Elimu bila malipo imekufa kimyakimya

Elimu bila malipo imekufa kimyakimya

Barackobama

Member
Joined
May 20, 2021
Posts
20
Reaction score
21
Ni miezi sasa takriban mitatu. Tangu Septemba hadi Desemba 2023, Serikali haijatuma fedha za ruzuku shuleni bila maelezo yoyote jambo ambalo limezua mjadala katika utekelezaji wa ebm kwa mujibu wa waraka wa elimu kama ulivyotolewa na Serikali.

Jambo hili linapelekea Walimu viongozi kuanza kupendekeza michango mbalimbali kutoka kwa Wanafunzi na wazazi! Serikali iweke wazi utekelezaji wa mradi huj ili kutowachonganisha walimu na wazazi/wananchi huko shuleni.

=== ===== =====

Serikali haijatuingizia pesa za Elimu Bure kwenye Shule, tunatumia fedha zetu za mifukoni kuendesha Taasisi

Tuna miezi miwili Oktoba na Novemba Serikali haijaingiza pesa za Elimu Bure yaani ‘CAPITATION’ na ‘POSHO YA MADARAKA’, hivyo inaleta ugumu katika utekelezaji wa majukumu ya kishule.

Badala ya kuhudumia familia zetu tunatumia mshahara kuendeshea shule kitu ambacho sio sahihi na kinatuumiza kama Walimu pia ni aibu kwa Serikali, naomba hii ifike TAMISEMI watolee ufafanuzi au Serikali haina fedha?

===== ========

Naomba Serikali ikumbuke wajibu wake ilipe pesa za elimu bure za October na November sisi kama wakuu wa shule tunapata shida sana kutoka kwa wazabuni, kila mara tunapigiwa simu kudaiwa. Naomba serikal iwe inalipa pesa kwa wakati ili kutuondolea usumbufu huu au itoe tamko ni lini italipa kuliko kukaa kimyaa huu mwezi wa tatu unaenda bila malipo.
 
Elimu bure ifutwe, posho ya madaraka iondolewe hili ndiyo mwarobaini wa kuepukana na changamoto hii. Kuhusu maslahi ya walimu kuboreshwa huu umekuwa ni wimbo wa taifa uendelee kuimbwa!
 
Elimu bure ni mzigo kwa serikali. Hebu fikiria kuna shule ngapi za msingi na sekondari halafu kila mwezi serikali inatakiwa kutoa fedha za uendeshaji.
 
Huduma za kijamii kama elimu, afya, usalama et. ni sehemu ya majukumu ya msingi ya serikali. Ndio huduma zinazotoa uhalali wa serikali kukusanya kodi.....

Labda tuangalie gharama za kutoa elimu bure vs mapato ya serikali.....
 
Dah! Nawaonea huruma hao wafanyakazi wenu mlio waajiri kwenye hizo shule zenu za Kata, huku mkitegemea kuwalipa mishahara kwa kutumia hela za ruzuku!! Sijui wanaishije!!! Na huu msimu wa sikukuu ndiyo kabisaaa!! Ni maumivu tu.

Nyinyi Wakuu wa shule hata siwaonei huruma. Maana hizo laki 2 na laki 2 na nusu mnazopewa kila mwezi, zimewageuza tu kuwa wakuda dhidi ya walimu wenzenu.
 
Huduma za kijamii kama elimu, afya, usalama et. ni sehemu ya majukumu ya msingi ya serikali. Ndio huduma zinazotoa uhalali wa serikali kukusanya kodi.....

Labda tuangalie gharama za kutoa elimu bure vs mapato ya serikali.....
Uwezo wa serikali ni mdogo kugharamia huduma hizo labda waongeze tozo. Hata nchi zenye uchumi mkubwa kama Marekani wananchi wanalipia huduma za elimu, afya nk na kodi wanalipa tena zaidi yetu
 
Eeeeeeee mwenyezi Muuungu uliyena mamlaka hapa duniani na Mbinguni FUTILIA MBALI POSHO YA MADARAKA !!! Kuna wakuu wa shule wamenunua hivyo vyeo wakidhani ukuu wa shule ni utajiri !!! Tunakuomba fulilia MBALI hawa" kenge" wakome
 
Hii Serikali Inafanya Mambo ambayo Muda Mwingine hayaeleweki Pesa yenyewe ya Septemba Imekuja Kuingiza Mwezi wa 11 Kinyume na Utaratibu kwa Hiyo Ngoja Tuona Tunakoelekea Maana Shule ni za Kwao Sio za Wakuu wa Shule au Walimu Wakuu
 
Elimu bure ifutwe, posho ya madaraka iondolewe hili ndiyo mwarobaini wa kuepukana na changamoto hii. Kuhusu maslahi ya walimu kuboreshwa huu umekuwa ni wimbo wa taifa uendelee kuimbwa!
Hii nayo ni sababu kumbe(posho ya ..)
[emoji3482][emoji3482][emoji3482][emoji3482][emoji3482]
Walimu wanachukian sana
 
Mimi wazo langu serikali ingetia nguvu kwenye sekta ya kilmo then kwenye Elimu waache kam miak ya 1990/2005 hv

Waendeleez miundombine vitendea kaz na motisha/ maslai
 
Ni miezi sasa takriban mitatu. Tangu Septemba hadi Desemba 2023, Serikali haijatuma fedha za ruzuku shuleni bila maelezo yoyote jambo ambalo limezua mjadala katika utekelezaji wa ebm kwa mujibu wa waraka wa elimu kama ulivyotolewa na Serikali.

