Entareyehirungu
JF-Expert Member
- Oct 27, 2006
- 488
- 471
Kuna kambi kuu mbili juu ya nadhari la chimbuko la ujasiriamali. Kambi ya kwanza inaamini ujasiriamali ni hali au sifa mtu anazaliwa nazo wakati kambi ya pili inaamini kwamba mtu yeyote anaweza kuwa mjasiriamali na hivyo ujasiriamali siyo jambo la lazima iwe hali au jambo la kuzaliwa nalo.
Katika mjadala wetu: Je, Kuna Umuhimu wa Kuandika Mchangamanuo/Mpango wa Biashara?hoja hii ya jasiriamali kama hali ya kuzaliwa nayo au kufundishika imejitokeza sana katika michango ya washiriki. Naomba kwa idhini yenu CONSULT, Kubota, Makirita Amani, Mrimi, Malila, Mvaa Tai, MILLIONS MOVEMENT, Mama Joe, Innocent Prince, Chasha, tuipe hii hoja mjadala wake rasmi hapa.
Mtagundua kwamba katika kichwa cha habari TABIA haijaorodheshwa. Nimefanya hivyo maksudi ili kupunguza upana wa eneo la mjadala na kutaka tujikite katika kuichambua nadharia ya kambi moja tu kwanza "UJASIRIAMALI KAMA JAMBO LINALOFUNDISHIKA"
Ili mtu afanikiwe katika nyanja yake ya Biashara kijasiriamali, anahitaji maarifa gani? Elimu kubwa kiasi gani inahitajika? na ni ujuzi upi ni muhimu kwake kufikia mafanikio?
AU kwa namna nyingine:
Elimu, Maarifa na Ujuzi vina nafasi gani katika kuchangia kumfanya mtu kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio?
Karibuni kwa mjadala