Nguvu sawa inahusiana vipi hapa ? Swali ni, kwa nini elektroni hazivutwi zikadumbukia kwenye kiini cha uchanya ? Hatuongelei kipimo cha hizo nguvu hapa!!! Absolutely irrelevant.
Wrong!
Nguvu inayotokana na chaji haitegemei tungamo!!!
Sikia Mutu. Coulombic force between chaji q1 na q2 is
F =
k (q1 X q2 )
distance squared,
Hakuna mass hapo!!!
Listen, Mutu, nataka kukwambia kitu super, super important:
Kutokana na udogo wa chembe hizi (proton, electron, kwaksi, sijui leptoni na hata atom yenyewe, kutokana na udogo huo, huwa nguvu zinazoendana au kukinzwa na tungamo ni ndogo ndogo mno kulinganisha na nguvu zinazoendana na chaji, kiasi huwa haziongelewi, yani hizi zinazotokana au kukinzwa na tungamo huwa zipo kama hazipo (negligible).
Kwa hiyo vitu kama proton au electron tungamo lake haliwezi kuwa na effect ya maana kulinganisha na nguvu ya chaji zao. Hivyo basi, sikia hapa Mutu, hivyo basi kule kuvutana kwa chembe zooote hizi kunakotokana na chaji huwa hakuzuiwi na hakutegemeani na ukubwa wa vinavyovutana! Always remember that. Mandatory in the story!
Tunajua zinavutana. Swali ni, kwa nini hazivutwi zikadumbukia kwenye kiini cha uchanya ?
Mutu unarudia lile kosa hapa, una consider mchango wa tungamo katika kuvutana kwa nguvu zinazotokana na chaji. Soma juu hapo: tungamano la elementary particle lina negligible effect katika hizi electrostatic forces. Kumbuka hilo siku zote.
Nimesema, na narudia, swali ni kwa nini hazivutwi na kudumbukia kwenye kiini kilichojaa uchanya ?
Unaona sasa, Mutu, unachanganya force of gravity na Coulombic force of electrostatic attraction and repulsion. Halafu unanambia mimi ndio nikafanye homework ! Homework ya basic definition ya coulombic force na gravity kweli ?
Sikia Mutu:
Force of gravity F:
F =
G (mass 1 X mass 2 )
distance squared,
where G = constant isiyohusiana na chaji!!
Halafu Coulombic force of electrostatic attraction/repulsion
F =
k (charge 1 X charge 2 )
distance squared,
where k = constant inayohusiana na medium, hakuna tungamo hapo!
Sasa katika ulimwengu wa elementary particles, hiyo force of gravity ni negligible kulinganisha na Coulombic force! Yani ukiwa na chembe mbili zenye tungamo na chaji, nguvu za aina zote mbili zitakuwepo lakini kipimo cha ile nguvu ya chaji itaazidi sana ya tungamo kiasi cha kuwa ipo kama haipo!!
Tunarudi tulipoanzia: Kama elektroni zinavutwa, ni kwa nini hazidumbukii kwenye kiini cha uchanya ?