El Merreikh yatoa dau kwa Manula

El Merreikh yatoa dau kwa Manula

Vilabu vya bongo acheni choyo mwacheni Manula akale maisha hapo Simba mnamlipa kiasi gani
Simba analipwa mil7 kwa mwezi mimi namshauri manula asiache hiyo offa
Ila kama simba wanaweza kumpa 15m anaweza kubaki kwa sababu nyunbani ni nyumbani
 
Klabu ya El Merreikh ya Sudan inadaiwa kuwa inataka kumsajili golikipa wa Simba Aishi Manula ,25, kwa dola 100,000 (Tsh milioni 231) na mshahara wa dola 8000 (Tsh milioni 18.5) kwa mwezi."

View attachment 1737958
Si mara ya Kwanza Simba kutoa golikipa kwenda kucheza mpira wa kulipwa alianza Mzee Idd Pazi tena Sudan huko huko huyu km sikosei alienda Al Hilal ndio maana wametengeneza urafika nao naona safari hii mahasimu wenzao anatoka Manula

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Daah! Kwahiyo Manula ana miaka 25!?..mbona miaka yangu mimi inaenda haraka sana, au nawahi kuamka kabla ya wenzangu
Mkuu kwenye swala la umri Kwa wachezaji wa Tanzania waga Tia maji Tia maji Sana Ila Kwa Manura ni sahihi, umri wa manula ni sahihi na historia yake tangu anaenda Azam inajulikana, alichukuliwa na Azam alipomaliza Tu kidato cha nne
 
Maisha anayokula pale simba hakuna sehemu nyingine ndani ya africa atayapata

Hata wachezaji wote wa yanga ndoto yao kubwa ni kucheza kwa kiwango kizuri ili siku moja waje wasajiliwe simba
Wanautani hao Manula thamani yake ni kubwa mno sio wa kumgombea kwa dau hilo. Ni goal keeper ambaye hata kukiwa na wachezaji watatu uwanjani bado yale mashaka ya kufungwa huyapati.

Kwa bei hiyo labda waongee na yanga wanaweza kupata wachezaji hata wanne (ila wote wabovu)

Tumekuwa tukisumbuliwa sana siku hizi za karibuni kwa clubs kubwa za kimataifa kutaka kununua wachezaji wetu.

Mfano juzi hapo Arsernal nao wametuma maombi yao kwa dau la 1B, uongozi wa simba uliwaambia tulieni kwanza tukimaliza msiba tutalifikiria ombi lenu
Kama kiwango cha Manula hakiendani na hio ofa basi yapaswa Simba kumlipa zaidi ya hiyo pesa. Kuishia kuongea hivyo halafu Manula kupokea mshahara wa chini ya milioni 15 ndani ya Simba basi itakuwa ni swala la ajabu. Mpira ni ajira
 
Maisha anayokula pale simba hakuna sehemu nyingine ndani ya africa atayapata

Hata wachezaji wote wa yanga ndoto yao kubwa ni kucheza kwa kiwango kizuri ili siku moja waje wasajiliwe simba
Mfano ni Morrison
 
Mil 18 gharama za maisha zikoje ukizingatia ni ugenini....
Ningekuwa mimi ningebaki simba nikiwaomba waniongezee mshahara kutoka saba mpaka 10
Haujui kama safari moja huanzisha nyingine? ngoja akae hapa aje afungwe kwa bahati mbaya mechi ya watani wa jadi atuhumiwe kahujumu team akae bench safari iishie hapo
 
Wanautani hao Manula thamani yake ni kubwa mno sio wa kumgombea kwa dau hilo. Ni goal keeper ambaye hata kukiwa na wachezaji watatu uwanjani bado yale mashaka ya kufungwa huyapati.

Kwa bei hiyo labda waongee na yanga wanaweza kupata wachezaji hata wanne (ila wote wabovu)

Tumekuwa tukisumbuliwa sana siku hizi za karibuni kwa clubs kubwa za kimataifa kutaka kununua wachezaji wetu.

Mfano juzi hapo Arsernal nao wametuma maombi yao kwa dau la 1B, uongozi wa simba uliwaambia tulieni kwanza tukimaliza msiba tutalifikiria ombi lenu
Hahahahahaa
 
Ndogo sana hio kwa manula.

Hio inatakiwa iwe pesa ya Wiki moja
Ndivyo anavyolipwa hapa Tz kwa wiki?. Ukisema ndogo,sema ndogo kwa ipi? Hiyo ni ndogo milioni 18 na point kwa anayopata sasa?. Acheni kudanganya,akaacha hiyo pesa kwa kusema ndogo halafu bado akaishia kwenye hii hii ya madafu milioni 1 anayolipwa sasa
 
Kwani kaiacha?
Hii ni tetesi mkuu.
Simba wapo tayari kuuza mchezaji yoyote dau likija.

Hayo ni maisha ya watu mkuu

Relax.
 
Ndivyo anavyolipwa hapa Tz kwa wiki?. Ukisema ndogo,sema ndogo kwa ipi? Hiyo ni ndogo milioni 18 na point kwa anayopata sasa?. Acheni kudanganya,akaacha hiyo pesa kwa kusema ndogo halafu bado akaishia kwenye hii hii ya madafu milioni 1 anayolipwa sasa
Mishahara ya million moja uko simba Queen's huko
 
Mshahara mdogo sana.. labda kama hiyo 18 ni baada ya makato yote na haihusiani na living coast and transport.
Klabu ya El Merreikh ya Sudan inadaiwa kuwa inataka kumsajili golikipa wa Simba Aishi Manula ,25, kwa dola 100,000 (Tsh milioni 231) na mshahara wa dola 8000 (Tsh milioni 18.5) kwa mwezi."

View attachment 1737958
 
Mkuu kwenye swala la umri Kwa wachezaji wa Tanzania waga Tia maji Tia maji Sana Ila Kwa Manura ni sahihi, umri wa manula ni sahihi na historia yake tangu anaenda Azam inajulikana, alichukuliwa na Azam alipomaliza Tu kidato cha nne
Mkubwa yule
 
Mfano ni Morrison
Kama hivi
IMG-20210202-WA0005.jpg
 
Back
Top Bottom