PrinceZuko
New Member
- Aug 26, 2022
- 2
- 1
Nina rafiki yangu ninamfahamu tunaishi naye mtaa mmoja, nimecheza naye mpira mara nyingi sana mtaani kwetu, nakiri kusema kuwa katika watu niliowahi kucheza nao mpira pengine yeye alikuwa ndiye mwenye kipaji kikubwa zaidi kuwahi kukishuhudia.
Alikuwa anafanya vitu basic kwenye mpira kwa ufasaha sana, pasi zake hazikuwa kama zetu, pasi zake zilikuwa za ufundi kweli kweli. Mikimbio yake na utafutaji nafasi uwanjani ulikuwa sio kama sisi wengine, alikuwa ni mchezaji wa daraja la juu kuliko sisi na wengi tulimtabiria kufika mbali na kwa kuwa ndoto yake ilikuwa ni kucheza soka basi tuliamini hatokuwa na miaka mingi pengine tungemuona ligi kuu.
Sijui ilikuwaje kwa maana shule na elimu zilitutenganisha kwa hiyo sikufuatilia sana maendeleo yake ingawa nilisikia kuna kipindi alikwenda kwenye moja ya vilabu ligi kuu kwa ajili ya majaribio.
Nina ndugu yangu mwingine wa damu kabisa, yeye ni msanii wa muziki aina ya rap mnaweza sikiliza kazi zake hapa Audiomack | Free Music Sharing and Discovery ni msanii anayejitafuta lakini unaweza kugundua kabisa ana kipaji kikubwa kwa kiasi gani! Tumemtabiria na kumsifia sana kuwa siku moja atakuja kuwa msanii mkubwa na kipaji chake kitampa kipato ambacho kitamsaidia yeye, familia yake, na taifa kwa ujumla.
Hawa wote wawili niliowataja hapo juu ni mifano tu michache kati ya mifano mingi kama hiyo kwa kuwa kama taifa tuna vijana wengi sana wenye vipaji tofauti tofauti na wengi wao wanatamani kujenga career zao kupitia vipaji vyao. Lakini tumewataka wasome! Si sawa!
Sina maana kuwa elimu haitawasaidia, hapana hata wenye vipaji wanahitaji elimu, tofauti inakuja kwenye mifumo ya elimu ambayo itasapoti michezo na sanaa na kuzalisha ajira kupitia wasanii na wana michezo wasomi. Kivipi?!
Kama nilivyoeleza kwenye makala yangu ya awali ya ELIMU NA UKOMBOZI WA AJIRA na makala hii tuichukulie kama sahemu ya pili au muendelezo wa makala ya kwanza kwa sababu haitofautiani sana
1. Mfumo wa elimu uunganishwe na mfumo wa michezo katika ngazi zote za kitaifa. Napongeza sana serikali ilipoanzisha mashindano kama UMISETA na UMITASHUMTA, lakini naona kama lengo lao lilikuwa ni kujenga afya za wanafunzi tu lakini sio kutafuta wanamichezo watakaojiajiri kupitia vipaji vyao. Inabidi ratiba za michezo zinazotambulika na wizara husika ziingizwe ndani ya ratiba za shule zote na vyuoni, kuwe na timu za shule za umri tofauti katika michezo tofauti na michuano inayotambulika na wizara. Ili watoto hawa waweze kupata nafasi ya kuwa katika timu zao za shule. Kuwe na vigezo ambavyo vitaangalia kipaji chake na pili vitaangalia ufaulu wa masomo yake, nikiwa na maana wanafunzi hawataingia kwenye timu zao kwa kutegemea vipaji vyao tu bali na ufaulu wao wa masomo.
2. Kuwe na scholarships kwenye shule zinazosifika sana kwa michezo fulani, kama kwenye elimu ya afya kusoma chuo cha Muhimbili (MUHAS) ni sifa kubwa vile vile hata kwenye michezo inaweza kuwa hivyo, shule nyingi za michezo lakini ufaulu wako utakupeleka kwenye best schools zilizobobea kwenye michezo hiyo. Kutoka sekondari kwenda vyuoni pia kuwe na scholarships za michezo kwa wanafunzi wenye vipaji husika.
Kuwe na mtindo wa drafting kutoka kwenye vilabu mbali mbali wakiangalia wanafunzi kutoka A level kupitia michuano ya kimichezo inayotambulika ki serikali. Na hata vipaji vya mtaani lazima viingizwe kwenye mifumo ya shule ili kupata nafasi ya kuonekana na vilabu. Hapo tunatengeza wanamichezo wasomi na fursa ya kuajiriwa itatokana na elimu pia.
3. Elimu ya muziki na uigizaji pia iangaliwe ambapo wanafunzi wenye vipaji wanaweza kupewa scholarship na hata mashindano ya kusaka vipaji yanaweza kuanzia mashuleni na vyuoni kwa ratiba na utaratibu unaotambulika na serikali na wadau.
Elimu yetu tukiunganisha nguvu na sanaa na michezo tunajenga mfumo mzuri wa kufanya elimu iwe njia ya ajira kupitia michezo na sanaa. Mifumo mizuri pia iwekwe kwenye sanaa ili kufanya sanaa iwe ajira kweli.

Upvote
1