Elimu Tanga Kunani?


Na mimi nilivyosoma nilijiuliza mwenyewe. Nashukuru kwa kuliweka wazi watu walione.
 


Unachosema kuwa Lushoto eti imetengwa kimaendeleo sio kweli. katika mkoa wa Tanga ukiacha jiji Lushoto ndio wilaya yenye uchumi mkubwa kwa kipato cha Mwananchi mmojammoja. Lakini pia ni moja ya wilaya zilizoendelea nchini. kuhusu Lushoto kutoa shule mbili mbovu au tatu ni tatizo la kimfumo. Kama ulivyosema, shule hizi ni za kata ambapo utakuta shule ina Mwalimu mmoja utegemee nini? lakini pia ukumbuke kuwa Lushoto kwa mkoa mzima wa Tanga ndio ina shule nyingi. Hivyo hii inaonyesha kuwa kuna shule nyingi zimefunguliwa kiholela au kwa mashindano ya kila kijiji kuwa na shule yake. Hili ni tatizo.
 
Tanga ni mkoa pekee ktk nchi hii wenye aina zote za hali ya hewa ndo maana karibu mazao yote ya biashara kama katani (korogwe, lushoto), kahawa (lushoto) chai, iliki,nk na ya chakula kama mahindi, maharage, ndizi yanastawi tanga. Shida hakuna uzalendo wa kimkoa wapo viongozi na wafanya biashara wengi na hawataki kuwekeza nyumbani kwao, ni wasaliti. Mfano mkoa mmoja ambao ni kati ya mikoa midogo nchini kilimanjaro una shule nyingi za sekondari kuliko kanda nzima ya magharibi tabora,shinyanga, kigoma na katavi.
-- lazima wazawa mbali na serikali wawe na uchungu na nyumbani, na huo sio ubinafsi bali ni uchungu wa kimaendeleo
 
Suala limeulizwa kielimu sasa linapelekwa kimkoa dah,mimi wa Tanga na nilifaulu vizur tu cha kufanya vijana na wazee wa Tanga bado hawajaona umuhimu wa elimu kijana kufaulu either ni juhudi binafsi au katoka familia yenye watu waliosoma kidogo,hapo ndipo tatizo lilipo maana kama ni starehe hakuna kwenye starehe kama Dar,Arusha na Moshi kwa mikoa niliyofika TZ hii
 

Kwenye red, usiamini habari za jeshi, hasa la CCM. Tumesikia mara ngapi Mwigulu anawasingizia wapinzani kuwa wameingiza silaha! Mabomu eti ni ya wapinzani! Aliyekwenda kuungama !!!!???.na sijui iliishia wapi? Nchi hii! ya CCM
 
Hivi Ndalichako bado katibu mkuu pale NECTA ama.....bado siielewi hiyo orodha ya hao kumi bora aisee!!
 
Tafadhali mkuu,hapo kwa Mzee Yusufu kuna ka-chumvi kidogo.
Maana haiwezekani kabisaaa
 

kula gwala kamanda
 
Kwani mikoa mingine haina shule za kata,za serikali?
Shule za kata zimeenea nchi nzima.
Tukubaliane kuwa mwamko wa elimu mkoa wa Tanga bado upo chini.
Baada ya kulitambua na kukubaliana na hilo ndio tukae kutafuta sababu za mwamko wa elimu kuwa chini.
Hakuna haja ya kukashifiana na kutukanana huku tukibeza ukweli.
 

Tatizo sio uislam kama wengine wanavyodai tatizo ni serikali yenyewe imeshindwa kuzisimamia izi shule na mikoa mingi ya pwani 6oka uhuru ilinyimwa kipaumbele katika kila nyanja alafu watu wanasema hawataki kusoma wakasome wapi sasa na shule amna. Hii nchi misingi iliyojiwekea tokea uhuru kuna watu hawatakiwi kushika nyadhifa serikalini sasa kikwete anajaribu kutoa huu ndo haya leo yanayomkuta sababu anawapa elimu watu ambao hawaruhusiwi.
 
Uzuri wa mada kama hizi unasaidia kuonesha kuwa wengi wetu tu weupe.

Badala ya watu kuja na uchambuzi, wanaleta porojo na upuuzi.

Binafsi naishi Tanga na naamini Tanga siyo ya mwisho kielimu na kiuchumi. Ila katika ujumla wake, serikali ya CCM imeharibu elimu na sekta nyingine za huduma ya jamii. Kwa hali ya sasa, mkoa wowote unaweza kuwa wa mwisho. Ndiyo maana hao NECTA hawawezi kuthubutu kutuwekea matokeo kwa mchanganuo na uchambuzi unaoeleweka (mfano, private Vs government schools na trends ya kila mkoa)!
 

Unaweza kutupa takwimu (for the past 5 yrs) kuthibitisha hayo?
 
muulizeni yule mtu anayetaka kuwa Rais na huku akishinda kwenye mitandao,cha kushangaza hata wana Tanga wenyewe hawajui mitandao
 

Babu DC, you might be right to some extent, but there are tradition that can not be denied! Look, Tanga Elimu ahera is over and above Elimu dunia. Nakubali kila mkoa unaweza kuwa wa mwisho lakini kwingine kuna vichocheo kuliko kwingine!
 
ndo kambi imara ya c.c.m,mnyime mtu elimu umtawale
 
Babu DC, you might be right to some extent, but there are tradition that can not be denied! Look, Tanga Elimu ahera is over and above Elimu dunia. Nakubali kila mkoa unaweza kuwa wa mwisho lakini kwingine kuna vichocheo kuliko kwingine!


Nitashukuru na kufurahi kama atajitokeza mtu na takwimu kutuonesha kuwa mkoa wa Tanga kweli unashika mkia kielemu. Miaka ya hivi karibuni, Shinyanga ilikuwa ya mwisho na pia kuna kipindi Kagera ilikuwa karibu na mwisho.

Zaidi ya hapo, ni jambo la kutumia nafasi (one time event) kuuponda mkoa wa Tanga. Hivi kuna mkoa Tanzania ambao hauna mila au tamaduni ambazo wengine tunaziona hazifai? Kama upo naomba kutajiwa!!
 
Unajua madhara ya comment yako ya kuweka kila kitu kwenye kapu moja?

Kwa nini usitupe takwimu za miaka 50 iliyopita kuonesha jinsi Tanga ilivyoshindwa kuwekeza kwenye elimu?

kwanini wewe usitoe hizo takwimu?au unataka kutafuniwa kila kitu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…