Elibariki Kingu: Wabunge wa CCM tuko vizuri kichwani, tusingezeweza kupitisha mkataba usio na maslahi kwa nchi yetu

hivi ni mkataba au makubaliano?.

GPA ya juu kutoka UDIZIM, CBE, IFM na MZUMBE... hahahaha.

Tatizo ni CCM.
 
Katika wabunge wa CCM wenye uelewa mdogo sana au akili kidogo sana, mmoja wapo ni Elibariki Kingu
 
Ni lini uliwahi kumsikia punguani akisema kuwa mimi mwenzenu sina akili ya kutosha? Tena wendawazimu huwa wanajiona wana akili kuliko walio wazima.
 
"Wabunge wa CCM tuliopitisha Mkataba wa Uwekezaji Bandarini tuko vizuri kichwani,pale Bungeni kuna wabunge wa CCM wako vizuri kichwani,mimi mwenyewe nimemaliza chuo mzumbe wakaning'ang'ania nibaki kufundisha pale kwa sababu nina akili nyingi, nilipata GPA ya juu sana, kwa hiyo hatukupitisha mkataba bila kuusoma, na tusingezeweza kupitisha mkataba usio na maslahi kwa nchi yetu" Mbunge wa jimbo Singida Magharibi"




Toa Maoni yako
 
Muulizeni na G.P.A yake zake alijua lini Mkataba ushapigwa sahini? Je alijua mkataba huo ulishachelewa kufikishwa Bungeni kuridhiwa...je anajua kuwa hata hapo(ucheleweshaji wa ridhaa ya chombo kikuu cha sheria) madhara yake ni tungeshapelekwa- kupelekwa mahakamani, kama wangeamua hivyo?

Je anajua ni baada ya Whistle blower ndio CCM nayo imekurupuka kusema ati Uwekezaji huo(wa mjomba) uko sambamba na Ilani ya CCM....mbona hatukumsikia hata Mbunge mmoja kusema hayo pale Bungeni....karaa

Muwekeni huyu mbunge kwenye ile listi ya wabunge wa kutupisha 2025
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…