Elimu: Changamoto za utekelezaji wa kalenda ya mtaala

Kila mwanasiasa anakuja na lake.

Walimu walishaandaa mpango kazi wa MWAKA mzima kabla shule kufunguliwa January, ghafla wanaitwa wanaambiwa Kuna marekebisho, maana yake wakaanze tena kutengeneza scheme of work upya.
unajiuliza wakati wote tangu shule zilipofungwa walishindwa Nini kutoa huo mwongozo.

Nchi ngumu sana hii
 
Tufanye nin sasa?? Kama tatizo tushaliona
 
Ila huu mpango umeonesha kufeli mapema sana
 
Kazi mnayo... Mnalazimishwa kufanya the imposible kua posible...
 
Katika kumoderate kazi ya ufundishaji na kuweka usawa kwa nchi nzima kalenda iko sahihi,changamoto ni kutokuwa na;

1. Muda wa mazoezi na majaribio

2. Muda wa kufanya marudio na masahihisho

3. Kuchelewa kwa umaliziaji wa mada, mfano, kidato cha NNE,kalenda inakutaka ufundishe hadi wiki moja au mbili kabla ya mtihani wa taifa,..huyu mwanafunzi kitu alichofundishwa wiki moja kabla atakisoma,kukifanyia mazoezi na kukirudia rudia ili kikae kichwani SAA ngapi?

4.Room ya kufidia magap kama mwalimu atapata dharura yoyote,means mwalimu anatakiwa kuwepo shule siku zote bila kujali ataumwa,atafiwa,atapata kazi maalum

Naungana na mdau aliesema ifanyiwe majaribio kidato cha kwanza tu kwa sekondari,vingnevyo walimu na wazazi wasipojiongeza mwaka huu matokeo yatakua mabaya.
 
Umeongea madini sana mkuu
 
Nina imani wahusika wanausoma huu uzi na watafanyia kazi maoni yetu.
 
Hivi ni nani msimamizi wa elimu nchini Kati ya tamisemi na wizara ya elimu?
Huu mpango umetoka tamisemi na wizara husika ya elimu ipoipo TU kama haihusiki na masuala ya elimu vile!
Nijuavyo mtaaluma mkuu anatoka wizara ya elimu na ndiye mhusika mkuu wa masuala ya taaluma katika shule zote za nchi hii.
Tamisemi watuambie Kama na wao Wana mtaaluma mkuu na anahusika na shule za serikali pia! Kama hawana mtaaluma mkuu mamlaka ya kuwapangia walimu mambo ya kitaaluma wanayapata wapi?
Vingine serikali au mpanga wizara awaambie walimu ni nani hasa anayehusika na masuala ya taaluma na mwalimu anawajibika Kwa nani Kati ya wizara ya elimu na tamisemi?
 
Kuna ombwe katikati. Walimu bosi wao ni mkurugenzi (mtamisemi), wizara ya elimu inaishia vuoni. Ni kama vile zahanati na vituo vya afya vipo chini ya halmashauri wakati wizara ya afya ipoipo tu kama ulivyosema. Wanaounda hii mifumo sometimes wawe wanaangalia basi. Kah!
 
Tuwe na Mfumo mpya wa Elimu ili vijana wengi wanapohitimu vyuo wasisubiri kuajiriwa bali wawe na uwezo MKUBWA sana wa kujiajiri,hizi kalenda wanazoleta kwenye Elimu ni aina nyingine ya upuuzi tunaoendelea nao ambao hauna tija yoyote kwa nchi hii.hapo tunawatafulia watu ulaji tu,watu wamekaa wakaandaa hilo li kalenda wamepiga mpunga na wamesepa.Ss tunajadili upuuzi wa wapiga deal.
 
Mpango huu nimeukubali kabisa kabisa, walimu wamefungiwa speed controller! wakuu wa shule walikuwa wanawakoromea walimu..'nataka kufikia mwezi mei mada zote ziwe zimeisha'.. kwa sasa hicho kitu hakipo tena, safi kabisa!
 
Hii ndio naisikia,Nani ameleta mpango huu,yaan ufundishaji uwe sawa?!ina maana walimu wapo wa kutosha mashule,niufuatilie Kwanza nijue undan wake
 
Iko hivyo..! Kalenda ipo ila haitekelezeki
 
Ukifuatilia kwa karibu unaweza kuona aliyetoa mwongozo hajawahi hata kufundisha kipindi kimoja darasani, ila ametengenezewa connection tu na jamaa fulani akapewa post
 
Hilo la afya ya watoto tatizo sio muda mrefu tu wa kusoma bila kupumzika ni pamoja na watoto kukaa na njaa muda mrefu Kuna watoto wanatoka nyumbani bila kula chochote na wanashinda na njaa shule kutwa nzima kiafya ni tatizo kubwa
 
Siasa ikiingia kwenye taaluma ni hatari. Hili wazo liboreshwe kwa upande mwingine lina faida kubwa sana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…