Elimu bila malipo imekufa kimyakimya

Elimu bila malipo imekufa kimyakimya

Ni miezi sasa takriban mitatu. Tangu Septemba hadi Desemba 2023, Serikali haijatuma fedha za ruzuku shuleni bila maelezo yoyote jambo ambalo limezua mjadala katika utekelezaji wa ebm kwa mujibu wa waraka wa elimu kama ulivyotolewa na Serikali.

Jambo hili linapelekea Walimu viongozi kuanza kupendekeza michango mbalimbali kutoka kwa Wanafunzi na wazazi! Serikali iweke wazi utekelezaji wa mradi huj ili kutowachonganisha walimu na wazazi/wananchi huko shuleni.


=== ===== =====

Serikali haijatuingizia pesa za Elimu Bure kwenye Shule, tunatumia fedha zetu za mifukoni kuendesha Taasisi

Tuna miezi miwili Oktoba na Novemba Serikali haijaingiza pesa za Elimu Bure yaani ‘CAPITATION’ na ‘POSHO YA MADARAKA’, hivyo inaleta ugumu katika utekelezaji wa majukumu ya kishule.

Badala ya kuhudumia familia zetu tunatumia mshahara kuendeshea shule kitu ambacho sio sahihi na kinatuumiza kama Walimu pia ni aibu kwa Serikali, naomba hii ifike TAMISEMI watolee ufafanuzi au Serikali haina fedha?

===== ========

Naomba Serikali ikumbuke wajibu wake ilipe pesa za elimu bure za October na November sisi kama wakuu wa shule tunapata shida sana kutoka kwa wazabuni, kila mara tunapigiwa simu kudaiwa. Naomba serikal iwe inalipa pesa kwa wakati ili kutuondolea usumbufu huu au itoe tamko ni lini italipa kuliko kukaa kimyaa huu mwezi wa tatu unaenda bila malipo.
Elimu bure ni upumbavu...
 
Huduma za kijamii kama elimu, afya, usalama et. ni sehemu ya majukumu ya msingi ya serikali. Ndio huduma zinazotoa uhalali wa serikali kukusanya kodi.....

Labda tuangalie gharama za kutoa elimu bure vs mapato ya serikali.....
True halafu tuangalie na vipaumbele pia
 
Dah! Nawaonea huruma hao wafanyakazi wenu mlio waajiri kwenye hizo shule zenu za Kata, huku mkitegemea kuwalipa mishahara kwa kutumia hela za ruzuku!! Sijui wanaishije!!! Na huu msimu wa sikukuu ndiyo kabisaaa!! Ni maumivu tu.

Nyinyi Wakuu wa shule hata siwaonei huruma. Maana hizo laki 2 na laki 2 na nusu mnazopewa kila mwezi, zimewageuza tu kuwa wakuda dhidi ya walimu wenzenu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Serikali ingeliweka wazi hili swala La Elimu Bila malipo Shule Zina struggle sana Wazabuni Wanaua Mitaji kwa Kuzikopesha shule Na Serikali haijali kuhusu hili wakati wa Magu haya hayakufanyika Dk Samia Kuna Watu wanakwamisha juhudi zake na yeye hajawashtukia

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Serikali ya wahuni lazima itafeli tu kwemye inshu za kuendesha nchi
 
Back
Top Bottom