Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Kombe la dunia ndio habari inayotamba kwa sasa. Mataifa 32 yenye ubora wa viwango vya soka yanachuana mpaka zinabaki timu mbili halafu zinagombea kombe siku ya fainali. Mpira ni mchezo wenye kupendwa kuliko michezo mingine yoyote ile.
Hawa tunaowaona wamejaa majukwaani na matarumbeta yao wakiwa wamevaa fulana za timu zao za mataifa walianza kuweka katika akaunti maalum pesa wanazotumia sasa, ndani ya kipindi cha miaka minne iliyopita tangu michuano ya mwisho iliyofanyika Russia ilipomalizika.
Pesa zote wanazolipa kwa ajili ya malazi, makazi na ulevi wa hapa na pale ni matokeo ya kuweka akiba (savings) kwa miaka minne mfululizo. Wakipata mshahara wanatenga fungu maalum kwa ajili ya safari ya Qatar ya 2022 Novemba.
Kwa huu mgao wa umeme unaomlazimu mlaji kutumia shilingi karibu elfu ishirini na tano kila siku kwa ajili tu ya mafuta ya generator ni uharibifu wa moja kwa moja wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na ule wa kitaifa kwa ujumla.
Nani anayeweza kuweka akiba pesa kama zinakwenda kununulia mafuta ya jenereta?. Nani anayeweza hata kuwazia tu kuweka akiba kwa hali hii ya uhaba wa nishati?. Hata ule utalii wa ndani hakuna anayeweza kuufanya kama kwa siku moja mtu anatumia zaidi ya elfu ishirini kwa mafuta tu!.
Tunapewa majibu ya kisiasa, anayeyatoa unamuona kabisa yupo katika wakati mgumu wa kujibu maswali anayoulizwa. Serikali inaposema hali ya umeme itakuwa nzuri mwaka 2025 ina maana haya mambo ya kununua mafuta ya jenereta yatakwenda mpaka mwaka huo?.
Nadhani tatizo ni kuchukuliana sana poa, kwamba hawa watanuna kwa muda mfupi tu na kesho watakuwa wamekwisha kusahau. Kwamba ni watu wapole wapenda amani na wengi wetu tunaposikia maneno haya tunakuwa wapole kweli.
Sababu za ukosefu wa nishati ya umeme na ziwe za kweli. Lakini kama ni siasa zenye malengo ya kuficha ufisadi, nasikitika kusema wote wanaofanya haya mambo wamejichumia laana mbaya sana na hiyo laana wanaisambaza kwa wengine hata wasiohusika.