Tetesi: Elie Mpanzu kutua Yanga kabla ya Weekend hii

Vichekesho

Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
66
Reaction score
3,277
Kuna taarifa kuwa boss wa AS Vita Club amemvutia waya Engineer Hersi kumweleza kuwa mchezaji Elie Mpanzu (wabongo wananwita Elia) amerudi Congo na hajafanikiwa kusajiliwa Belgium.

Boss huyo ambaye ni askari jeshi amesema kuwa mchezaji huyo yuko tayari kuja Yanga endapo atapata nafasi na ameonesha kuvutiwa na project ya Yanga.

Inasemekana Engineer ameomba atoe majibu kesho kabla ya saa 5 asubuhi ili apate muda wa kuuliza benchi la ufundi kama kuna haja ya kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji na endapo benchi litasema kuna uhutaji basi atatua kabla ya weekend ya kesho kutwa.
 
Soma Pia:

Asante kwa taarifa
 
Nilifuatilia interview ya Hersi na salama jabir akisimulia jinsi alivyompata Mayele na jinsi alivyodiriki kusafiri na kutimba ofisi za kiongozi mkubwa wa majeshi ya DRC anayeogopeka General Gabriel Amisi Kumba ambaye ndiye mmiliki wa AS Vita na kufanikiwa kujenga naye urafiki na kumshawishi kumnasa Mayele kiulaini baada ya General kumueleza kwamba hata yeye ni shabiki wa Yanga! Akambariki na kumpatia Mayele na kumwambia kama kuna lolote lingine atahitaji basi amtafute!

Hivyo basi, kama huyo mchezaji anatoka As vita nashawishika kuamini Hersi akimtaka, basi hana pingamizi.
 
Back
Top Bottom