Ili kumpata tena Mkjj inabidi nasi tumnunue,
Steve sisi hatuna haja ya kumnunua MKJJ kwa sababu, MKJJ hana picha zetu, lakini sisi tunapicha zake na za hao rafiki zake, kwa hiyo yeye na wenzie wanatakiwa kutununua
Wana JF,
Kama ni meli basi naona mwamba huo hapo mbele, tunaelekea kuugonga. Damn!, nikiwa kama abiria ninasikitishwa sana na vitendo vya hawa watu:
1. Mwanakijiji, attention grabber, Mwanakijiji amekuwa akitafuta umaarufu usio na maana. EL anayo hiyo sifa ya kununua waandishi (sijui km ni kweli) baada ya Mwanakijiji kusikia hayo akaanza kumwandika EL kwa ubaya hata pale aliposema mazuri, kwake yeye EL hafai hafai hafai tuuuu!. Wakati watu wana turn liabilities into assets yeye akawa anaturn assets za Lowassa into liabilities. Alifanya haya akitegemea KUNUNULIWA. PM ni smart wala hajajali, wapambe huku chini ndio wanahangaika na Mwanakijiji, maskini wangejua wala wasingehangaika. Njaa mbaya sana!
2. Hasara, Mzee wa Ar huyu naona amekuwa TOTAL LOSS. Kitendo cha kuanzisha topic ya udaku humu sio cha busara. Kusambaza picha tu (FEKI) hakikuwa jambo la busara, sijui ni nini jamani, Kaka mbona ushakula dili nyingi tu hapo IKULU hataka kama ni ndogo ndogo lakini si mkono ulienda kinywani? sasa yote haya ni nini tena?!
Ninaamini lengo kuu la Mwanakijiji ni kuiua hii forum, sijui kwanini naamini, lakini labda ni kwa sababu ileile iliyomfanya aamue kujiunga na CCM!
Kaeni MACHO si kila king'aacho ni ALMASI.
mwanakijiji kama ni kweli wameleta pesa kula
Money ruls the world bwana, kama ni kumnunua Mkjj wanaweza kabisa kununua. Kwani nani alijuia akina Hiza Tambwe, Dr Kaburu, Ngawaiya etc wangenunuliwa. Watu hapa wanasema mwanakijiji anataka kurudishwa kundini, kundini lipi? Mwanakijiji mwenyewe hajawahi kuwa kwenye kundi labda kundi la nyuma ya screen ya computer sasa atarudishwa kwenye kundi gani? No one knows mwanakijiji, anonymos man ambaye amejifungia kwenye kachumba na komputer moja na ka microfone. hamna amjuae bwana kama nipicha watu tulizisave watanunua wangapi kwaajili ya picha? wao si ajabu wana muona mwana kijiji ni kichaa fulani aliyejikatia tamaa kabisa sasa kwa woga anapiga kelele huku kajificha nyuma ya komputer kama Kambwa kanakokimblia nyuma ya nyumba na kubweka.
lakini akili kichwani..."revolutionaries has no price taga..."..hivi kweli mtu mwenye akili anaweza kununuliwa ...
Mkubwa kwani nani kakuambia mwanakijiji anakili? angekuwa na akili asingeweka zile picha hapa na kuzitoa kwa sababu watu wamepiga kelele weka!weka! weka wengine wakampa sifa eti thats why I love this badboy Mkjj! naye sivyokuwa na akili akaweka. watu wakapiga kelele toa!toa!toa, akatoa.
kwani bei ya mtu ni shilingi ngapi....wanaotaka kumununua au waliomnunua wanapoteza pesa yao kwa kuwa zimewazidi.....
Mbona mwanakijiji ni price less mzee kama sio vry cheap? Hivi kweli mwanakijiji akipewa kazi nzuri sasa hivi akiambiwa mwanakijiji unaenda China kuwa balozi wetu unafikiria atakataa? wewe unafikiri mwanakijiji mwenyewe anapenda kujificha kwenye komputa usiku na mchana kila siku hadi kaandika post zaidi ya 5000? Naapa mwanakijiji wakiamua kumnunua wala haitagharibu kitu ila atakuwa tuu kasaliti.
Rwabugiri, hayo ndiyo mawazo niliyoamka nayo leo.. sijui yataishia wapi lakini nimeamka nikiwa na hisia ya kukata tamaa, na hisia ya kuchoshwa na kujaribu kufikiri mkakati mwingine. Mkakati nilioamka nao leo ni wa kujiunga nao siyo wa mimi kubadilika.
