π₯ KELVIN HK
: CLIENTS KUNUNUA MATERIAL WENYEWE KWA HOFU YA KUIBIWA β HII MBINU IMEPIGWA NA WAKATI!
Kuna jambo ambalo nimekuwa nikiliona kwenye ujenzi mara kwa mara.
Mteja anamwambia fundi:
βMaterial zote nitanunua mimi. Sitaki kukupa pesa ya material kwa sababu naogopa utaniibia.β
Kwa mtazamo wa haraka unaona kama umepata suluhisho la wizi.
Lakini kama Building Master, sikubaliani na mfumo huu kama unatumika kama njia kuu ya kumdhibiti fundi.
Kwa nini?
π§± FUNDI ANAWEZA KUIBA HATA MATERIAL ZIKIWA MIKONONI MWAKO
Tusielewane vibayaβ
wizi ni wizi na hauna justification.
Lakini tatizo la ujenzi halitatatuliwa kwa kusema tu,
βMimi nitanunua material mwenyewe.β
Kwa sababu unaweza kuwa na cement, mchanga, kokoto na nondo zako site, lakini bado ukawa huna mfumo mzuri wa kuhakikisha material hizo
zinatumika kwa ufanisi na hazipotei.
Na hapa ndipo tunahitaji kuangalia mfumo mzima wa kazi.
π° MFUMO NINAOUPENDEKEZA
Fundi au mtaalamu amekufanyia makadirio:
Material = Tsh X
Ufundi = Tsh Y
Badala ya wewe kununua kila kitu mwenyewe kwa hofu ya kuibiwa, unaweza kufanya hivi:
Mkabidhi anayesimamia kazi bajeti iliyokubaliwa kwa material + ufundi, kwa masharti kwamba kazi inayokabidhiwa ni KAZI ILIYOKAMILIKA.
Hapo mtoa huduma anakuwa na wajibu mkubwa zaidi wa kusimamia matumizi.
Material ikipotea bila sababu, yeye ndiye anayepata presha ya kuhakikisha kazi haijasimama.
Material ikitumika vibaya, yeye ndiye anayebeba mzigo wa gharama za ziada kulingana na makubaliano yenu.
ποΈ MFANO MDOGO: UDONGO UNAODONDOKA WAKATI WA KUPIGA UJENZI
Hapa ndipo tofauti ya mfumo inaweza kuonekana.
Wakati fundi anajenga, udongo unaweza kuanguka chini.
Fundi makini ataokota na kuutumia tena pale unapofaa.
Lakini kwenye mfumo ambao mteja ndiye anayesimamia material zote, fundi anaweza kuona suala la material kama
βhilo ni la bossβ, hivyo umakini wa kupunguza upotevu unaweza kupungua.
Sio kwamba mafundi wote wako hivyo.
La hasha!
Kuna mafundi waaminifu na wazalendo sana.
Lakini mfumo mzuri unatakiwa kumfanya hata mtu asiye na umakini mkubwa awe na sababu ya kulinda material.
Kwa mfano, kama fundi amekabidhiwa kazi kwa makubaliano ya gharama ya jumla, atakuwa na motivation kubwa zaidi ya kuhakikisha:
β
Hakuna material inayopotea bila sababu
β
Material inatumika kwa kiwango kinachotakiwa
β
Kazi inafanyika kwa mpangilio
β
Hakuna kurudi dukani mara kwa mara kununua material iliyotumika vibaya
β
Bajeti haivuki bila sababu ya msingi
Kwa lugha rahisi:
π Mteja asijenge mfumo unaomfanya fundi aseme,
βMaterial ni za boss, mimi nimepewa hela ya ufundi tu.β
Badala yake, tengeneza mfumo unaomfanya anayesimamia kazi ajisikie kuwa
matokeo ya kazi ndiyo wajibu wake.
β οΈ LAKINI HAPA KUNA JAMBO MUHIMU!
Usimpe mtu pesa kwa sababu tu amesema:
βNipe hela zote, mimi nitamaliza.β
Huo nao ni ujinga mwingine.
Lazima kuwe na:
π Makubaliano ya maandishi
π BOQ/mchanganuo wa material
π Viwango na quantities zinazoeleweka
π Hatua za malipo
π Scope ya kazi iliyo wazi
π Ukaguzi wa kazi unaoendelea
π Risiti/uthibitisho wa manunuzi pale inapohitajika
π Makubaliano ya nani anawajibika endapo material au fedha itapotea
Usimamizi mzuri wa ujenzi sio kumficha fundi material.
Ni kuweka
mfumo wa uwajibikaji.
π₯
CLIENTS, kama unaogopa fundi atakuibia, usikimbilie tu kusema βmimi nitanunua material zote.β
Jiulize kwanza:
βNimeweka mfumo gani wa kumfanya anayesimamia kazi awajibike kwa material, fedha na matokeo ya kazi?β
Hapo ndipo tunaanza kujenga kwa akili.
UFUNDI NI MAELEWANO.
THE BUILDING MASTER ποΈ
π
Call & WhatsApp: 0789005562
π
Ramani natoa Bure β utalipia mchanganuo wa gharama na vipimo.
π Kwa elimu zaidi ya ujenzi, ramani, makadirio na ushauri wa ujenzi, jiunge na group letu la WhatsApp:
#BuildingMaster #Ujenzi #UjenziWaNyumba #ConstructionTanzania #UshauriWaUjenzi