Nitashukuru na kufurahi kama atajitokeza mtu na takwimu kutuonesha kuwa mkoa wa Tanga kweli unashika mkia kielemu. Miaka ya hivi karibuni, Shinyanga ilikuwa ya mwisho na pia kuna kipindi Kagera ilikuwa karibu na mwisho.
Zaidi ya hapo, ni jambo la kutumia nafasi (one time event) kuuponda mkoa wa Tanga. Hivi kuna mkoa Tanzania ambao hauna mila au tamaduni ambazo wengine tunaziona hazifai? Kama upo naomba kutajiwa!!
Mkuu. Mkoa wa Tanga (nadhani mikoa ya pwani kiujumla excluding Dar es Salaam, but including kisiwa cha Pemba) unahitaji uhamasishaji kuhusu elimu kwani FACTs zinasema kuna tatizo.
Kwa haraka haraka tu. Ukiangalia takwimu* za matokeo ya kidato cha nne kati ya mwaka 2010 hadi 2012, inaonyesha hali ni mbaya sana mkoa wa Tanga. Kati ya mwaka 2010 hadi 2012, asilimia 66% (wastani) ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne walipata division 0 kila mwaka. Yaani, wanafunzi 13705 (mwaka 2010), 13742 (mwaka 2011), na 17474 (mwaka 2012) walifeli mtihani wa taifa, na idadi yao kati ya watihaniwa wote ilikuwa 61%, 62%, na 76% respectively. In fact, ukijumlisha wale waliopata Divisheni 4 (ambayo kwa maoni yangu nao hawakufaulu kwa viwango vya kimataifa), idadi inakuwa, kwa miaka ya 2010, 2011, na 2012 asilimia 85%, 85% na 95% ya wanafunzi wote wa mkoa wa Tanga 'walifeli' kidato cha nne. (*Takwimu zimetolewa katika
ripoti ya maendeleo ya mkoa wa Tanga)
Pia kwa kutolea mfano mwaka 2012. Inaonekana mkoa wa Tanga ulikuwa na idadi nyingi ya shule zilizofanya vibaya zaidi katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne. (Kwa maoni yangu mikoa ya pwani kiujumla inawaangusha wanafunzi wake).
Nadhani kuna haja wa serikali kuweka 'marshall plan' kwa ajili ya elimu ya mikoa ya pwani, la sivyo tutakuwa na tatizo kubwa sana huko mbeleni. Haya matatizo ya uhalifu tuliyosikia jana huko Tanga, yanaweza shamiri zaidi tusipotatua tatizo la elimu katika hiyo mikoa.