Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Ukiangalia kwa makini siasa za Afrika zinavyoendeshwa Kwa Sasa, unaweza kuona pasina shaka kuwa mserereko wa kurudi nyuma miaka 200 iliyopita ni mkubwa sana.
Kabla ya Mkutano wa Berlin ulioigawanya Afrika vipande vipande. Afrika yenyewe tayari ilikuwa imegawanyika kikabila na kiukoo.
Maarifa ambayo Kwa lugha nyepesi ndiyo Elimu, kwa upande wa Afrika yalikuwa chini Sana ukilinganisha na watu toka Asia, Arabuni ama ulaya..
Uduni wa Elimu yetu ndiyo uliosababisha tuwe na mifumo dhaifu ya kiutawala ambayo ilikuwa rahisi kushambuliwa na kutekwa/kuvunjwa na wavamizi toka Uarabuni, Asia na Ulaya.
Elimu yetu kuhusu Mungu na kuabudu ndiyo ilisababisha dini zetu kuonekana za "kishenzi" na mpaka leo athari na taathira zake zinaonekana kwenye maisha yetu ya Kila siku.
Kwa kuwa Elimu maana yake ni uwezo wa binadamu kutumia maarifa yake aliyonayo kutatua changamoto zinazomkabili, basi bila ya shaka Afrika imo hatarini kurudi utumwani.
Ukiwaangalia viongozi wa Afrika (pamoja na wale ambao hawakwenda Korea ya Kusini) jinsi wanavyojaribu kutatua matatizo ya nchi zao, unapata shaka kama wanayo Elimu inayohitajika kuwa viongozi.
Leo hii wakati mabara mengine yanasonga mbele kimaendeleo kwa kutumia maarifa mapya na ya zamani toka kwa watu wao, Afrika bado imeshikilia utambuzi wa Elimu kwa vyeti.
Mabara mengine mbali ya cheti ulichonacho cha kuthibitisha ulichosomea, kupata kazi ama kubakia kazini kunategemea zaidi tija unayoileta kwenye taasisi na siyo ukubwa wa cheti chako.
Mwenendo huu wa hali ya Mambo duniani, unaleta shaka kama Afrika tunayo Elimu ya kutosha kuzuia kuingizwa utumwani Kwa mara nyingine tena.
Uchaguzi wa Afrika ya Kusini ni ishara mojawapo kuwa Elimu ya Afrika ni duni Sana.
Waafrika ya kusini walipambana dhidi ya utawala wa wazungu walowezi wachache zama za ukaburu,. Leo wanapambana na waafrika weusi wenzao ili kuwarudisha wazungu madarakani.
Ukiwasikiliza Kwa makini wanaona waafrika wenzao hawana Elimu ya kuiongoza Afrika ya kusini kiufanisi. Lakini wao pia wananchi wa kawaida wameonekana hawana Elimu ya kutosha kuhusu umajumui (Pan Africanism) wa Afrika.
Elimu ni uwezo wa kutumia maarifa kutatua changamoto zinazokuzunguka na siyo uwezo wa kukariri ili kufaulu mitihani.
Kwa kuwa mabara mengine yanarudi kwenye msingi huu kuhusu Elimu, si ajabu kizazi hiki nacho kikaja kuzalisha kina Mangungo wa zama zetu.
Maana inawezekana tukawa na Rais Profesa lakini bado akawa anasaini mikataba uchwara kama alivyofanya Babu yetu Mangungo.