Mzee elinino ilikuwa 98, na sio 97...97 ilikuwa ni vuli ya kawaida tu..
na nina historia mbaya sana kuhusu elinino na ndo ilikuwa nimetoka kuoa Tu mzee wangu mwaka 98, baba angu mkwe alifariki kwenye ajali ya basi na chanzo kikiwa ni elnino nina matukio Zaidi ya 10 nikikumbuka elnino huwa nasema Mungu inawezekana yupo...
Ntakupa experience ya baba mkwe...
Alikuwa akitoka Tanga kuja Dar kunisalimia!
Kapanda basi la kampuni ya No Challenge aina ya Isuzu yenye namba za usajili TZK 960,
basi lilikuwa limeondoka Tanga saa 11:00 lilifika eneo la mto Msangazi maeneo ya muheza huko saa 11:45 jioni.
Ndipo lilipopata Ajali kutokana kuwa na mvua kubwa na elnino walikuwepo watu 75 kati ya hao walionusurika watu watatu tu"
mzee naijua elnino vizuri sana kuliko hata mwanangu..
nakumbuka Nyumba zilivyokuwa zinaharibika nikikumbuka ni kama napata flash lights za matukio ya elnino..
halafu mpuuzi mmoja anafananisha elnino na Hivi vinyunvyu...