Stars wapate uzoefu kutoka kwa The Pharaos,mabingwa wa Afrika
 
Back
Top Bottom