Jambo hili linapelekea Walimu viongozi kuanza kupendekeza michango mbalimbali kutoka kwa Wanafunzi na wazazi! Serikali iweke wazi utekelezaji wa mradi huj ili kutowachonganisha walimu na wazazi/wananchi huko shuleni.

=== ===== =====

Serikali haijatuingizia pesa za Elimu Bure kwenye Shule, tunatumia fedha zetu za mifukoni kuendesha Taasisi

Tuna miezi miwili Oktoba na Novemba Serikali haijaingiza pesa za Elimu Bure yaani ‘CAPITATION’ na ‘POSHO YA MADARAKA’, hivyo inaleta ugumu katika utekelezaji wa majukumu ya kishule.

Badala ya kuhudumia familia zetu tunatumia mshahara kuendeshea shule kitu ambacho sio sahihi na kinatuumiza kama Walimu pia ni aibu kwa Serikali, naomba hii ifike TAMISEMI watolee ufafanuzi au Serikali haina fedha?

===== ========

Naomba Serikali ikumbuke wajibu wake ilipe pesa za elimu bure za October na November sisi kama wakuu wa shule tunapata shida sana kutoka kwa wazabuni, kila mara tunapigiwa simu kudaiwa. Naomba serikal iwe inalipa pesa kwa wakati ili kutuondolea usumbufu huu au itoe tamko ni lini italipa kuliko kukaa kimyaa huu mwezi wa tatu unaenda bila malipo.
Tena ni mateso makubwa mno ambayo yamekuja muda ambao pesa ilikuwa inahitajika sana kwa ajili ya kugharamia usimamizi wa mitihani ya kitaifa kidato cha pili na cha nne. Watu imebidi wakope na wenye unafuu wametumia pesa zao za mfukoni
 
Ni miezi sasa takriban mitatu. Tangu Septemba hadi Desemba 2023, Serikali haijatuma fedha za ruzuku shuleni bila maelezo yoyote jambo ambalo limezua mjadala katika utekelezaji wa ebm kwa mujibu wa waraka wa elimu kama ulivyotolewa na Serikali.

Jambo hili linapelekea Walimu viongozi kuanza kupendekeza michango mbalimbali kutoka kwa Wanafunzi na wazazi! Serikali iweke wazi utekelezaji wa mradi huj ili kutowachonganisha walimu na wazazi/wananchi huko shuleni.

=== ===== =====

Serikali haijatuingizia pesa za Elimu Bure kwenye Shule, tunatumia fedha zetu za mifukoni kuendesha Taasisi

Tuna miezi miwili Oktoba na Novemba Serikali haijaingiza pesa za Elimu Bure yaani ‘CAPITATION’ na ‘POSHO YA MADARAKA’, hivyo inaleta ugumu katika utekelezaji wa majukumu ya kishule.

Badala ya kuhudumia familia zetu tunatumia mshahara kuendeshea shule kitu ambacho sio sahihi na kinatuumiza kama Walimu pia ni aibu kwa Serikali, naomba hii ifike TAMISEMI watolee ufafanuzi au Serikali haina fedha?

===== ========

Naomba Serikali ikumbuke wajibu wake ilipe pesa za elimu bure za October na November sisi kama wakuu wa shule tunapata shida sana kutoka kwa wazabuni, kila mara tunapigiwa simu kudaiwa. Naomba serikal iwe inalipa pesa kwa wakati ili kutuondolea usumbufu huu au itoe tamko ni lini italipa kuliko kukaa kimyaa huu mwezi wa tatu unaenda bila malipo.
Pesa hakuna hata kwenye hazina. Hali sio hali kipindi hiki.
 
The so called "elimu bure" ilishindwa hata kabla haijaanza. Wanailazimisha tu kisiasa ila kiuhalisia ni danganya toto tu. Fedha zenyewe zitolewazo hazikidhi kabisaa mahitaji ya shule, bado ipite miezi hazijatolewa.
 
Walimu wakuu ndo wamebeba mzigo huuu! Kuna watu wanazani walimu wakuu wananufaika na Elimu bule pole Yao! Fuatilieni Mjue walimu wakuu kwenye changamoto kama hizi wanafanya nini! Wasipotoa pesa za elimu bule hapa serikali Itakuwa imetumia mishahala ya walimu wakuu kuendesha shughuli za shule hasa Mitihani ya December Ambapo inajulikana huwa inaendeshwa Kwa fedha za captation.Binafsi nawapa pole walimu wakuu!!!!!!
 
Back
Top Bottom