Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shule 10 za mwisho ni;
Manolo mkoa wa Tanga
Chokocho mkoa wa Pemba
Kwalugulu mkoa wa Tanga
Relini mkoa wa Dar es salaam
Mashindei mkoa wa Tanga
Njelekela Islamic Seminary mkoa wa Kigoma
Vudee mkoa wa Kilimanjaro
Mnazi mkoa wa Tanga
Ruhembe mkoa wa Morogoro
Magoma mkoa wa Tanga.
Mleta uzi nahisi huijui vizuri tanga. Ukiangalia vizuri hizo shule
1.Nyingi au tuseme karibia zote ni za WIALAYA YA LUSHOTO
2.Nyingi ni SHULE ZA KATA
3.Wilaya ya lushoto iko nyuma si tu kielimu lakini kwa mambo mengi tu mf.miundo mbinu ya barabara,maji safi na salama
3.Wakazi wake wengi ni wa asili ya wasambaa/wapare(hawa wamechanganyia na usambaa) ,historia ya maendeleo "ILIWATENGA" tangu zamani, tangu tupate uhuru kuna vijiji huko havijawahi kupata umeme,maji safi nk. Ni sawa na ile mikoa ya kusini "ilivyotengwa "kihistoria.
4.hali ya hewa ya lushoto ni nzuri MNO kama tu uwekezaji mzuri ungefanyika kwa upande wa serikali ,kwa kulijua hilo wajasiriamali wa shule binafsi wamekamata fursa na shule zao zilizoko lushoto zinafanya vizuri mno kama KIFUNGILO,MAZINDE JUU,SONI SEMINARI na kuna shule moja ya wakorea jina limenitoka kidogo.
kwa hiyo TUSIHUKUMU KWA KUANGALIA ATHARI(EFFECTS) Tuangalie CHANZO , kusema kuwa ni watu wa imani fulani wanakaa huko basi ndo mana wanafeli itakuwa HATUJATENDA HAKI , ieleweke kuwa ENVIRONMENTS AFFECT LEARNING. Na tunapozungumza ENVIRONMENT tunazungumza dhana pana zaidi ,
Tuache chuki na kejeli, tujadili kihoja sio kichafua hali ya hewa,haitusaidii kujenga chuki za kidini kati yetu......
Sioni suala la imani hapo; anyway, mwendawazimu huwezi kumzuia kufanya chochote akiamua; hata kuvua nguo hadharani ni kawaida kwa mwendawazimu. Je, si kweli kwamba Tanga imeboronga? Je, si kweli kwamba magaidi wamefurumushwa huko Tanga jana kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Jeshi? Je, si kweli kwamba Tanga ndio mkoa unaoongoza kwa kuichagua CCM kwa mtindo wa kimbunga? Je, si kweli kwamba mganga wa kienyeji kuotoka Tanga ni Mbunge? Tanga ina tatizo na lisiposhughulikiwa litaisumbua sana nchi huko tuendako.
Tanga, mkoa wangu niupendao... Inanisikitisha sana. Kuna siku nilikwenda mkutano wa Kinana pale Tangamano. Nakumbuka wakati Kinana anahitimisha na kutoa shukran kwa mahudhurio aliuliza siku akirudi Tanga, awafanyie nini watu wa Tanga kama shukrani? Amini usiamini, pamoja na matatizo yaliyopo kila sekta Tanga, wao walipiga kelele waletewe Mzee Yusuph wa taarab. Siku ile mpaka leo sitahisahau.
Mkuu hakuna aliyesema Tanga haina mazuri; yapo sana tu; lakini mazuri hayo hayaondoi ukweli kwamba Tanga safari hii kitaaluma imechemsha. Turudi kwenye suala la ugaidi, kama kweli ilikuwa ni issue ya kutengeneza unadhani kwanini fabricators waliamua kucheza sinema yao Tanga? Waliona Tanga ni mandhari inayoendana na igizo lao.
Nyinyi makafir nguruwe wanaharibu akili ndo maana akawa haram sasa unalinganisha shule zilizofanya vizuri za private na zilizofanya vibaya za kata kuna uwiano hapo kweli izo shule zilizoongoza ni zakulipia kwa nini usiweke za serikali kwa serikali na private kwa private tupate uwiano. Alaf izo zilizoongoza za pwani ujasema kama wakazi ni waislam. Acha chuki za kijinga
Kwani mikoa mingine haina shule za kata,za serikali?
Shule za kata zimeenea nchi nzima.
Tukubaliane kuwa mwamko wa elimu mkoa wa Tanga bado upo chini.
Baada ya kulitambua na kukubaliana na hilo ndio tukae kutafuta sababu za mwamko wa elimu kuwa chini.
Hakuna haja ya kukashifiana na kutukanana huku tukibeza ukweli.
Kwani mikoa mingine haina shule za kata,za serikali?
Shule za kata zimeenea nchi nzima.
Tukubaliane kuwa mwamko wa elimu mkoa wa Tanga bado upo chini.
Baada ya kulitambua na kukubaliana na hilo ndio tukae kutafuta sababu za mwamko wa elimu kuwa chini.
Hakuna haja ya kukashifiana na kutukanana huku tukibeza ukweli.
Uzuri wa mada kama hizi unasaidia kuonesha kuwa wengi wetu tu weupe.
Badala ya watu kuja na uchambuzi, wanaleta porojo na upuuzi.
Binafsi naishi Tanga na naamini Tanga siyo ya mwisho kielimu na kiuchumi. Ila katika ujumla wake, serikali ya CCM imeharibu elimu na sekta nyingine za huduma ya jamii. Kwa hali ya sasa, mkoa wowote unaweza kuwa wa mwisho. Ndiyo maana hao NECTA hawawezi kuthubutu kutuwekea matokeo kwa mchanganuo na uchambuzi unaoeleweka (mfano, private Vs government schools na trends ya kila mkoa)!
Babu DC, you might be right to some extent, but there are tradition that can not be denied! Look, Tanga Elimu ahera is over and above Elimu dunia. Nakubali kila mkoa unaweza kuwa wa mwisho lakini kwingine kuna vichocheo kuliko kwingine!
Unajua madhara ya comment yako ya kuweka kila kitu kwenye kapu moja?
Kwa nini usitupe takwimu za miaka 50 iliyopita kuonesha jinsi Tanga ilivyoshindwa kuwekeza kwenye elimu?