Elimu ilianzia ikulu ikapelekwa tandale na haikuanzia buza kuelekea ikulu.

Elimu ilianzia ikulu ikapelekwa tandale na haikuanzia buza kuelekea ikulu.

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
5,315
Reaction score
13,269
Habari wakuu.

Zingatia kichwa cha habari tajwa hapo juu, soma kwa kutafakari sababu huu uzi mfupi unakupa majibu kwanini elimu ya sasa licha ya kusoma mpaka chuo kikuu ila haimsaidii mtu mmoja mmoja asiye na ajira kujikwamua kiuchumi.

Kihistoria elimu ilianzia ikulu special for kings, prince and noble men kwaajili ya kuongoza nchi, ma prince walifundishwa historia za tawala zilizopita na sera za wafalme waliopita kisiasa na huu ndio ulikuwa mwanzo wa elimu.

Elimu ikavuka kuta za ikulu na kuwafikia wananchi kwa lengo la kuwafundisha kwa pamoja kilimo na sekta zingine ili serikali iongeze mapato na kuboresha huduma za kijamii kwa watu wote.

Haikulenga kumuinua mtu mmoja mmoja ililenga watu wote kupanua uzalishaji na kodi.

Elimu haikuanzia mtaani

Elimu ya kumkomboa mtazania au mwafrika inatafutwa na yeye mwenyewe haitafutwi shuleni ???

Nawasilisha
 
Naunga mkono hoja. Ukitaka kujua ukweli wa hilo angalia wanafunzi waluokuwa wanafaulu darasa la Saba miaka ya 90 halafu linganisha na wanaofaulu Leo hii.

Miaka ya 90 watu siyo kwamba hawakuwa na akili, hapana! Hakukuwa na shule nyingi ndiyo maana vigezo vya kufauli vilikuwa vigumu. Tunakoelekea watu wote watafaulu mitihani ya ngazi zote za elimu kwa sababu shule ziko nyingi.
 
Uwezo wetu wa kuunda mfomo wa elimu utakaokuwa na manufaa Kwa Kila mtu ni mdogo na kuenda kujifunza Kwa wenzetu kama China au Irani hatutataki
 
Uwezo wetu wa kuunda mfomo wa elimu utakaokuwa na manufaa Kwa Kila mtu ni mdogo na kuenda kujifunza Kwa wenzetu kama China au Irani hatutataki
Huko china ndiko elimu ilipoanzia vilikuwa vinafundishwa vitoto vya mfalme wapwa mashemeji na wajomba za mfalme pekee wengine haikuruhusiwa kupata elimu.

Ukija korea utakutana na huyu mwamba anaitwa SEJONG

5686.jpg

Miaka ya 1400 huyu ndiye aliyeitoa elimu kutoka nje ya kuta za ikulu kwa kuanzisha alphabet zake za kikorea kutoka zile za kichina na akakumbana na uponzani mkali kutoka kwa familia na koo za kifalme noble men.

Alilenga kuwafundisha wakulima kilimo ili kuongeza mapato hakulenga kumuinua mtu mmoja mmoja
 
Back
Top Bottom