Mwanakijiji mwenyewe huko anakobeba mabox kashakata tamaa watu bado mnamuona shujaa wa wenu. anawadanganya anataka kujiunga nao na si yeye kubadilia nana kawadanganya. wewe ukishajiunga na mafisadi nawe unakuwa fisadi mkuu wala usijidanganye eti naenda kuganga njaa.
kwanini unafikiri naitwa na Sisiemu, nimechagua mwenyewe baada ya kufikiri kwa makini. CCM ndiyo chama pekee kinachoweza kuingoza Tanzania na it is about time to recognize that na kujiunga na watawalao. Wakati mwingine inabidi mtu ucheze ngoma wanayopiga wengine hata kwa kutingisha mguu tu
Unajua mara nyingi mtu ayasemayo ndio yako kichwani mwake. Mwanakijiji si cheap nawaambia. Mwanakijiji hongera sana ku kuamua kutumua uhuru wako kujiunga na CCM chama unachokiona kinakufaa. Mimi sitaki kusema unarudi kundini kwani najua hujawahi kuwa kundini. Naona umeamua kwenda kucheza ngoma ya ufisadi na najua wakigundua kipaji chako cha ulaghai wanaweza kukushirikisha kwenye ulaji wa Kasungura.
Hasara pole sana kwa kulia lia mwenzako kakuzidi ujanja.
watu watamlamba miguu humu ndani ! na mbaya zaidi anasema kwamba yeye ni disabled ili kuficha ID yake, lakini ni mbaya sana kwake kukaa siku zote hizo akiamini hakuna anayemjua !
watu wakichoka siku, watamtolea uvivu laivu !
just waiting for the day !
Huyu mtu saa nyingine ananishangaza kweli kama anavyojishangaza yeye mwenyewe na kucheka bila sababu !
Duh!
Hivi naomba kuwauliza WATU.
Huwa tunasoma thread toka mwanzo hadi mwisho ndio tuachangia/kujibu au tunakurupuka tu na kuandika tuliyoyaota usiku wa jana?!?
Angalia usije na wewe ukapewa masaa 24 kulitaja hadharani jina lake kama ilivyokuwa kwa Dokta Hu/ Game Theory. Halafu ukimchefua zaidi atakupa hadi anwani yake ya nyumbani anakoishi...kama alivyowahi kufanya huko nyuma(of course ilikuwa dead end)
Kada,
Its too baaaaad! mtu kufikiri hujulikani, mbaya mbaya tena sana. banking transactions tu zinaweza kufanya uwe traced kiulaini hasa nyie wa nje ya nchi........
Sheria ya hapa hainiruhusu kutaja watu, wala sio nia yangu kwa sababu LIKE THIS TOPIC haisaidii wananachi wa Vijijini, ni UPUUUZI MTUPU kama hii topic hapa.
KWELI KUNA MTU WA KUTAKA KUMNUNUA MWANDISHI WA INTERNET INAYOSOMWA NA 0.0000...% YA WAPIGA KURA?
If any....
That guy must be the dumbest guy in this planet!
mwanakijiji(na wanaJF woote) kuna ujumbe wako hapa chini FROM ZITTO kabwe !!
Wana JF,
Nilizungumza na mwandishi wa MwanaHalisi na kumweleza ya kwamba siamini kama ajali ile ilipangwa. Ninaamini ni ajali kama ajali nyingine tu. Kuendekeza habari hizi ni hatari sana kwa utulivu wa nchi. Nilimwambia hivyo mwandishi. Ajali ikitokea na nikapoteza maisha, ni mipango ya mungu. Wala sitembei nikiogopa kuwa nitauwawa. Siogopi hata kidogo.
Ni kweli nilipigiwa simu na naibu waziri. Lakini haihusiani hata kidogo na ajali. Mimi kama kiongozi ninawasiliana na viongozi mbalimbali. Sasa kama kiongozi akinipigia simu halafu ikatokea ajali na nikasema yeye ndio kapanga, basi sitakuwa ninawasiliana na viongozi.
MwanaHalisi limekwenda out of the way. Na nimewasialiana na Mhariri wake juu ya hili.
(sasa nataka uje uthibitishe uliyosema wewe mwanakijiji na timu yako nzima ya SMEARING CAMPAIGN)